Didmus Wekesa Barasa Mutua

Parties & Coalitions

  • Not a member of any parties or coalitions

All parliamentary appearances

Entries 441 to 450 of 471.

  • 29 Mar 2018 in National Assembly: Kenya imekuwa nyuma katika hali ya kiteknolojia. Sasa tutakuwa na mwamko mpya na polisi watakuwa na uwezo wakuwafuata wahalifu wanaotumia mitandao. Naomba kuwa tunapopitisha sheria hii lazima polisi pia wawajibike kwa sababu mara nyingi wamekuwa na mazoea ya kusema kwamba hawawezi kutekeleza sheria kwa kuwakamata wahalifu. Wanasema kwamba hakuna sheria ambayo inawaruhusu ama labda wakipeleka ushahidi hautoshi kwa sababu sheria hairuhusu ule ushahidi kutumika. Sasa lazima polisi wawajibike. Wakenya hawatavumilia tena visingizio ambavyo si vya muhimu sana. Hii sheria ikipitishwa watampambana na majangili. view
  • 29 Mar 2018 in National Assembly: Pia ni jambo muhimu kwa Mkuu wa Polisi, Inspekta Generali mwenyewe ajitahidi kuhakikisha ya kwamba maafisa wa usalama wanapelekwa kwa mafundisho yatakaowapatia ujuzi wa kupambana na uhalifu wa teknolojia. view
  • 29 Mar 2018 in National Assembly: Kama Bunge la Kitaifa, tunapojiandaa na kujitahidi kupitisha huu Mswada, lazima polisi waanze kujipanga katika mafunzo na kwa kujua teknolojia za kisasa ili tupatie nafasi nzuri sheria hii. Nawarai Wabunge wenzangu tuipitishe kwa sababu ni sheria muhimu sana ambayo itahakikisha polisi na majasusi wetu wanatumia mbinu za kimataifa za kupambana na uhalifu wa teknolojia ambao umekua ukiongezeka kila wakati. Vile vile, naomba washikadau kwamba tunapopitisha hii sheria, lazima pia wawe wakitafuta mafunzo kutoka nchi ambazo zimeendelea kama Malaysia na Marekani ili kujua jinsi tekinolojia imewasaidia. Hiyo itatusaidia kupunguza uhalifu hapa nchini. Vile vile, ningependa kuchukua nafasi hii kuwaambia Wakenya ambao ... view
  • 27 Mar 2018 in National Assembly: Thank you, Hon. Speaker. I would like to comment on the first Petition by Dr. Nyongesa. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor. view
  • 27 Mar 2018 in National Assembly: I would like to make it very clear that the only way of increasing engineers in this country is for people to go to school and study engineering. I speak as an engineer. Engineering is not like medicine whereby once you go to the university, you acquire the title. I am an engineer, but I have not reached the level of calling myself an engineer. There is no shortcut. If you want to be an engineer, you have to go to the university and study. We must be very careful about trying to repeal the Act to pave way for ... view
  • 15 Feb 2018 in National Assembly: Thank you, Hon. Speaker, for giving me this opportunity. I just want to say that, as a House, we are setting a very bad precedent. It is not just about the Reports that we need, but we need concrete and detailed reports. Every member is aware that these Committees were constituted a few weeks ago and members need time to read these Bills. These are very important Bills. We are not just going to push the Members to bring here half-baked The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can ... view
  • 15 Feb 2018 in National Assembly: reports that they have not done enough research on. We should not blame the chairmen and members because they need time to read these existing Bills so that they are able to bring something that is very important and that is going to guide the members in debating and passing quality laws for this country. That is all I wanted to say. We should give them time to read and do proper research and bring quality reports for us to debate. Just pushing them is setting a very bad precedent. view
  • 14 Feb 2018 in National Assembly: Asante sana Mhe. Spika kwa kunipatia hii nafasi ili nami niweze kuchangia hii Hoja kwa kupitisha Ripoti ya Kamati ya Uteuzi. Kwanza, ninaunga mkono tupitishe hii Ripoti. Pili, ninaomba tusibadilishe hata koma bali tuipitishe tu vile ilivyo. view
  • 14 Feb 2018 in National Assembly: Mhe. Spika, ukiangalia historia ya nchi ya Kenya, mipaka yake ilikuwa na usalama na imara zaidi wakati Waziri wa Mambo ya Usalama wa Nchi za Nje, Mhe. Njenga Karume, alikuwa kwenye usukani. Wapo wale wanaosema kuwa masomo ya Mhe. Njenga Karume alipata kwa kukaa na wasomi tofauti kwa sababu sio lazima uende shuleni ili upate masomo ama tajriba ya kuendesha mipango nyingi ya Serikali. Unaweza kukaa na daktari na uanze kufikiria kama daktari na pengine huenda ukapata ujuzi wake. Unaweza kukaa na mawakili na uwe na ujuzi wa kuelewa sheria za barabara na sheria zingine tofauti zilizoko katika nchi ya ... view
  • 14 Feb 2018 in National Assembly: Wapo Wakenya wengi sana ambao hivi sasa wanaishi na matumaini kwa kufuatia uteuzi wa Rashid Echesa Muhamed kwa sababu wanafikiria kwamba hata kama unatoka katika familia maskini ama isiyojiweza, familia ambayo wazazi wako hawajulikani angalau tu na chifu wa eneo lako ama mtaa ambao nyinyi mnatoka, unaweza kuwa Rais, Waziri wa nchi ama mtu ambaye utakuwa na umaarufu zaidi na kujenga jina hilo. Ningependa kuambia marafiki zangu wa mrengo wa Upinzani kuwa sasa hivi kuna mwamko mpya katika nchi ya Kenya kwa sababu vijana wale hawakuwa wanajulikana kwa jina wameweza kufika, hata wameweza kuwa Mawaziri. Wale watu ambao familia zao ... view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus