All parliamentary appearances
Entries 31 to 40 of 105.
-
25 Apr 2012 in National Assembly:
Kuhusu swala la Mombasa Republican Council (MRC), nataka nieleweke vizuri. Ilitushangaza jana kwamba Rais alisimama na akataja MRC, ambayo ni baadhi ya makundi ambayo yanajaribu kujiunda katika hii nchi. Swala la KAMATUSA halikuwa muhimu kwa Rais kuliongelea. Swala la GEMA aliona si muhimu; lakini MRC ambalo leo ni kundi ambalo limekuwa katika midomo ya Wakenya na hata Serikali, aliona muhimu aongee. Kundi hili linakutana kila mara na Mkuu wa Mkoa. Limekutana na Waziri wa maswala ya ndani ya nchi na wamejadili mambo kadha wa kadha. Jambo linalotushangaza bali na lile la kujitenga kwa Pwani na ambalo si mjadala wa viongozi ...
view
-
25 Apr 2012 in National Assembly:
Swala lingine ambalo ni muhimu pia kwa watu kulijua ni kuwa Serikali hii haijakaa kitako na kuangalia kikundi cha MRC na viongozi wake ambao pengine hawajachaguliwa na wananchi wakichukua uwezo wa kuendesha shughuli za Pwani. Sisi kama viongozi waliochaguliwa tumejaribu sana. Miaka mitatu iliyopita, sisi kama Wabunge wa Pwani tulikutana na Rais wa Jamhuri hii na Waziri Mkuu na tukawaelezea maswala kuhusu ardhi, uajiri wa wafanyakazi katika mashirika ya umma na wizara mbablimbali za Serikali. Pia tuliongea kuhusu watu ambao wamefutwa kazi ambao wako na uwezo wa kufanya kazi. Lakini mfano mkubwa utaona hata leo katika magazeti kuwa Bw. Kijana ...
view
-
25 Apr 2012 in National Assembly:
Ningependa kuihimiza Serikali na sisi kama viongozi wa Pwani tuongee na kuona tutajadili vipi swala la MRC. Tusije kuwalaumu kwamba wanasema Pwani si Kenya; pengine swala lao lingekuwa: Kwa nini Pwani si Kenya? Hii ni kwa sababu hawa watu wote ambao wameachishwa kazi Serikalini ni wakutoka Pwani, swala la ardhi na maswala haya mengine yote yanafanyika katika Mkoa wa Pwani. Tumeambiwa leo na hata Waziri mwenyewe amekubali leo kwamba barabara ya Namanga imetengenezwa, lakini aangalia Voi-Taveta Road. Hata ile barabara ambayo ilianzishwa mwaka jana, haina hata debe moja ya lami ambayo imemwagwa juu yake. Hayo ni maswala ambayo ni lazima ...
view
-
25 Apr 2012 in National Assembly:
Maswala ambayo nimeongea juu yake kama vile barabara, mipaka, ardhi na kadhalika ni maswala nyeti ambayo yanahitaji tuyajadili pamoja. Nikiunga mkono baadhi ya maswala katika Hotuba ya Rais, ningependa maswala hayo yatiliwe maanana na tushikane pamoja. Tusiwe kwamba makundi mengine katika Kenya yanahalalishwa na mengine yanalaaniwa kuwa haramu.
view
-
29 Feb 2012 in National Assembly:
Thank you, Mr. Speaker, Sir.
view
-
29 Feb 2012 in National Assembly:
Mr. Speaker, Sir, I beg to move that the Motion be amended as follows:-
view
-
16 Feb 2012 in National Assembly:
Ahsante Bw. Naibu Spika wa Muda. Pia ninataka kuchukuwa fursa hii kumpongeza Waziri wa Serikali za Wilaya kwa Mswada huu ambao tunachangia. Mengi yameongewa lakini pia mimi nitachangia kidogo ijapokuwa mimi ni mwana kamati wa kamati ambao kuanzia kesho itajihusisha na washika dau hili kupata maoni zaidi juu ya Mswada huu ambao uko mbele yetu. Ningependa kuongezea kwamba kama tumeamua kuwa na serikali za ugatuzi na kwamba tunapeleka mamlaka mashinani, basi tusipeleke mamlaka nusu nusu. Lazima viongozi watakao chaguliwa kama Gavana na wale wengine wapewe uwezo kamili hili waweze kutatua matatizo ambayo yamekumba watu wa sehemu tofauti tofauti kutoka uhuru. ...
view
-
3 Nov 2011 in National Assembly:
On a point of order, Mr. Deputy Speaker, Sir. Going by the mood of the House, could I request that the Mover be called upon to respond?
view
-
19 Oct 2011 in National Assembly:
Hoja ya nidhamu, Bw. Spika.
view
-
19 Oct 2011 in National Assembly:
Jambo la ya nidhamu, Bw. Spika. Swali la pili katika ratiba itakayofuata ni uteuzi wa Baraza la Mawaziri. Kama tunavyojua, Serikali yetu ni ya Mseto na kila mrengo wa Serikali hii ya Mseto huwateua Mawaziri wake. Ningetaka kupata mwongozo kutoka kwako: Tunajua kwamba, Waziri Mkuu anahusika na usimamizi wa Baraza lote la Mawaziri lakini hahusiki na uteuzi wote wa Baraza la Mawaziri. Je, atajibu maswali kuhusu suala hili kama msimamizi wa Baraza la Mawaziri ama kama mteuzi wa Baraza la Mawaziri ama katika mrengo wake wa Baraza la Mawaziri?
view