Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 11 to 20 of 272.

  • 2 Mar 2022 in Senate: Sen. Cherargei, amefanya research yake na kujua pesa imetoka mahali fulani na kuongezwa. Waziri akuje kwenye makao ya Kamati na kutueleza kinaga ubaga ni vipi hadi pesa ikaongezeka nani kwa sababu gani? Barabara hii itaisha lini ili tuweze kuisheherekea? Naunga Sen. Cherargei katika hii Kauli ametoa. Asante, Bw. Spika wa Muda kwa kunipa nafasi. view
  • 2 Mar 2022 in Senate: Asante, Bw. Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi. Wakongwe walio mashinani na wale ambao hawajabahatika ni watu walio na shida tofauti tofauti katika jamii na kaunti tofauti tofauti. Kwa hivyo, ni muhimu sana kuangalia masilahi ya watu hao popote walipo, hata iwe mashinani ambako tunawakilisha katika Bunge hili. view
  • 2 Mar 2022 in Senate: The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view
  • 2 Mar 2022 in Senate: Kwa mfano, kuna jamii za kuhamahama ambazo mimi nawakilisha katika Bunge hili la Seneti. Wazee na wasiobahatika katika jamii wanaishi katika sehemu ambazo hakuna network. Kwa hivyo, ni vigumu sana kuwafikia. Kama ilivyosemwa hapo awali, hata wazee wa “Nyumba Kumi” pia wako mbali na wazee ambao wanaishi katika sehemu hizo. Ni vigumu kwao kupata habari kikamilifu kuhusu yale yanayoendelea katika Jamuhuri yetu ya Kenya. view
  • 2 Mar 2022 in Senate: Kuna pesa ambayo wazee hupewa. Kule Tana River, wazee hukaa hata kwa miezi sita bila kupata pesa hizo. Utawahurumia ukijua mwendo wanaosafiri kwenda kwa benki ama posta. Ili kupata hiyo pesa kidogo, humlazimu mzee kusafiri kilomita nyingi katika sehemu ambazo barabara ni mbovu na hazipitiki haswa wakati wa mvua. Kuna mito ambayo huwa wakati wa mvua. Kwa hivyo, huwa vigumu kwa wazee hao kuvuka na kufika katika sehemu za kupata pesa zao. Wazee hao wanafaa kufikiwa mahali waliko. Mzee wa miaka 70 au 80--- view
  • 2 Mar 2022 in Senate: Acheni niwaeleze jambo: Wazee kutoka jamii za wafugaji hawafi haraka kwa sababu wanakunywa maziwa na kula chakula cha asili. Hawatumii vyakula vya kemikali za siku hizi. Wengi wao huishi zaidi ya miaka 100. Wazee wa miaka zaidi ya 90 au 100 wakiwa mbali na pahali ambako kuna huduma, basi wao hupata shida. Kunafaa kuwa na sheria ili wazee hao wafikiwe mahali walipo. Hiyo itasaidia watu sana hasa wakongwe. view
  • 2 Mar 2022 in Senate: Bw. Spika wa Muda, unafahamu vizuri kuwa wakongwe ni mbegu na sisi ni mazao. Sisi tumetoka kwa wazee. Ikiwa tutaacha mbegu zetu vibaya, basi tutakuwa na jamii ambayo haina mwelekeo. Wengi wetu tulizaliwa na hao wakongwe. Wengine wetu tumebahatika kusoma. Wengine wetu ni Wabunge na wengine wanafanya kazi sehemu tofauti tofauti duniani. Baadhi ya watu wako nje ya Kenya. Ni vizuri kuangalia mbegu ambayo ilituleta. Mbegu hiyo ni wale wakongwe. Tukiwa na sheria mwafaka jinsi Hoja hii inavyopendekeza, basi sisi tutakuwa jamii ambayo inajali maslahi ya watu wasiobahatika na wakongwe ambao wako sehemu tofauti tofauti. view
  • 2 Mar 2022 in Senate: Kuna wakati nilienda uzunguni. Huko kuna sehemu zilizotengwa na zinajulikana kama homes for old people. Inamaanisha kwamba kuna mahali ambapo wazee wametengewa. Serikali inawashughulikia kwa kuwapa pesa, kuwapelekea madaktari na kuwapa lishe. Kwa hivyo, wako katika hali sawa. view
  • 2 Mar 2022 in Senate: Sijui kama hilo linawezekana hapa Afrika kwa sababu ukipeleka wazee mahali moja, wanaweza kukataa wakidhani kuwa wanaenda kutupwa kama takataka. Tukipendekeza kuwa na makao ya wazee, vijana wengine ni vichwa maji. Wanaweza kubeba wazee kwa lori na kuwapeleka huko. Pengine hiyo inafaa kuwa tu kwa Wazungu kwa sababu haitufai sisi. view
  • 2 Mar 2022 in Senate: Pia natoa wito kwa vijana na watu wengine walio na nguvu na waliobahatika. Kabla hatujasukuma Serikali kusaidia wazee, wao pia wanafaa kuangalia wazee. Kila mtu anafaa kushughulikia mzee wake. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus