Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 21 to 30 of 272.

  • 2 Mar 2022 in Senate: Bw. Spika wa Muda, wewe na mimi bado ni vijana lakini tuna vijana kule nyumbani. Tukipitisha sheria kama hiyo, siku ile tutakosa nguvu, basi tutalazimishwa kubebwa kwa magari na kupelekwa huko. Itasemekana kuwa wakati ukiwa Spika, view
  • 2 Mar 2022 in Senate: The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view
  • 2 Mar 2022 in Senate: ulipitisha sheria kuhusu wakongwe. Kwa hivyo, hutaweza kukataa. Wacha tujaribu kuitengeneza vizuri. Bw. Spika wa Muda, wewe ni mfugaji na ninajua kwamba wewe unajua maisha ya ufugaji vile inavyo kaa. Hebu angalia vizuri kama wewe ni mfugaji na umehama, na mzee leo hawezi hama na wewe, atakwambia mimi kichwa inaniuma, mara goti liko hivi. Kuna walemavu kadhaa ambao hawawezi kutembea kufika katika kituo cha pili mahali ambapo ng’ombe ama mbuzi zinaweza kuweka nanga zipate maji na nyasi. Itabidi wale ambao hawajabahatika kijamii wabaki katika sehemu ya mahame. Ukishawaacha katika hiyo sehemu ya mahame, basi utakua umepoteza watu muhimu. Kwa hivyo, ... view
  • 23 Feb 2022 in Senate: Mr. Speaker, Sir, I second. view
  • 14 Oct 2021 in Senate: Asante Bi Spika kwa kunipatia fursa hii. Suala la pending bills limekuwa dondasugu katika serikali za kaunti, hasa katika kaunti ambayo ninawakilisha hapa. Kila kona ya nchi hii, wananchi wazungumza juu ya pending bills . Kutolipwa kwa hizi pending bills kufanya watu wetu kuwa katika hali ya umaskini na ufukara. view
  • 14 Oct 2021 in Senate: Watu wengi walijidhamini na kuweka pesa nyingi katika miradi ya Serikali, lakini hawajui watalipwa lini. Sisi kama Maseneta wakati tunapozuru kaunti zetu, watu wengi ambao walifanya kandarasi ya Serikali wanatufatilia nyumbani wakisema ya kwamba, hali yao imedorora kabisa. Watoto wao hawaendi shule na umaskini umeongezeka. view
  • 14 Oct 2021 in Senate: The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view
  • 14 Oct 2021 in Senate: Wengine waliuza mifugo na mashamba yao ili kufanya kadarasi ya Serikali. Ni uchungu sana kwa sababu mpaka siku ya leo hawajapata pesa zao. Utakuta wengi wao wamekaa katika majengo au ofisi za kaunti wakidai pesa zao na hawajui watalipwa lini. Mambo haya ni mazito siyo ya kuchukulia rahisi. Ikiwa kandarasi ya Serikali itafanya watu wetu wakuwe maskini na wawe hohe hahe, basi watu hawataweze kuendelea kuishi katika hali hii ngumu iliyojaa shida na uchungu mwingi. Jambo hili linapaswa kuchukuliwa kwa uzito ili suluhisho la kudumu lipatikane. view
  • 14 Oct 2021 in Senate: Kuna wakati Bw. Ukur Yatani. Waziri wa Fedha, alisema pesa hizi zitalipwa na akatuma barua kwa kaunti zetu. Pesa zinafika kaunti zetu lakini watu hawalipwi. Ukiangalia nyuso za hawa watu zinaonyesha watu wanaoishi katika hali ngumu ya maisha. view
  • 14 Oct 2021 in Senate: Bi. Spika wa Muda, jambo hili linafaa kuchukuliwa kwa uzito na Serikali ya Kitaifa na serikali za kaunti. Ni lazima watueleze ni kwa sababu gani watu ambao walifanya kandarasi za Serikali hawajawahi kulipwa. Magavana waeleze ni kwa sababu gani watu hawalipwi pesa zao na ilhali kila mwaka pesa hupelekwa katika kaunti zetu zote. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus