14 Oct 2021 in Senate:
Sisi tunatoa wito na kuisihi Kamati itakayoshughulikia suala hili, ichunguze kwa makini na waweze kuja na suluhisho ya kudumu. Tuko katika msimu wa pili wa ugatuzi ambao unakaribia mwisho wake. Kama watu hawajalipwa na Serikali iliyopita na bado
view
14 Oct 2021 in Senate:
zinarudikana katika kaunti zetu na wanaendelea kuisha katika hali ngumu ya maisha, watalipwa lini?
view
14 Oct 2021 in Senate:
Bi. Spika wa Muda, wakati huu ni wa kiangazi na hakuna pesa katika Kenya hii. Taarifa hii imetolewa na Seneta ni ya muhimu sana. Ni Bunge la Seneti peke yake ambayo inaweza kwenda kuokoa watu kutoka janga hili la p ending bills . Hizi pendingbills zinawaathiri watu wengi katika kaunti zetu. Watu wa kaunti yangu wameathirika sana. Ninaomba Serikali ifuatilie jambo hili kwa makini na ijulikane ni nini pending
view
14 Oct 2021 in Senate:
hazilipwi. Kwa nini watu hawapati pesa zao? Kwa nini watu wanaendelea kuwa na shida? Bi. Spika wa Muda, ninaunga mkono Taarifa hii. Ninaomba suala hili lifanyike hala hala ili kuokoa Wakenya wengi ambao wamefanya kandarasi ya Serikali.
view
7 Oct 2021 in Senate:
Ahsante, Mheshimiwa Spika wa Muda, kwa kunipatia nafasi hii. Maseneta ambao wamechaguliwa kujiunga na Kamati ya Ugatuzi na Mahusiano Kati ya kiserikali za Kaunti na Serikali Kuu na pia wale ambao waliochaguliwa hivi karibu, tunawakaribisha kwa Bunge hili. Tunatoa wito kwao waweze kukaa katika Bunge hili na kuendeleza mambo ya ugatuzi. Kwa hakika hakuna njia nyingine ambayo mtu anaweza kufanya kazi yake iwe mzuri zaidi sababu ugatuzi vile ulivyonakiliwa ndani ya katiba ya sasa. Kwa wale waliopata fursa kutekeleza mambo ya ugatuzi wamepata bahati kubwa haswa kukaa katika Seneti.
view
7 Oct 2021 in Senate:
The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view
7 Oct 2021 in Senate:
Kazi yao haitakamilika bila kufanya kazi ya ugatuzi. Wao wamewekwa katika Kamati hiyo ya Ugatuzi na Mahusiano Kati ya Serikali za Kaunti na Serikali Kuu na ni nafasi mwafaka ambayo wanaweza kufanya kazi hiyo ili waweze kujua vile watakavyoendesha kaunti zao na pia wafanye kazi na magavana katika kaunti zao. Kwa siku ya leo, vile tumepitisha Hoja hii wajiunge na Kamati hiyo kama wataweza basi kazi ya ugatuzi itaenda mbele. Mimi natoa wito kwao waweze kukaa katika Kamati hii na waendeleze shughuli za ugatuzi. Ninaunga mkono, Mheshimiwa Spika wa Muda. Asante.
view
7 Oct 2021 in Senate:
Asante Bw. Spika wa Muda kwa fursa. Ninampongeza Sen. (Dr.) Musuruve kwa kuleta Arifa hii ya Siku ya Ulimwengu ya Walimu. Kwa hakika, sisi sote tumepitia kwa mikono ya waalimu. Ualimu ni msingi mkubwa katika kutengeneza mtu awe mwanadamu kamili kwa sababu mwanadamu bila elimu hayuko kamili. Ukiangalia walimu wa Kenya wakati mwingi wanaenda kulima kwa sababu ya marupu rupu ama mshahara ile ambayo wanapata. Ukiangalia kwa kina walimu wanalipwa mshahara kidogo zaidi. Sen. Cheruiyot alisema mwalimu huwezi ukamlipa na hii ni ukweli. Hakuna pesa ambayo inaweza kumlipa mwalimu kwa sababu hata ukisema ni pesa kiasi gani bado hiyo kazi ...
view
7 Oct 2021 in Senate:
Sisi hatuna budi kuongeza sauti yetu kwa sababu tunaelewa kuwa walimu ni wengi katika taifa la Kenya. Katika siasa, wengi ndio huhesabika. Tutasimama na walimu usiku na mchana, wakati wanapoenda kusherekea siku yao ya Walimu Ulimwenguni. Hongera walimu wote wa Kenya na duniani.
view