All parliamentary appearances

Entries 1 to 10 of 74.

  • 15 Jun 2017 in National Assembly: Asante sana, Mhe. Spika. Ninakushukuru kwa kunipatia nafasi hii ili niongee machache. Ninawashukuru watu wa Matuga kwa kunipatia kipindi cha miaka minne na miezi miwili kuwatumikia. Ni imani yangu kwamba kutokana na kazi ilivyofanyika, tutakuwa pamoja tena hapa mimi na wewe kwani nina imani pia kwamba wewe utarudi na kumbuka kwamba kura yangu ni yako. Kwa hivyo tutakuwa pamoja hapa mara tu baada ya uchaguzi. Mhe. Spika, safari yangu ya kuja Bunge hili ilikuwa ndefu sana. Ilianza mwaka wa 2002 nikipelekwa huku na huku, nikiibiwa hapa na pale na nikienda kortini na hakimu akiniambia kwamba mjadala wangu ulikuwa mzuri na ... view
  • 29 Mar 2017 in National Assembly: Ahsante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Nimesimama kuunga mkono Mswada huu muhimu sana ambao unazungumzia masuala ya elimu ya msingi. Elimu ni muhimu sana, haswa elimu ya msingi. Watoto wanapokwenda kwenye shule za msingi, ofisi za elimu na viongozi wanatakiwa wawe wamekata shauri kulizingatia jambo hili kwa makini sana, ili wahakikishe kwamba watoto wamefanya vyema katika shughuli zao za baadaye. view
  • 29 Mar 2017 in National Assembly: Elimu ni muhimu. Pendekezo langu ni kwamba mzazi yeyote atakayepatikana akidharau kuwapeleka watoto shuleni aadhibiwe vikali. Ninaliunga mkono pendekezo hilo kwa asilimia 100. Nataka Serikali ihakikishe kwamba inaangalia jambo hili kwa makini sana. view
  • 29 Mar 2017 in National Assembly: Masuala ya visodo ni muhimu. Naona ni kama elimu ya msingi imeachiwa serikali za kaunti, lakini wameshindwa kuishughulikia. Kwa hivyo, tunataka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ihakikishe kwamba inatia mkono wake kikamilifu katika shughuli hizi ili watoto wapate elimu ya msingi itakayowafaa siku za baadaye. Hili ni jambo ambalo limeshughulikiwa na Hazina ya Kitaifa ya Maendeleo ya Maeneo Bunge (NG-CDF). Sipigii debe NG-CDF kwa sababu mimi ni mhusika, lakini ukiangalia shughuli ambazo NG-CDF imefanya, ziko juu zaidi kuliko zile zilizofanywa na serikali za kaunti. Kwa hivyo, masuala ya NG-CDF yaingizwe ndani, ili waweze kuhakikisha wanashirikiana ili elimu ya msingi ... view
  • 29 Mar 2017 in National Assembly: Naunga mkono Mswada huu ili hatua ya Serikali iwe kamili na ihakikishe kwamba imesimama kindete kwenye vita dhidi ya ufisadi, kwa sababu kuna pesa nyingi sana ambazo zinatumika ovyo ovyo. Kama Serikali ingekuwa inawajibika kikamilifu katika mapambano dhidi ya ufisadi, pesa ambazo zinatumika ovyo ovyo zingetumiwa kuboresha elimu ya msingi. Watoto wanashida, wazazi ni maskini, na pesa hakuna. Serikali ina pesa lakini imelegeza mkono. Watu wanaiba vile wanavyotaka, lakini hawachukuliwi hatua yoyote. view
  • 29 Mar 2017 in National Assembly: Kwa hayo machache, naunga mkono. view
  • 19 Oct 2016 in National Assembly: Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi hii. Kwanza, ninataka kumshukuru Mhe. Omar Mwinyi kwa Hoja hii aliyoileta kwa sababu ni ya maana sana. Ninasema tumechelewa kwa sababu watu wetu wamekandamizwa kwa muda mrefu sana. view
  • 19 Oct 2016 in National Assembly: Ni haki hii stakabadhi itolewe bure kwa sababu tayari mtu amefanyiwa madhara au dhambi. Si vizuri tena atafute pesa anunue stakabadhi hii. Ninawaomba Wabunge walio hapa waipitishe Hoja hii. Jambo hili linafaa lifuatiliwe sawasawa kwa sababu mbali na kuwa unatakikana ulipe ile ada ambayo ni ya Serikali, bila kitu kidogo polisi hawakupatii P3 Form. Kwa hivyo, ni bora wale wanaohusika wahakikishe kwamba shahada hii inatolewa bure, na iwe bure kweli. Si bure na Serikali ikose kile ilichokuwa ikipata lakini mtu binafsi anapatiwa kitu kidogo ndio atoe P3 Form. Hiki ni kitu ambacho kila mwananchi ana haki ya kupata ili haki ... view
  • 5 Oct 2016 in National Assembly: Ahsante sana, Mhe Naibu Spika wa Muda. Kwanza, nataka kumshukuru Mhe. Odanga kwa kukubali maoni yangu kwamba alete Hoja hii, na akafanya hivyo. view
  • 5 Oct 2016 in National Assembly: Hoja hii ni muhimu sana kwa sababu hali ilivyo hivi sasa ni kwamba, nchi yetu inaelekea mahali pabaya sana. Vijana wanachoma mashule, wazee wanafanya mapenzi kiholela bila ya kujali, vijana wanafanya mapenzi wakati usiofaa, watu wengine wanaiba na kufanya mambo chungu nzima, ambayo hayana maana na ambayo yanamuudhi Mwenyezi Mungu. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus