All parliamentary appearances

Entries 71 to 74 of 74.

  • 19 Nov 2014 in National Assembly: Asante sana, Naibu Spika wa Muda. Kwanza, kwa niaba yangu kama kiongozi wa CORD Wilaya ya Kwale nzima na kwa niaba ya watu wangu, ninaomba kupeleka rambirambi zangu kwa familia na marafiki wa kiongozi wa mapambano ambaye ametuwacha. Nikirudi upande wa Hoja tulionayo, ninataka kumshukuru kisawasawa aliyeleta Hoja hii. Jambo hili litakapofanyika, litaondoa madhara mengi sana. Ni jambo la kusikitisha kwamba kutoka hapa mpaka Embakasi, ambapo mtu anaweza kusafiri kwa gari kwa muda wa dakika kumi na tano kama nilivyofanya jana usiku kama saa tano, The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version ... view
  • 19 Nov 2014 in National Assembly: watu wanachukua muda mrefu sana. Leo asubuhi, nimelala nikifikiria kwamba hali itakuwa ile ile, lakini nilipopata teksi kuja hapa, imenichukuaa masaa matatu na nusu. Nilipochukua taxi kuja huku, nilichukua masaa matatu na nusu; jambo ambalo limenisikitisha sana. Kwa hivyo, Hoja hii haihitaji mjadala kwa sababu ni Hoja ya maana. Ni jambo ambalo linafaa kushughulikiwa na Serikali haraka sana ili tuhakikishe kwamba barabara hiyo imepanuliwa na kuondoa madhara mengi. Kwenye msongamano, watu wanabakurwa vipochi. Wengine wanavutwa, skati zao zinatolewa kwa sababu mhalifu amejificha mahali penye watu wengi ambao wamesongamana mahali pamoja. Mtu huyo anapenya bila kuonekana. Jambo hili likitekelezwa, madhara haya ... view
  • 29 Oct 2014 in National Assembly: Asante sana, Bi. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipatia nafasi hii. Kwanza, nataka kumpongeza mhe. Chris Wamalwa kwa kuuleta huu Mswada na kidogo ni mlaumu kwa sababu amechelewa sana. Huu ni Mswada ambao ungeletwa Bungeni mwaka mmoja na nusu uliopita wakati tulipoingia Bungeni. Hii ni kwa sababu ni muhimu sana kuwatambua mashujaa wetu ambao wametuletea nafasi nzuri na faida katika nchi hii. Vile vile, ningetaka kumshukuru yule ambaye ameuleta Mswada kwamba kila kaunti iwe na chuo kikuu. Hili ni jambo la maana na ambalo litahakikisha kwamba elimu, ambayo ndiyo mwenge katika ulimwengu na maisha ya kila mtu, itatanda kila mahali ... view
  • 30 Apr 2013 in National Assembly: Asante sana, Mhe. Spika. Nilikuwa nimevunjika moyo nikifikiria labda Mhe. Spika anafikiria mimi ni marembo ya Bunge hili kwa sababu kila nikiinuka, nanoa. Kwa hivyo, ninakushukuru sana kwa kunipatia nafasi hii kuzungumza machache kuhusu Marehemu Mutula Kilonzo. Mutula hawezi kusahaulika kwa sababu ya shughuli ambazo alikuwa akifanya. Mimi binafsi, ningetaka kupeleka rambirambi zangu kwa sehemu yake ya uwakilishi Bungeni na pia kwa familia yake. Mhe. Mutula alikuwa rafiki yangu na hata aliwahi kuwa wakili wangu nilipokuwa nimedhulumiwa katika uchaguzi kule Matuga. Ni matumaini yangu kwamba watu watakuwa wastahimilivu na wanyenyekevu kwa sababu Mungu amesema wazi wazi katika Koran na Bibilia ... view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus