All parliamentary appearances

Entries 11 to 20 of 74.

  • 5 Oct 2016 in National Assembly: Hii yote ni kwa sababu watu hawana elimu ya kidini ya Kikiristo, Kiislamu, Kibudha na kadhalika. Haya yote ni kwa sababu Serikali haijashugulika kuhakikisha ya kwamba inaweka masheikh, makasisi na watu wengine wa kidini ambao wangeweza kuwafanya vijana wawe na maadili ya kidini kutoka awali. Hii ni muhumi sana na inataka kufuatiliwa. Ikiwa tunataka hali hii iwe sawa, ni lazima tuirekebishe Katiba ya nchi hii haraka inavyowezekana, ili shida hizi ziweze kuondoka. Nilikuwa nije huku siku ya Jumatatu lakini ilibidi nije Jumanne kwa sababu shule mbili katika sehemu yangu ya uwakilishi Bungeni zilichomwa na vijana, na hayo yote ni kwa ... view
  • 5 Oct 2016 in National Assembly: Namuunga mkono kikamilifu Mhe. Odanga kwa kuleta Hoja hii Bungeni. Nawaomba Wabunge wenzangu waipitishe haraka iwezekanavyo. view
  • 5 Oct 2016 in National Assembly: Kwa hayo machache, naunga mkono. view
  • 4 Oct 2016 in National Assembly: Asante sana Mheshimiwa Spika. Kuna mtu hapa analia akisema umenihurumia zaidi kwa sababu yeye amebonyeza mbele yangu. Hata hivyo, achana naye. Nataka kuchukua nafasi hii nikushukuru kwa kunipatia wakati huu. Ni fikra yangu kwamba walioleta Mswada huu hawajui wanakoelekea. Mimi naupinga kikamilifu. Mtindo wa Harambee ambao umeletwa na mwanzilishi wa taifa hili, Mzee Jomo Kenyatta, uungwe mkono mia kwa mia na watu waendelee na shughuli hizo kila uchao. Mheshimiwa Spika, wengi hapa hawataki kujieleza lakini tunajua kwamba wamesomeshwa kwa njia ya Harambee. Hata nakumbuka siku moja nilienda Harambee ya Mheshimiwa Duale, tukamchangia kwa sababu hili ni jambo ambalo ni muhimu ... view
  • 4 Oct 2016 in National Assembly: Mheshimiwa Spika, ingawa rafiki yangu hapa pia amesema kwamba kuwe na marekebisho ili mradi ambao umefanywa kupitia kwa NG-CDF usifanyiwe Harambee, mimi nataka kumwambia kwamba hata kama mradi umegharamiwa na NG-CDF lakini umekwama bado, Harambee ni muhimu. Ningependa kumfahamisha ndugu yangu ya kwambe pesa ya NG- CDF haitoshi kabisa kumaliza tatizo la uhaba wa mijengo katika nchi hii. Mimi naunga mkono kauli kwamba Harambee ziendelee haswa nikijua ya kwamba Serikali haitii mkono wake katika masuala ya makanisa na miskiti. Mambo ya Harambee kama alivyozungumza mwenzangu ndiyo yamefanya wagonjwa wengi waweze kupata tiba nje ya nchi hii. Kwa hivyo, yeyote anayepinga ... view
  • 1 Sep 2016 in National Assembly: Shukrani Mheshimiwa Spika kwa kunipatia nafasi hii. Ningelipenda kwanza nikushukuru wewe kikamilifu kwa sababu ya vle ulivyopambana katika hali ya kudumisha na kuhakikisha kwamba sheria zinafuatwa. Ninakumbuka mwaka wa 1967 marehemu muanzilishi wa taifa hili, Hayati Mzee Jomo Kenyatta aliulizwa na rafiki yake Hayati Julius Nyerere: ―Ni kwa nini wewe unatembea na askari wengi?‖ naye akajibu ―Ninatembea na askari wengi kwa sababu Tanzania si kama Kenya. Kenya ina wanaume.‖ Na ninataka kukuhakikishia umepambana vikali Mheshimiwa Spika kwa sababu Bunge hili lina wanaume kuliko Mabunge yote ulimwengni. Kwa hiyvo, umefanya kazi nzuri pamoja na kamati yako na ninakuombea likizo njema ili ... view
  • 1 Sep 2016 in National Assembly: Kuhusu NGCDF, mimi naunga mkono Mswada uliopitishwa lakini pia naomba kuwe na mipango ya haraka haswa kuhusu ili kamati ya Oversight . Hii kamati inaweza kufanya kazi nzuri lakini mpaka sasa nikiangalia hawana chochote wamefanya. Naomba Kamati ya NGCDF ihakikishe kwamba imepangia kamati ya Oversigh t mambo itakayoweza kufanya kwenye The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor. view
  • 1 Sep 2016 in National Assembly: shughuli zake kwa sababu kukaa bure bila chochote ni shida. Huko kwangu nilifanya hesabu na kuona watapata 30,000 peke yake kila mwaka. Hiyo ni pesa kidogo na lazima kuwe na marekebisho ili waweze kufanya kazi hii kwa juhudi. Hii ni kwa sababu wao ndiyo watafanya ile bodi ifanye kazi kisawasawa, bila hivyo mambo yataende segemnege. Nikiketi naunga mkono na kukusifu tena kwa kazi nzuri ambayo umefanya bila ubaguzi. view
  • 1 Sep 2016 in National Assembly: Asante Mhe. Spika. view
  • 3 Aug 2016 in National Assembly: Sorry, Hon. Temporary Deputy Speaker. I was just preparing myself for the Motion on provision of water to public facilities by Hon. Mwadime. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus