All parliamentary appearances

Entries 21 to 30 of 74.

  • 3 Aug 2016 in National Assembly: Shukrani, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Kwanza, nataka kukupongeza kwa kazi nzito ambayo umeipata. Naamini unaiweza. view
  • 3 Aug 2016 in National Assembly: Mhe. Spika Naibu wa Muda, Hoja hii ni muhimu sana kwa sababu hakuna kitu kinachoweza kufanyika katika kijiji au shuleni bila maji kuwepo. Badala ya umeme kupewa kipaumbele, ingefaa maji yapewe umuhimu zaidi kwa sababu maji ni uhai. Hivi sasa, watoto wetu katika shule nyingi wanafaidika na mpango wa chakula cha mchana. Ni lazima chakula hicho kipikwe kutumia maji. Watoto wetu wanapitia hali taabani, wakitembea mwendo wa kilomita 10 wakitafuta maji. Licha ya masaibu yanayowakumba wanafunzi shuleni, kuwepo kwa maji vijijini pia ni muhimu. view
  • 3 Aug 2016 in National Assembly: Watu wengi wanapata magonjwa kwa sababu wanachimba mashimo ili maji yatoke. Wengi wao hunywa maji mitoni – mito ambamo ngómbe, mbuzi na wanyama wengine wameenda haja zao ndani. Hali hiyo huwafanya wananchi kuwa wagonjwa. Ningependa kukuhakikishia kwamba kule nitokako, Matuga, nyumba zimevunjika kwa sababu ya ukosefu wa maji. Mnajua, utamu wa bwana na bibi kitandani ni masaa ya kuanzia saa kumi hadi saa kumi na mbili asubuhi. Wakati huo, unapata bibi akiruka kutoka kitandani na akiulizwa, anasema anaenda kutafuta maji. Bibi anarauka kwenda kutafuta maji wakati bwana anahitaji kukumbatiwa. view
  • 3 Aug 2016 in National Assembly: Mhe. Naibu Spika wa Muda, tungependa kuondoa hali hii kwa sababu miji imebomoka. view
  • 3 Aug 2016 in National Assembly: Watoto wanajua kwamba walizaliwa pia. Maji ni muhimu na tunaiomba Serikali ihakikishe kwamba imechukua jukumu hili kwa dhati zaidi na kulipa umuhimu. Nampongeza Mhe. Mwadime kwa kuuleta Mswada huu Bungeni. Nakupongeza tena, Mhe. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi hii. Ahsante na Mungu atubariki sote. view
  • 3 Aug 2016 in National Assembly: Kwa hayo machache, naunga Mkono Hoja huu. view
  • 20 Jul 2016 in National Assembly: Ahsante sana Mhe. Naibu Spika wa Muda. Kabla sijaendelea, ningependa kuwafahamisha kwamba sisi ndio tunatengeneza Bajeti, na sisi tuko katika Serikali ya kitaifa. Ni jambo la kusitikisha kwamba walio katika serikali za majimbo, wanaweza kuangalia watu wao huko ilhali ni sisi ndio tunaowagawanyia pesa. Sisi tunaowagawanyia pesa watu wetu ambao wako katika Serikali ya kitaifa, ambao ni wazee wa vijiji, wanapata matatizo na shida nyingi mno. Hili ni jambo ambalo sisi wenyewe tungeliangazia kwanza kabla hatujaangalia serikali za majimbo. Ukweli ni kwamba wazee wa vijiji wanaojulikana kama view
  • 20 Jul 2016 in National Assembly: , wanafanya kazi ngumu mno na wanaifanya katika umri wowote bila kupoteza hata dakika moja. Mwenyekiti wa kijiji anaanza kazi kutoka asubuhi hadi kesho asubuhi. Akiishi miaka 60, basi atakua amefanya kazi hiyo kwa takriban miaka 60, ilhali watu wengine ambao wanafanya kazi masaa manane kwa siku wanapata mishahara minono. Nataka kuwaunga mkono wale wenzangu ambao wamesema kwamba wazee wa vijiji ndio wazee ambao wanaweza kuleta shida katika usalama, na ni wao tu ndio wanaoweza kuleta nafuu kubwa katika usalama. Kila kitu kinamwangalia yeye. Ikiwa kila kitu kinamwangalia, kule kwetu wengi sana wamepigwa risasi wakionekana kwamba wanatoa siri za watu, ... view
  • 20 Jul 2016 in National Assembly: Ninakumbuka Mhe. Mwadime hapa akisema kwamba yeyote atakayekataa Hoja hii achukuliwe hatua. Watu wamecheka na kuona kwamba labda anazungumza utani. Mimi ninarudia kwamba yeyote ambaye hataki kuunga mkono Hoja hii ni adui wa maendeleo na ukweli anastahili kuchukuliwa hatua ya kufaa. Mwaura awe mfano mzuri wa kuchukuliwa hatua hiyo. Kwa hayo machache ninataka kukushukuru kwa kunipatia wakati huu japo wengine waliokuja nyuma wamepewa mapema kuliko mimi. Asante. view
  • 6 Jul 2016 in National Assembly: Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Nakubali kwamba mvumilivu hula mbivu. Kuna watu wamebofya saa mbili baada yangu na wamepata nafasi. Kwa hivyo, ni kuvumilia. Nachukua nafasi hii nikupongeze, nimpongeze aliyeleta Hoja hii na yule aliyeuunga mkono kwa mara ya kwanza. Serikali na watu wanalalamika kwa ukosefu wa kazi. Lau Serikali ingalikuwa inatia bidii na kuzingatia masuala ya uvuvi katika nchi hii, upungufu wa kazi ungalipungua kiasi kikubwa mno. Kwa sababu Serikali imeweka mkono nyuma, mambo haya yanaharibika. Watu haswa walio sehemu zilizo na maumbo makubwa ya maji kama Ziwa Victoria, Ziwa Naivasha na Bahari ya Hindi kule Pwani ... view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus