6 Jul 2016 in National Assembly:
Naunga mkono Hoja hii. Nawaomba Wabunge wenzangu walio hapa waunge mkono Hoja hii bila kujali hiki wala kile. Hii ni ili tufaulu na kupunguza ukosefu wa kazi katika nchi hii. Asante, Naibu Spika wa Muda. Naunga mkono.
view
5 May 2016 in National Assembly:
Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipatia nafasi hii ili niunge mkono Hoja iliyoko mbele yetu siku ya leo. Ni lazima Serikali itafakari kwa sababu mara nyingi huwa na zogo kwa sababu ya hawa watu wa IEBC. Ingawa mmoja wetu hivi sasa amezungumza na kuuliza watu wa CORD wako wapi, nataka kumwambia ya kwamba mambo haya si ya CORD. CORD inasimamia haya mambo na yoyote anayezungumza ana simamia mambo haya kwa sababu ya kuleta amani nchini. Kwa hivyo, awe mtu wa CORD ama Jubilee mimi naona kwamba iko haja jambo hili liangaliwe kwa makini na watu wote ili ...
view
5 May 2016 in National Assembly:
mtihani nafikiri hapo ndipo wakati utajuwa kwamba huyo ni kiongozi ama si kiongozi sawasawa. Kwa hivyo, masuala ya elimu mimi naona kwamba cheti kisiwe na uzito zaidi. Nakumbuka kwamba zamani kulikuwa na mibabe ya kisiasi ambao hawakufika hata darasa la nne. Nikitoa mfano, kule kwetu tulikuwa na mbabe wa siasa Mhe. Masoud Mwakileo, Mhe. Mwarua Abdalla, na Mhe. Abdalla Ndovu Mwidao. Hawa nina imani kuwa elimu yao haikuwa ya juu kama vile watu wanavyofikiria lakini walikuwa wanasema maneno sawa sawa na wakizungumza mtu anajua. Nina wasiwasi kama marehemu Shikuku alikuwa na degree. Pengine alikuwa na diploma tu lakini alikuwa akizungumza ...
view
5 May 2016 in National Assembly:
Bunge hili huwa na matatizo wakati Mwanyoha anazugumza. Watu hutoa maneno ili wakati wangu uishe. Mhe. Naibu Spika wa Muda, nashukuru kwa kunitetea; uendelee namna hiyo. Nataka sasa niongee kuhusu nambari ya wale ambao wanahitajika kupiga kura katika kituo. Mara kwa mara kuna watu wengi sana, mpaka watu wengine huja saa kumi na mbili za asubuhi. Lakini ikifika saa kumi na mbili za jioni wanaambia wakati umeisha na wanaachwa nje. Naomba kuwe na marekebisho ili badala ya kuwa na watu 1,000 wawe 500 kwa kila kituo. Vituo viweze kuongezwa ili kuwe na muda mrefu na kila mtu aweze kupiga kura.Kwa ...
view
5 May 2016 in National Assembly:
Asante sana. Hiyo ni kuonyesha maneno haya ni kabambe. Kwa hivyo naomba ya kwamba uteuzi ufanywe baada ya uchaguzi na tuhakikishe kwamba mambo yamekuwa sawa sawa. Asante, Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi hii. Naunga mkono.
view
3 May 2016 in National Assembly:
On a point of order, Hon. Temporary Deputy Chairlady.
view
3 May 2016 in National Assembly:
Mhe. Mwenyekiti wa Muda, mambo yanayozungumzwa hapa ni muhimu sana. Yanahitaji watu wa kutosha kwa sababu Wakenya wote wanaangalia siku ya leo. Nikiangalia watu hawajatosha; hakuna quorum kamili ya kuendelea na maneno haya. Kwa hivyo ifungike na watu wangoje mengine kwa sababu pana klabu hapa ambayo imejipanga makusudi kuhujumu maneno ambayo yametengenezwa na Wakenya wote. Asante, Mhe. Mwenykiti wa Muda.
view
30 Mar 2016 in National Assembly:
Ahsante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Pia ninataka kumshukuru Mhe. Wanyonyi kwa kuileta Hoja hii Bungeni. Kupiga kura ni haki ya kila Mkenya. Kila mtu anastahili kupata nafasi ya kutosha ya kupiga kura vile anavyotaka. Kulingana na sheria ni sawasawa kabisa kwamba kila anayetaka kupiga kura apate stakabadhi maalum. Kama stakabadhi ile ambayo mtu hupewa kwa mara ya kwanza ina nambari zote ambazo zitaonekana katika kitambulisho, sioni sababu yoyote ya mtu kukatazwa kupiga kura wala kutumia stakabadhi hiyo katika benki. Hali hii huleta dhuluma. Juzi The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified ...
view
30 Mar 2016 in National Assembly:
tulipokuwa kule Malindi ambako tulilibeba kombe, nilifuatwa na vijana zaidi ya 2,000 ambao walikuwa wanajua kwamba mimi ni rafiki wa Mwenyekiti wa KADU Asili. Walijua kwamba nilikuwa nikimfanyia kampeini mwenyekiti huyo. Vijana hao walikuja mbio na kadi ambazo hazikuwa za vitambulisho vya kawaida. Wakanilalamikia kwamba wao wanataka wapige kura. Ukweli ni kwamba kama nilikuwa Jilore peke yake na nilipata vijana 2,000 wa KADU Asili---
view
30 Mar 2016 in National Assembly:
Mhe. Naibu Spika wa Muda, ningependa Mhe. T.G. Ali ajue kwamba hiyo ndiyo sababu ya kuibadilisha sheria hiyo. Nilipokuwa kule Malindi nilifuatwa na vijana wanaofika 2,000, wakiwa na maua yao wakipiga kelele; wakifikiria kwamba mimi ni mfuasi wa KADU Asili, rafiki yangu, Mhe. Gunga. Inaonekana kwamba kama vijana wale wangelipata ruhusa ya kupiga kura – wale wakiwa vijana kutoka Jilore peke yake, hatujui Malindi nzima kulikuwa na vijana wangapi waliokuwa na kadi za aina ile – nina hakika kwamba badala ya Jubilee nambari kuwa ya pilli ingekuwa KADU Asili. Lakini kwa sababu haki haikuzingatiwa, wale vijana hawakupiga kura.
view