All parliamentary appearances

Entries 51 to 60 of 74.

  • 16 Mar 2016 in National Assembly: Kwa hayo machache, naunga mkono Hoja hii. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor. view
  • 3 Dec 2015 in National Assembly: Asante sana, Naibu Spika wa Muda. Ningependa kuchukua nafasi hii kumshukuru Mwenyekiti wa Kamati ya Mazingara na Rasilimali kwa kuleta Hoja hii. Ikiwa Serikali itafuata Hoja hii inavyotakikana, itakuwa ya maana sana. Watu wa Pwani, kwa mfano Mombasa na Kwale, wamekuwa wakisumbuka na kuteseka sana kwa sababu ya hali ya kutoweza kumudu shughuli zao. Serikali ilikuwa inawaachilia watu kuingililia Mwambao wa Pwani bure tu na kuvuruga mambo. Nina imani kwamba, kutokana na Hoja hii, mambo yatakuwa sawasawa. Naiomba Serikali ifuatilie mambo haya baada ya hapa. Kama vile Mheshimiwa alivyozungumza, miradi mingine kama ule wa kuchimba makaa ya mawe kule Lamu ... view
  • 24 Nov 2015 in National Assembly: Shukrani, Naibu Spika wa Muda. Nilidhani hunioni, kumbe waniona! Mhe. Naibu Spika wa Muda, mimi nasimama kuunga mkono Hoja hii kwa sababu anayekuja ni mtu mtukufu, na hata kama dini ni tofauti zote zaelekea kwa Mungu mmoja. Mimi ni Muislamu na najua kwamba Bunge hili lina Waislamu wa kutosha. Nawauliza Waislamu wenzangu, waheshimu Baba Mtakatifu ili tuweze kuhakikisha kwamba tunaenda kukutana na yeye. Baraka hazitoki sehemu moja. Zinatoka sehemu mbalimbali na nina imani kuwa yeye akiwa kiongozi wa ulimwengu, atatupatia baraka zake. Langu tu ni kumuuliza Mwenyezi Mungu, siku moja Baba Mtakatifu aje awe mtu wa Kenya kama Mhe. Gunga, ... view
  • 26 Aug 2015 in National Assembly: Ahsante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Ningependa kukushukuru kwa kunipatia nafasi hii na pia kumshukuru Mhe. Keynan kwa kuleta Mswada huu. view
  • 26 Aug 2015 in National Assembly: Mswada huu ni muhimu kwa sababu sisi Wabunge ni watu ambao tunafanya kazi kama mawakili wa wananchi na vile vile tunafanya kazi kama watetezi wa wananchi na pia kama viongozi ambao lengo letu ni kuhakikisha kwamba maendeleo yameingia kila mahali katika zile sehemu tunazoongoza. view
  • 26 Aug 2015 in National Assembly: Wakati wowote, Mbunge ni lazima aweze kuzungumza maneno hata kama yataonekana kama ni maneno makali. Anastahili kulindwa kwa sababu bila ya kulindwa, tutakuwa waoga na hatutaweza kuwatetea watu wetu. Kwa hivyo Mswada huu ni muhimu sana kwa sababu utatuwezesha kutetea watu wetu bila hofu ama uoga. Kwa hivyo, tunahitaji tupate ulinzi mkali katika hali hii. Mswada huu ukipita ndio tutakua tumepata ulinzi mzuri. view
  • 26 Aug 2015 in National Assembly: Kwa hivyo, sitakua na marefu sana. Langu ni kuwauliza Wabunge wenzangu waweze kuunga mkono Mswada huu ili tuweze kuwa katika hali nzuri, isiwe kama ile hali ya kutoka zamani ambapo mtu anahangaishwa hapa na pale kwa sababu ya kuzungumza ukweli. Ni ukweli tu ndio utatengeneza nchi hii na ni Mswada huu upite ili tuweze kupata nafasi ya kutengeneza nchi hii. view
  • 26 Aug 2015 in National Assembly: Ahsante. Naunga mkono Mswada huu. view
  • 15 Apr 2015 in National Assembly: Asante sana Mheshimiwa Naibu Spika . Kwanza nataka kumtangaza Mheshimiwa Joyce kama mtu mwenye maono ya hali ya juu sana kwa sababu jambo hili lilikuwa linatakikana liletwe mapema. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor. view
  • 15 Apr 2015 in National Assembly: Asante sana Mheshimiwa Naibu Spika . Kwanza nataka kumtangaza Mheshimiwa Joyce kama mtu mwenye maono ya hali ya juu sana kwa sababu jambo hili lilikuwa linatakikana liletwe mapema. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus