Isaac Maigua Mwaura

Parties & Coalitions

Born

1982

Email

mwaura.isa@gmail.com

Web

www.isaacmwaura.com/

Telephone

0721864949

Telephone

0733864949

Link

@MwauraIsaac1 on Twitter

All parliamentary appearances

Entries 1131 to 1140 of 1711.

  • 17 Feb 2016 in National Assembly: No, they do not. Even yesterday when they made their submissions, it was clear that they do not. We may want to work in conjunction with the National Construction Authority. That would make sense. We have the minimum--- view
  • 17 Feb 2016 in National Assembly: Hon. Temporary Deputy Speaker, I am persuaded by the wisdom of the House. Let us domicile that responsibility to the National Construction Authority (NCA). But they should work in conjunction with the council because they have the--- view
  • 17 Feb 2016 in National Assembly: Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Ninasimama hapa kuunga mkono Mswada huu hususan kwa sababu mimi nimekuwa nikijaribu kuwasaidia watu wengi ambao wanakuja kwenye afisi yangu wakitaka usaidizi hususan wa kisheria na kuweza kupata haki yao. view
  • 17 Feb 2016 in National Assembly: Mhe. Naibu Spika wa Muda, namkumbuka sana aliyetuacha, Oscar King’ara, ambaye alikuwa na Oscar Foundation ambayo ilikuwa na kiosk pale nje ya Mahakama ya Supreme Court wakati ule ilikuwa ni High Court. Kwa sababu ya kujihusisha ma maswala haya akaletewa kesi za watu ambao walikuwa wameuwawa bila ya kujulikana kama vile Mungiki . Mwishowe, kwa sababu ya kujitolea kwa kazi yake, hata yeye mwenyewe aliuwawa. view
  • 17 Feb 2016 in National Assembly: Hili ni jambo ambalo linafaa kutuelezea kwamba kumekuwa na changamoto nyingi sana kwa wale ambao wamejitolea kuwasaidia maskini, walalahoi, watu ambao wanaitwa vikaragosi na watu ambao wanaonekana hawana mbele wala nyuma hususan ukifika katika mambo ya mkono wa sheria. view
  • 17 Feb 2016 in National Assembly: Nchi hii yetu imekuwa taabani kwa sababu inaonekana ni kana kwamba wenye hela wanaweza kupata haki. Wenye hela wanaweza kuhonga mahakama na wanaweza kuwa na mawakili wazuri ambao wanaweza kuwasaidia kujikwamua hata kama wao wenyewe wamekisiwa kwamba wamewaua watu. Na kuna aina nyingi sana za kesi ambazo tumeona watu ambao wangefaa kuhukumiwa hata baada yao wenyewe kukubali kwamba wamefanya makosa,wanawachiliwa. Kesi ambayo inakuja kwa akili yangu ni kesi ya Simon Ole Sisina katika lile swala la Delamare. view
  • 17 Feb 2016 in National Assembly: Katika afisi yangu, ninakutana na watu wengi sana. Kwa mfano, Rockerfeller Okeyo, ambaye ni mlemavu, alifanya kazi katika shule moja kule Asumbi na wakati pesa zilipotea akiwa mhasibu wa shule, akazingiziwa ilhali yeye ni mlemavu na watu walikuwa wamevunja ufa na kuingia kule ndani. Amefuatilia ile kesi lakini amekuwa na mawakili matapeli ambao wanahongwa na mwishowe wanamuachia ile kazi. Mwishowe, kumekuwa na kesi ya mama mwingine anayeitwa Lucy Wangeci, ambaye ako na ulemavu wa kutokuona. Ameachiwa shamba kubwa kule Kirinyaga lakini kwa sababu yeye hajaolewa kwa sababu ya ulemavu wake, ananyimwa lile shamba na linauzwa na ndugu yake na hana ... view
  • 17 Feb 2016 in National Assembly: Pia, kuna jambo jingine. Kuna watu, hata sasa tunapozungumza katika hili Bunge la Kitaifa, ambao wako korokoroni kwa sababu hawakuwa na uwakilishwaji mwema. Hilo ni The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor. view
  • 17 Feb 2016 in National Assembly: jambo ambalo Mswada huu unajaribu kuangazia. Kwa muda mrefu, mawakili katika afisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikari ndio wanafaa kuwasaidia watu ambao hawana usaidizi. Wao wanazembea kazini kwa sababu hawana ari au motisha ya kuweza kufanyia watu ambao ni maskini kazi. Mwishowe, hizo kesi zinatupiliwa mbali. Kwa mfano, unakuta hawaji kortini na hawana wakati wa kumpatia wasia yule muadhiriwa. Kwa hivyo, kesi inapotelekezwa, basi yule mtu hana nafasi yoyote ya kuridhia mambo yake. view
  • 17 Feb 2016 in National Assembly: Ninapoangalia Mswada huu, naweza kuupigia upato zaidi na niseme kongole kwa wale wameufikiria kwa muda mrefu. Mwanzo, Mswada huu umetoa mkakati ambao unafaa kufuatiliwa wakati tunatafuta watu ambao watatetea maskini. Mwanzo, kuna mfuko wa fedha ambao umetengwa lakini ningependa kusema kuwa ni jukumu la Bunge hili kuhakikisha kwamba pesa za kutosha zimetengwa mle kwa sababu ile ada ambayo inatozwa na mawikili ni ya bei ghali mno. Nikiuangalia huu Mswada, naona ile huduma ya kuwapatia Wakenya huduma za kisheria bure inaweza kutoa ada fulani. Lakini ningependa kusema kwamba hilo ni jambo ambalo tunafaa kuliangazia kwa sababu ukiseme kwamba ni lazima yule ... view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus