Issa Juma Boy

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 121 to 130 of 162.

  • 13 Jun 2019 in Senate: Asante, Bi. Spika wa Muda, kunipa fursa hii kuchangia Petition iliyoletwa hapa. Ni jambo la kusikitisha kwa sababu kuna malalamiko kuhusu ufisadi na ukosefu wa kazi katika kaunti 47. Tusipochunga, tutakuwa na petitions 47 hapa. view
  • 13 Jun 2019 in Senate: Naunga mkono hii Petition iliyoletwa hapa kwa sababu swala hili linafaa kutatuliwa. Kule Kwale, kila mara ninapopiga kelele kuhusu ufisadi, watu wanapuuza na kujiuliza kama mimi ni kiranja. Mojawapo ya majukumu yetu ni kuchunguza matumizi ya pesa za umma. view
  • 13 Jun 2019 in Senate: Tunafaa kushughulikia hii Petition haraka iwezekanavyo ili watu wa Nyamira wapate haki yao. view
  • 28 May 2019 in Senate: Bw. Spika, najumuuika na Maseneta wenzangu kuwakaribisha wanafunzi kutoka Kaunti ya Makueni. Kama wanafunzi wanavyo tuona hapa katika Seneti, tunawakilisha makaunti 47. Wanafunzi wanapaswa kujua kwamba wakitia bidii wanaweza kuwa viongozi wa nchi hii. Nawasihi wawe na bidii. Nawatakia siku njema na wajifunze mengi watakayo yaona hapa. Karibuni. view
  • 23 May 2019 in Senate: Asante sana, Bw. Spika wa Muda. Ningependa kuchangia Taarifa hii ambayo imeombwa na Mhe. Madzayo. Hili ni jambo la kusikitisha sana kwa sababu kwa sasa shida kubwa ambayo tuko nayo ni swala la ardhi. Utakuta mtu anaondolewa katika ardhi na nyumba yake kubomolewa siku ya Ijumaa au Jumamosi asubuhi. Hiki kitendo kilitokea huko Mtwapa na watu walionyeshwa katika runinga wakipigwa. Mwakilishi wa eneo la Mtwapa katika Bunge la Kaunti (MCA) ameshikwa na kutiwa ndani. Mimi niliona jambo hili likiwa mbaya sana. Swala hili lazima litatuliwe kwa haraka sana. Kamati itakayopewa jukumu la kuchunguza jambo hili inafaa kwenda huko Mtwapa kwenye ... view
  • 23 May 2019 in Senate: Bw. Spika wa Muda, hili ni swala ngumu sana, lakini kuna njia ya kuitatua. Tunapata shida sana kuhusu mambo ya ardhi katika sehemu za Kwale, Kilifi, Taita na sehemu zingine za Pwani. Ninaunga mkono Taarifa hii ya Mhe. Madzayo na ningependa sheria ifuatwe. Kamati ambayo itachunguza mambo kuhusu hiyo ardhi inafaa iende mpaka Kilifi ili itatue hiyo shida. Wasizunguke tu hapa Nairobi; hapana! Asante sana, Bw. Spika wa Muda. view
  • 10 Apr 2019 in Senate: Asante sana, Madamu Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii kuchangia ombi hili ambalo limeletwa na Seneta wa Taita-Taveta, Seneta Mwaruma. view
  • 10 Apr 2019 in Senate: Ni jambo la kusikitisha sana hasa ukiona kwamba mwananchi amekubali kutoa ardhi yake kwa Serikali kujenga barabara. Leo watu hao ambao wametoa ardhi yao na hawajalipwa pesa zao wana familia na wanategemea kupata pesa hizo waweze kusaidia familia zao. view
  • 10 Apr 2019 in Senate: Kwa hivyo, mimi naunga sana ombi hili ambalo liletwa na Mhe. Mwaruma hapa na ile Kamati ambayo itakayohusika kuchunguza jambo hili, iweze kufanya hili jambo kwa haraka sana ili wananchi ambao wameathiriwa walipwe haki yao. view
  • 10 Apr 2019 in Senate: Sisi kama majirani wa Taita-Taveta na Kwale, tunaunga mkono sana ombi hili ambalo limeletwa na Mhe. Mwaruma. Kwa hivyo, tuntaka kamati hii iende, sio kwamba izungumzie, waende wenyewe mpaka kwa watu hawa na kuchunguza idadi yao na ardhi zao ambazo wamepeana kwa Serikali ili walipwe haki na fidia yao. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus