Issa Juma Boy

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 131 to 140 of 162.

  • 10 Apr 2019 in Senate: Naunga mkono. view
  • 21 Nov 2018 in Senate: Asante sana Bw. Spika. Kwanza natoa kongole kwa Sen. Mwaruma kwa kuleta Ombi hili katika Seneti. view
  • 21 Nov 2018 in Senate: Mheshimiwa Spika, swala la ardhi ni sugu sana katika nchi hii yetu ya Kenya. Watu wa Kaunti ya Taita Taveta wanapaswa kujua kwamba hili swala limeletwa katika Seneti. Kwa niaba ya watu wa Kwale, ambao ni majirani wa Taita Taveta, naomba, hili swala liweze kushughulikiwa kwa haraka sana. Unapotoa mwelekeo wa kutatua swala hili, ningeomba Kamati husika waende nyanjani kwenye hizo ardhi. Ilhali, wasishughulikie jambo hili wakiwa hapa. Wanafaa waende katika hizo ardhi wahakikishe na wasikize wananchi wa Taita Taveta. Nina hakika wananchi wa Taita Taveta watapata haki yao. Bw. Spika, naunga mkono ombi hili. view
  • 6 Nov 2018 in Senate: Asante, Bw. Spika, kwa kunipa fursa hii. Swala hili limeleta utata sana katika sehemu za Pwani. Kwa niaba ya Kaunti ya Kwale na mimi binafsi, natoa rambirambi zangu kwa watu wa Kaunti ya Taita Taveta kwa sababu ya maafa ya juzi. view
  • 6 Nov 2018 in Senate: Sen. Mwaruma amesema maneno mazito sana hapa kwamba watu wameuawa. Kama tunavyojua mwananchi akiuawa, watu hawapigi kilele nyingi. Lakini ingekuwa ni mnyama amapetikana ameuawa katika mbuga, wakati huu watu wangekuwa wameenda huko mbio kushughulikia jambo hilo. view
  • 6 Nov 2018 in Senate: Ninaomba hili swala lishughulikiwe kwa haraka sana na Kamati hii. Ningeomba Kamati hii itoe utaratibu wake haraka iwezekanavyo kwa sababu wananchi wanaishi kwa taharuki kubwa bila kujua mwelekeo wao ni upi. view
  • 6 Nov 2018 in Senate: Sisi ni majirani na maafa haya yametuhuzunisha muno. view
  • 25 Jul 2018 in Senate: Asante sana, Bw. Naibu Spika. Nitachukua muda mfupi sana. Kwanza, ninataka kuunga mkono jambo liloletwa hapa na kiongozi wa wengi; Sen. Murkomen. Kama unavyojua, sisi Maseneta ni watu muhimu sana katika nchi hii, hasa katika kaunti. Hakuna mtu ambaye anaangalia rasilmali ya kaunti na kila kitu katika kaunti isipokuwa Bunge la Seneti. Hawa Wabunge wenzetu katika Bunge la Kitaifa wanafikiria ya kwamba sisi Maseneta tutaacha useneta na kwenda katika ugavana miaka inayokuja. Hii ndiyo shida yao kubwa. Mimi ningeomba Seneta wenzangu tuungane ili tuweze kupigania Bunge letu la Seneti na kuhakikisha kwamba Seneti inaheshimiwa na isimame imara kuwatumikia wananchi wetu ... view
  • 11 Jul 2018 in Senate: Asante sana, Bw. Spika. Mimi pia naungana na Maseneta wenzangu kukaribisha ujumbe huu wa Kaunti za Busia na Trans Nzoia. Kama unavyojua, sisi tuko hapa kwa ajili yao ili kuwatumikia hasa wananchi. Pia, ni vizuri waje hapa watuone vile tunavyoendesha Kikao chetu cha Seneti. Kama mnavyojua, sisi ndiyo jicho la kaunti zetu zote. Tutafanya kazi na ninyi na tutahakikisha kwamba rasilmali za kaunti zinatumiwa vizuri. Mungu awajalie, tuweze kukutana tena. view
  • 19 Jun 2018 in Senate: Ahsante sana, Bw. Naibu Spika. Ninakushukuru kwa kupata fursa hii siku ya leo kuungana na Maseneta wenzangu kuomboleza kifo cha Seneta mwenzetu, Sen. Okello. Siku ya leo ni siku ya huzuni sana. Mheshimiwa Oliech alikuwa ni Seneta mwenzetu ambaye--- view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus