She has established the Janet Nangabo Foundation, a community based organization specifically created to provide solutions for problems of the Trans Nzoia people.
13 Mar 2019 in National Assembly:
Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda.
view
6 Mar 2019 in National Assembly:
(Trans Nzoia CWR, JP) : Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi hii nichangie mjadala huu ambao umeletwa na Mhe. Didmus, Mbunge wa Kimilili. Ningetaka kushirikiana na wenzangu ambao wanaunga mkono mjadala huu kuhusu nauli zinazolipishwa watu kwenye barabara zetu, hasa sekta ya uchukuzi katika nchi yetu ya Kenya. Vile Mhe. Dennitah Ghati ameongea hapa, kuhusu walemavu kutumia usafiri huu hapa nchini Kenya ni kweli kabisa. Baadhi ya hawa watu, hupata shida sana. Hii ni kwa sababu hawana nafasi ya kusimama ama kuongea na manamba wa matatu, na kusema wangependa nauli iteremshwe ama wanatoka pahali fulani wakielekea ...
view
6 Mar 2019 in National Assembly:
Sisi kama viongozi katika Bunge hili hatujakuja hapa ili kuzozana kama nilivyowaona wenzangu wakifanya. Baada ya mmoja kuongea, mwingine anamrushia matusi. Sisi sote tulikuja hapa sio kwa sababu tunafaa bali ni kwa mambo yake Mwenyezi Mungu kupitia kwa wapigakura kule mashinani kuhakikisha kwamba tuko hapa tukifanyia kazi wananchi waliotutuma katika Bunge hili. Mimi humpa kongole Rais mstaafu Moi ambaye alikuwa rais wetu kwa miaka 24 kwa sababu hawakusema alikuwa amehitimu kiwango fulani. Uongozi unamfaa mtu mwenye hekima zake za kuhakikisha kwamba anakuwa rais, kiongozi au katibu katika nchi yetu ya Kenya. Tukiwa katika Bunge hili tumetumwa na Hoja hii ambayo ...
view
20 Feb 2019 in National Assembly:
Asante sana, Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda kwa kunipa nafasi ya kuchangia Hoja hii iliyoletwa na Mbunge mwenzetu, Ali Mohamed. Namshukuru sana kwa Hoja hii. Imekuja wakati mzuri kwa sababu maeneo ambayo baadhi yetu tunatoka, watu wanaumia sana. Mwenzangu Oluoch alichangia na kusema kwamba kulikuwa na hospitali moja katika eneo langu kule Trans Nzoia, Crystal Hospital iliyomtoza ada mtu ambaye alikuwa ameumia katika sehemu hizo Ksh200,000. Kijana huyo anayeitwa Wanjala, alikuwa anaishi maisha ya umasikini na upweke. Hakika, hangeweza kulipa hiyo ada na ndiposa inatulazimu sisi kama viongozi kutafuta marafiki wenzetu na tuungane pamoja kuhakikisha kwamba tunamchangia pesa za kumsaidia. ...
view
20 Feb 2019 in National Assembly:
Hivi juzi kulikuwa na janga la magaidi pale Riverside. Kuna watu ambao hawangeweza kujimudu hata kulipa ada katika hospitali na ikamulazimu Seneta wa Kaunti ya Nairobi kutoa pesa zake katika mfuko wake kumlipia yule aliyekuwa ameathirika. Kuna wengi ambao hawawezi kutufikia sisi viongozi. Vile ambavyo wengine wamechangia hapa, kuna walemavu miongoni mwao. Kuna wale wametoka katika maisha ya upweke na hawawezi kutufikia sisi viongozi kuwasaidia na senti kidogo kuhakikisha kwamba wanapata matibabu kama watu wengine. Nawaunga wenzangu mkono kwa sababu wakati tunapewa nafasi hii kama viongozi katika Bunge hili, haimanishi kwamba sisi ni matajiri. Sisi pia tumetoka katika maisha ya ...
view
21 Nov 2018 in National Assembly:
Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipa nafasi hii ili pia nichangie kuhusu Mswada huu wa jinsia. Ninashukuru wanenaji ambao wamezungumza mbele yangu kuhusu mambo ya jinsia. Nitaanza kwa kushukuru mwenyekiti wa Kamati ya Sheria na Haki kwa sababu alitupatia maoni ya washika dau ambao alikutana nao akitembea Kenya kukusanya maoni yao. Alisema kwamba The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor.
view
21 Nov 2018 in National Assembly:
walikutana na watu na vikundi karibu 59. Na kutokana na hivyo vikundi 59, vikundi 55 vilikubaliana kwamba mambo ya jinsia lazima yakamilishwe kulingana na Katiba yetu. Mimi pia nitasema hivi kwa wale walioteuliwa katika nyadhifa mbalimbali katika nchi yetu ya Kenya kuanzia kwa Mhe. Cecily Mbarire, Rachael Shebesh and Millie Odhiambo, hawa ni dada zetu waliokuwa wanafanya bidii katika vyama vyao. Walijitolea kuhakikisha kwamba angalau vyama vyao vimepiga hatua katika nafasi yao. Mimi pia nilikuwa nimeteuliwa katika
view
21 Nov 2018 in National Assembly:
ya Kitale. Nikiwa huko, sikukaa kungoja kuteuliwa mara ya pili, nilifanya bidii kuhakikisha kwamba nimesonga kutoka kiwango hicho hadi kiwango kingine. Ndiposa unaona kwamba nimekuwa kama mwakilishi wa akina mama mara ya pili. Na vile dadangu Janet Ong’era amesema, haujui kutoka hapo, itakuwa vipi. Kama wenzetu walivyosema, tukisema jinsia hatumaanishi jinsia moja, ni yote mbili. Wakati ujao utaona kwamba huenda wanawake watachaguliwa katika Bunge hili na wanaume wenzetu wapatikane kwamba ni wachache. Hawa pia watapata nafasi ya kuteuliwa, walemavu wakiwa miongoni mwao. Ninachukua nafasi hii kumshukuru Rais, Naibu wake, Mheshimiwa Raila Amolo Odinga na Kalonzo Musyoka kwa kuamua kwa kauli ...
view
15 Nov 2018 in National Assembly:
Thank you, Hon. Temporary Deputy Chairman. I want to agree with my Committee because I also took part in making the Report. I do not know why we are being misled by others on the issue of children. When you look at child trafficking in this country, it is a big issue which we need to bring our heads together and look for a way forward, so that we can help the children. I oppose the amendment by the professor.
view
13 Nov 2018 in National Assembly:
Hon. Speaker, I rise to ask Question No.134/2018 directed to the Cabinet Secretary for Foreign Affairs. a. Is the Cabinet Secretary aware that there are fresh claims of abuse of migrants in the Middle East leading to loss of lives? b. What is the status of bilateral labour agreements with Middle East countries like Qatar and Saudi Arabia regarding safety of Kenyan migrant workers? c. What measures is the Ministry putting in place to ensure safety of migrant workers, recruiting agencies are licensed by the Ministry and that Kenyans seeking employment in Middle East do so through licensed and registered ...
view