Janet Nangabo Wanyama

Parties & Coalitions

Janet Nangabo Wanyama

She has established the Janet Nangabo Foundation, a community based organization specifically created to provide solutions for problems of the Trans Nzoia people.

All parliamentary appearances

Entries 81 to 90 of 247.

  • 27 Mar 2019 in National Assembly: Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi hii nichangie mjadala huu kuhusu wazee wa mtaa. Kwanza, ninachukua nafasi hii kumshukuru Mhe. Murugara kwa kuleta Hoja hii katika Bunge hili. Miaka miwili iliyopita, tulikuwa na Hoja kama hii katika Bunge hili na hakuna mabadiliko yoyote yalitendeka. Ninafikiria leo tunapojadili Hoja hii, tutahakikisha kwamba imetekelezwa vilivyo kwa sababu vile wenzangu wamechangia katika Bunge hili, ni kweli wanafanya kazi nyingi sana. Katika utoaji wa vitambulisho, wazee hawa wanachukua nafasi ya maana sana kuwatambua wenyeji katika vijini wanavyotoka. Pia wana majukumu makali sana hasa ikija katika mambo ya ugomvi wa nyumbani ... view
  • 20 Mar 2019 in National Assembly: Thank you, Hon. Speaker. I rise to ask Question No. 127/2019 which goes to the Departmental Committee on Defence and Foreign Relations. view
  • 20 Mar 2019 in National Assembly: (Trans Nzoia (CWR) JP): My Question goes to the Cabinet Secretary for Foreign Affairs. (i) Is the Cabinet Secretary aware of fresh claims of abuse of migrants in the Middle East leading to loss of lives? (ii) What is the status of bilateral labour agreements with Middle Eastern countries like Qatar and Saudi Arabia regarding the safety of Kenyans migrant workers? (iii) What measures has the Ministry put in place to ensure safety of migrant workers, licensing of recruiting agencies by the Ministry and that Kenyans seeking employment in the Middle East do so through licensed and registered recruiting agencies ... view
  • 20 Mar 2019 in National Assembly: Hon. Speaker, I stand guided. view
  • 13 Mar 2019 in National Assembly: Asante Mhe. Naibu Spika wa Muda. Nataka kuchukua fursa hii pia kuunga mkono mwenzangu kuhusu mjadala huu kuhusu mambo ya ugonjwa wa kisukari katika nchi yetu ya Kenya. Ni ukweli vile wachunguzi wamesema kuhusu asilimia ya watu ambao wanaugua ugonjwa wa kisukari. Ni ukweli mtupu. Ningeomba kama kiongozi kwamba tuwe na mahali ambapo watu wanaweza kufanyiwa uchunguzi ili wajue hali yao iko namna gani. Vile mwenzangu, Mhe. Tom, amesema, ni kweli ukienda kule mashinani watu hawajui maana ya kupima miili yao. Hivi juzi nilikutana na mmoja wao aliyekuwa akiugua ugonjwa wa kisukari na nikamuuliza kama ameenda kupata matibabu. Alinijibu akasema ... view
  • 13 Mar 2019 in National Assembly: Nataka kugusia maneno ambayo wenzangu wameongea katika Bunge hili kwamba ni chakula tunachokula katika nchi yetu na Kenya na maisha tunayoishi sisi kama viongozi na pia watu wanaohudumia nchi yetu ya Kenya. Wenzangu wamesema kwamba lazima tuwafunze watu jinsi ya kujipima katika jamii ili wasikumbwe na ugonjwa huu wa kisukari na wajikute The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor. view
  • 13 Mar 2019 in National Assembly: hawajaenda katika hospitali zetu kujipima. Ninaungana na wenzangu. Serikali yetu kuu ichukue nafasi yake kuhakikisha kwamba matibabu ambayo tunayasema kuhusu watu wanaogua kisukari yametiliwa maanani. Wenzangu pia wamesema watu wawe wanaspoti, yaani wafanyie miili yao mazoezi. Ninashukuru kwa sababu wanaspoti katika Bunge hili wakati tulienda mazoezi na viongozi wenzetu, tuliona kwamba nchi zingine zinatenga nafasi za watu wao kwenda kufanya mazoezi. Hiyo inatupatia sisi nafasi ya kuhamasisha watu wajue kwamba miili yao inatakikana ifanye mazoezi ili wasikumbwe na mambo kama haya. Hata katika Bunge hili, kuna wale ambao wameathirika miongoni mwetu sisi kama viongozi. Huenda ikawa wengine hawajajua wachukue nafasi ... view
  • 13 Mar 2019 in National Assembly: Ninamshukuru Mhe. Ruweida kwa kuleta Hoja hii katika Bunge hili nasi pia tutoe maoni yetu. Ninajua kwamba hata tukienda mashinani, sisi pia tutapata nafasi. Ninashukuru kuna madhehebu katika nchi yetu ya Kenya, kama vile kanisa la Seventh Day Adventist (SDA), ambayo yana vipimo vya kupima magonjwa katika kanisa hilo. Ninawasihi wachungaji katika nchi yetu ya Kenya watusaidie katika sehemu zao kuhakikisha kwamba vipimo hivi vimeenda mahali hapo. Jambo hilo litatusaidia sana. Nikirudi kwa serikali za kaunti, katika kaunti yangu, watu wanateseka mno. Ukienda sehemu za Kwanza ambako Mhe. Ferdinand anatoka, unaona kwamba tumepoteza watu wengi mno wanaougua ugonjwa wa kisukari ... view
  • 13 Mar 2019 in National Assembly: Asante, Mhe. Naibu Spika wa Muda, niko karibu kumaliza. Nataka kumshukuru mwenzangu na kusema tusiwe tu na mjadala katika Bunge hili lakini alete Mswada ili tukifika kwenye mambo ya Bajeti, tuhakikishe tumetenga pesa. Hii ni kwa sababu katika jamii tuna walemavu ambao hawawezi kutembea mpaka mahali pa matibabu. view
  • 13 Mar 2019 in National Assembly: Kwa hivyo, ninamsihi alete Mswada na tutauunga mkono ili kuhakikisha tunaendelea mbele. Namshukuru mwenzangu, Mhe. Ruweida kwa maoni mazuri ya Hoja hii. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus