Janet Nangabo Wanyama

Parties & Coalitions

Janet Nangabo Wanyama

She has established the Janet Nangabo Foundation, a community based organization specifically created to provide solutions for problems of the Trans Nzoia people.

All parliamentary appearances

Entries 161 to 170 of 247.

  • 5 Mar 2017 in National Assembly: huwa tunapinga sana katika nchi yetu kwa sababu yanatuletea madhara. Unapata mtu amehitimu lakini ukimpa kazi afanye, hafanyi kwa njia sawa kwa sababu hakutumia njia mwafaka ya kuhakikisha kwamba anafika penye amefika. Ninataka kuunga mkono Mhe. Agoi kwa kuleta huu Mswada katika Bunge hili, wa kuhakikisha kwamba tuko na jopo kazi la kuhakikisha kwamba kuna usawa. Iwapo kutakuwa na matatizo ama iwapo tutakuwa na mambo yale yasioeleweka katika nafasi ya mtu kuhitimu ama ya kupewa cheti chake – tunafahamu yaliyompata Mhe. Joho - hilo jopo kazi litasaidia wananchi ambao hawana nafasi ya kujitetea. Tena, ni aibu kubwa sana kwa sababu ... view
  • 23 Feb 2017 in National Assembly: Asante sana, Mhe. Naibu Spika, kwa kunipatia nafasi hii nami pia nichangie Ripoti ya Mheshimiwa Rais. Naungana na wenzangu walionena hapo awali kuhusu mambo yanayoikumba nchi yetu hasa upande wa usalama. Vile wenzangu wamesema ni kweli. Tumekuwa na changamoto katika upande wa usalama katika nchi yetu ya Kenya. Mhe. Naibu Spika, unakumbuka kwamba miaka miwili iliyopita tulikuwa na shida ya usalama katika Kaunti ya Bungoma. Watu walikuwa wanuawa kiholela. Mwishowe Serikali ilisadia angalau kuweka mikakati ya kuhakikisha kwamba mambo ya kuuana katika Kaunti ya Bungoma yameisha. view
  • 23 Feb 2017 in National Assembly: Mhe. Naibu wa Spika, ningependa kumshukuru Rais kwa sababu ya mikakati ambayo amejaribu kuweka licha ya kuweko kwa shida ya wanamgambo wa Al Shabaab katika nchi yetu. Mwenzangu alisema kuwa Raisi, akiwa Amiri Jeshi Mkuu, hakusema pole kwa wale waliopoteza maisha yao kwenye shambulizi la hivi juzi lililotekelezwa na wanamgambo wa Al Shabaab dhidi ya wanajeshi wetu kule Somalia. Rais alikuwa mstari wa mbele kupokea mili ya askari wetu waliouawa kule Somalia. view
  • 23 Feb 2017 in National Assembly: Ningependa kuongea kuhusu ufisadi katika nchi yetu ya Kenya. Ni kweli kwamba ufisadi umekita mizizi katika nchi yetu ya Kenya, lakini hiyo haimaanishi kwamba ufisadi umeletwa nchini na Mhe. Rais. Ufisadi unapatikana hata kwenye nyumba zetu, na hata makanisani. Ningependa kuishukuru Serikali kwa kuhakikisha kwamba wale wanaopatikana na makosa ya ufisadi wanachukuliwa hatua kulingana na sheria. Kwa sababu ya ugatuzi, katika nchi yetu kumekuwa na changamoto chungu nzima. Utaona kwamba watu ambao wameajiriwa na viongozi wenzetu wamejipatia utajiri kwa njia isiyo halali. Ningependa kusema kwamba sisi, kama viongozi, ni lazima tushikane bega kwa bega kuhakikisha kwamba tunapambana na ufisadi katika ... view
  • 23 Feb 2017 in National Assembly: Ningependa kuzungumzia mazingira yetu. Tangu Jubilee ichukue uongozi mwaka wa 2013, mazingira katika nchi yetu ya Kenya yamelindwa vilivyo. Hapo awali, ungeona watu wanakata misitu yetu ili wapate makaa ama kuni. Hivi sasa, watu hawavamii misitu na kukata miti. Hii inamaanisha uhaba wa maji hausababishwi na kutotiliwa maanani suala la kuhifadhi mazingira. Sisi, Wabunge tunaowakilisha kaunti, tungependa kumshukuru Rais kwa sababu baadhi yetu tulihakikisha kwamba tumeongea na Rais kwa sababu ya kazi yetu inayo tulazimu kutembelea sehemu zote za kaunti nzima, ndiposa akatupatia hazina ambayo tunatumia kama viongozi wa kaunti. view
  • 25 Oct 2016 in National Assembly: Ahsante Mhe. Naibu Spika kwa kunipa nafasi hii nichangie mjadala huu wa jinsia ya kike. Nakubaliana na mnenaji, ndugu yangu Mheshimiwa aliyeongea kuhusu Mswada huu ulioletwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Masuala ya Kisheria. Kama kiongozi katika Bunge hili, natumai wenzangu kule nje wananisikiliza ndiposa tuwaambie nini kinachoendelea. Jumamosi iliyopita, nilikuwa Bungoma kwa hafla ya mazishi mahali fulani. Mama mmoja aliamka akasema kwamba wale akina mama ambao wako Bungeni hawataki kushughulikia masuala ya akina mama kule nje. Alisema kwamba tuwe na akina mama wengi ndiposa sauti zetu zisikilizwe katika Bunge. Niliwahakikishia wananchi kwamba viongozi ambao tuko Bungeni, haswa akina mama, ... view
  • 25 Oct 2016 in National Assembly: Tumeelezwa kuwa kuna mtu ambaye alienda mahakama kutaka kujua kwa nini tumechelewa kutekeleza Katiba hii. Nimeshangaa sana kusikia wenzetu wakisema kuwa Katiba hii ni mbaya kwa asilimia 20. Kwa nini waliipitisha Katiba hiyo na makosa hayo bila kuangalia uongozi wa wanawake? Wanawake lazima wawe na nyadhifa mbalimbali katika nchi yetu. Ni lazima tuwatendee haki akina mama ambao ni viongozi nchini. Katika eneo langu, akina mama ambao ni viongozi ni wachache sana. Nilikuwa diwani, lakini sikubaki hapo kwa sababu nilihakikisha kuwa nimepigania kiti na nikachaguliwa kama mwakilishi wa akina mama katika kaunti. Tusilale bali tuhakikishe kuwa masuala yetu yanatekelezwa. Tukiwa kule ... view
  • 9 Aug 2016 in National Assembly: Asante Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi hii ili nichangie Mswada huu ulioletwa na Mhe. Duale. Kama wanenaji wa kwanza walivyosema, ni kweli kuna ufisadi katika nchi yetu. Watu wanachukua pesa za umma na kufanya mambo ya kuwafaidi wenyewe. Utakuta mtu ameajiriwa leo na kesho amenunua nyumba kubwa ama gari la kifahari. Mswada huu utatusaidia kurekebisha baadhi ya mambo kama haya katika nchi yetu. Wawekezaji katika nchi yetu hawana imani na Wakenya kwa sababu wanapoleta pesa zao na kuwachagua watu wa kusimamia, watu wetu wanachukua hizo pesa na kuzitumia kujinufaisha. Tukiwa na sheria kama hii, nchi yetu itaendelea ... view
  • 9 Aug 2016 in National Assembly: yetu ya Kenya. Mswada huu utabadilisha nchi yetu na watu kutoka nje watatamani kuwekeza hapa nchini. Sisi tutajivunia nchi yetu kwa sababu maisha yetu yatabadilika. Watakaoajiriwa kwa ofisi hizi wanatakikana wawe watu wa nidhamu na watu ambao wamepitia majukumu yao kwa kazi nzuri. Tukiajiri mtu tu kwa sababu heunda ana karatasi zifaazo, mwishowe, hataweza kuzitumia zile karatasi bali atakuwa akiiba pesa za Wakenya. Watakaowekwa katika bodi hii wanatakikana wawe watu walio na nidhamu ya kutosha na watu ambao wataweza kufanya kazi kuendesha nchi yetu mbele. Tunahitaji kuwa na watu wenye nidhamu. Hata kwa mashule yetu, huenda usimamizi ukawa sio mzuri ... view
  • 9 Aug 2016 in National Assembly: Kwa hayo machache, ninaunga mkono Mswada huu. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus