Janet Nangabo Wanyama

Parties & Coalitions

Janet Nangabo Wanyama

She has established the Janet Nangabo Foundation, a community based organization specifically created to provide solutions for problems of the Trans Nzoia people.

All parliamentary appearances

Entries 31 to 40 of 247.

  • 11 Mar 2021 in National Assembly: Thank you, Hon. Temporary Deputy Speaker. I support the Bill. view
  • 4 Mar 2021 in National Assembly: (Trans Nzoia (CWR), JP): Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi hii nichangie Mswada huu kuhusu mihadarati. Ninataka niungane na wenzangu wale wameshukuru Kamati ya Usalama. Wamefanya kazi nzuri sana kuhusu haya mambo ya mihadarati katika nchi yetu ya Kenya. view
  • 4 Mar 2021 in National Assembly: Vile wanenaji wa kwanza wamesema, ni kweli watoto wetu na watu wa rika zetu wameumia. Iwapo sheria kama hii italetwa katika Bunge letu ama nchi yetu, tutazuia hao wakora ama wahalifu ambao wanakuja kunyanyasa watoto wetu. Hao watu wanalenga vyuo vikuu katika nchi yetu ya Kenya. Hivi majuzi, mama alitafuta mtoto wake kwa miaka miwili na kumbe alikuwa ameharibikia hapa katika kaunti ya Nairobi. Watoto wetu wamekuwa wateja wao wa kuwaletea hii mihadarati. Nimefurahi kwa sababu Kamati imeweka faini ya kuhakikisha kwamba walanguzi na wanaotumia dawa za kulevya hawataenda nje ya mkono wa sheria. Watashikwa, kushtakiwa na kutoa faini ya ... view
  • 4 Mar 2021 in National Assembly: Watu wanaongea kuhusu Pwani. Sio Pwani peke yake ambapo watu wanatumia mihadarati. Ukija upande wa magharibi katika eneo Bunge la Ikolomani ama Kaunti ya Trans Nzoia, utaona kwamba tumepoteza vijana wetu, kwa sababu wanatoka shule na wanatumia mihadarati. Hawamalizi hata masomo yao. view
  • 4 Mar 2021 in National Assembly: Ninataka pia kukubaliana na wenzangu wale wamesema jinsi ya kupata ujumbe. Hiki ni kitu cha maana mno. Iwapo tutakuwa na mahali pa kupata huu ujumbe kwamba ni fulani ambaye anahusika na jambo fulani ama yule anatoa hii mihadarati na kuuza, itakuwa ni jambo la maana sana. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor. view
  • 4 Mar 2021 in National Assembly: Pia, ninataka kuungana na wenzangu ambao wamesema kwamba kuna watu wanakodesha nyumba mahali iwe kama ofisi yao ya kuleta hii mihadarati halafu waitoe hapo na wapeleke kwingine. Ninaona ni vyema hata hao ambao wanapeana nyumba zao wachunguze ni biashara gani inaendelea katika mahali hapo. view
  • 4 Mar 2021 in National Assembly: Waheshimiwa wameongea kuhusu maofisa ambao wanafaa washike doria ama kuchunguza hao watu wa kuleta mihadarati. Wenzangu wamesema kwamba hapo awali kulikuwa na wale wanatengeza biashara. Wakipata hii mihadarati na kuuza, wanapewa kitu kidogo. Kwa sababu tunaweka hii sheria saa hii, hata hao askari wataogopa. Wakipatikana, watapoteza kazi na hata wengine pia watafungwa jela. Hii sheria italeta manufaa katika nchi yetu ya Kenya. Itafanya sisi, kama viongozi katika Bunge hili, tuhamasishe watu kule nje. Wengine hawatajua kwamba tuko na sheria kama hii na mwishowe watatumia watoto wetu. Nilishukuru sana Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama, Mhe. Koinange leo asubuhi. Alisema kwamba wanaoendesha ... view
  • 4 Mar 2021 in National Assembly: Wakati wa Krismasi, vijana kutoka Nairobi walienda nyumbani na pikipiki zao. view
  • 23 Feb 2021 in National Assembly: Asante, Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi hii nichangia Mswada huu wa maktaba katika nchi yetu ya Kenya. Vile wanenaji waliotangulia wamesema, ni muhimu tuwe na maktaba katika nchi yetu ya Kenya. Ni kweli watoto wetu wameharibika kwa sababu hawajapata nafasi ya kuenda kusoma katika maktaba mahali popote. Wengi wamerudi kuvuta bangi. Wengine wamerudi kwenda tu kunywa pombe. Nilitembea ng’ambo kule England na nikaingia katika maktaba katika nchi hiyo na nikaona kwamba iko na vifaa ama vitabu vile vinatosha kabisa kusema hata historia katika nchi hiyo na hata historia ya viongozi katika nchi hiyo. Ndiposa, kama sisi pia ... view
  • 23 Feb 2021 in National Assembly: Asante, Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi hii nichangia Mswada huu wa maktaba katika nchi yetu ya Kenya. Vile wanenaji waliotangulia wamesema, ni muhimu tuwe na maktaba katika nchi yetu ya Kenya. Ni kweli watoto wetu wameharibika kwa sababu hawajapata nafasi ya kuenda kusoma katika maktaba mahali popote. Wengi wamerudi kuvuta bangi. Wengine wamerudi kwenda tu kunywa pombe. Nilitembea ng’ambo kule England na nikaingia katika maktaba katika nchi hiyo na nikaona kwamba iko na vifaa ama vitabu vile vinatosha kabisa kusema hata historia katika nchi hiyo na hata historia ya viongozi katika nchi hiyo. Ndiposa, kama sisi pia ... view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus