John Kinyua Nderitu

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 1791 to 1800 of 2259.

  • 17 Feb 2021 in Senate: Sheria hizi zinapendekeza kwamba watu watakaopewa majukumu ya kusimamia mashirika haya wawe wenye tabia, nia na mienendo sawa. Wasimamizi wa vyama vya ushirika wanapaswa kufanya kazi zao kwa ungalifu bila ya kuwa na tamaa au nia mbaya. Mara kwa mara, wakuu wa vyama vya ushirika hupatwa na nia mbaya baada ya kuanza kushughulikia hela ambazo wanachama wameleta kwa pamoja. view
  • 17 Feb 2021 in Senate: Sheria anayopendekeza Sen. (Dr.) Zani, italainisha sheria hii na katiba yetu. Pili, Wakenya wengi wanategemea sana vyama vya ushirika. Kwa mfano, wenye mapato madogo kama wandeshaji boda boda na wachuuzi wengi sokoni. Sheria nzuri ikiwepo, wengi wao watanufaika kwani hakutakuwa na watu ambao wanataka kujitajirisha kwa mali ya wengine bila kutumia sheria. view
  • 17 Feb 2021 in Senate: Jambo lingine ni kwamba watu wanaofanya biashara moja wataweza kujuana zaidi. Makundi ya wanabodaboda, wachunaji wa majani chai na wengine wa vyama vya ushirika watauza mazao yao pamoja. Kwa hivyo, itakuwa vizuri kuwa na sheria zitakazofuatilia mambo yatakayokuwa yakitendeka. Nampongeza Sen. (Dr.) Zani kwa kuleta Mswada huu. Hiyo inamaanisha kwamba Katiba yetu pamoja na Sheria ya Vyama vya Ushirika vizingatie kaunti zetu ambazo tunawakilisha. Asante Bi. Spika wa Muda. view
  • 11 Feb 2021 in Senate: Bw. Spika wa Muda, nashukuru kwa kunipa fursa hii. Kwanza kabisa, nataka kumpongeza Sen. Wambua wa Kitui kwa kuleta Mswada huu. Kwa kweli, Serikali inasema tunahitaji usalama wa chakula. Kitu ambacho kitasaidia zaidi ni mimea ambayo inahitaji mvua kidogo ama maji yasiyo mengi, ili iweze kuwa katika kipaombele ya hili jambo ambalo linasemwa na Serikali. Ndengu inaweza kukuzwa katika sehemu nyingi. Sehemu nyingi za Kenya ni za ukame. Ukienda Laikipia, Isiolo, Marsabit, Tharaka-Nithi, Kitui na Machakos, ndengu inaweza kupandwa na itafanya mambo mawili. Jambo la kwanza ni kuwa watu ambao wanasema kuna ukosefu wa kazi watapata kazi ya kufanya. Jambo ... view
  • 11 Feb 2021 in Senate: kupigana na mchakato wa hustlers ama wanyonge au walala hoi kwa sababu watafaidika sana na sisi kama Seneti tunafaa kupitisha Mswada huu bila kupoteza wakati. Itasaidia Wakenya wengi. Nchi yetu ya Kenya itapata mapato kwa sababu watu wengi wataanza kufanya kilimo biashara. Kilimo biashara itawezekana kwa mimea ambayo haihitaji mvua nyingi, kwa sababu sehemu nyingi za Kenya hazina mvua ya kutosha. Kwa hivyo, mimi naunga mkono Mswada huu. Nataka kuambia Sen. Wambua kuwa hii juhudi ni nzuri sana. Amechelewa na angefanya hivi mwaka wa kwanza tulipoingia hapa. Hata hivyo, ni vizuri kwa sababu tunaweza kuchukua fursa hii kuleta mabadiliko katika ... view
  • 11 Feb 2021 in Senate: Mr. Temporary Speaker, Sir, from what he is saying, what is wrong with that because trade is willing seller and willing buyer? Is there a problem with that? The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view
  • 21 Dec 2020 in Senate: Asante sana, Bi. Naibu Spika kwa kunipa fursa hii. Kwanza kabisa, ningependa kutuma rambirambi zangu na za familia yangu na watu wote wa Laikipia kwa familia ya mwendazake Sen. (Dr.) Kabaka, pamoja na watu wa Machakos. Jambo ambalo ninakumbuka kuhusu Sen. (Dr.) Kabaka ni kwamba alikuwa mtu mkarimu sana. Ninakumbuka wakati ndugu yetu, mwendazake Sen. Oluoch, alipotuacha, Sen. (Dr.) Kabaka alijitolea kulipa karo ya wanafunzi wa mwendazake. Ninakumbuka aliandika hundi ya kusaidia. Ukarimu wake ulijitokeza vizuri sana. Ninamkumbuka kama msomi. Tulisafiri naye katika nchi ya Australia. Tulipokua huko, aliniambia kitu kizuri zaidi. Alienda kwenye maktaba na akanunua vitabu vya wanasheria. ... view
  • 16 Dec 2020 in Senate: Mr. Speaker, Sir, we are here to listen. That is why we want the questions to be asked, so that we can follow. Somebody should not assume any role. We are here to listen. You learn a lot by listening. That is why I am here keenly listening. Any question that they can ask, we are here to listen and that is why we set this day to listen, so that we can be clear in what is being discussed. We will make a decision after listening. However, nobody should insinuate sinister motive about anything that somebody asks. We are ... view
  • 16 Dec 2020 in Senate: Mr. Speaker, Sir, even watching videos, we can still watch videos. view
  • 16 Dec 2020 in Senate: Asante Bi. Naibu Spika. Nimesoma ushahidi wote ambao tulipewa, lakini mambo ambayo ninasikia sasa ni hekaya na historia. Tulipenda tufuatilie ushahidi tuliopewa. Tumeusoma usiku kucha, halafu yale tunayosikia sasa ni hekaya. Tufuatilie ushahidi ulioko hapa. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus