2 Oct 2019 in Senate:
Asante sana, Bi Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii ili kuunga mkono Mswada huu. Kwanza, ninataka kushukuru mheshimiwa kwa sababu Mswada huu unapendekeza kuwa sehemu fulani zitatengewa wachuuzi rejareja wafanyie biashara zao. Pili, Mswada huu unapendekeza kwamba sehemu ambayo itatengewa wachuuzi rejareja inapaswa kuwa na vyoo vya kutumia na usalama. Hii ni kwa sababu inavunja moyo kwa mtu yeyote kuambiwa afanye kazi mahali ambapo hakuna usalama na vyoo vya kutumia. Jambo lingine ni kwamba ukitembea katika sehemu nyingi huku Kenya, utaona kwamba wachuuzi rejareja wanaishi maisha ya kukimbizwa kila wakati; wanaishi maisha kama ya swara. Unapata kwamba askari wa ...
view
2 Oct 2019 in Senate:
Seneta wa Kakamega amesema kwamba sisi hatuna haja ya kuujadili Mswada huu. Nataka kumkosoa kwamba sisi tuko na haki ya kuujadili Mswada huu, kwa sababu tuna jukumu la kuwaangalia wachuuzi wa reja katika kaunti zetu kwa sababu ugatuzi umekuja. Hizo ni sehemu ambazo tutaziangalia. Kwa hivyo, naiomba Kamati inayohusika iaangalie zile sehemu zinazosema kwamba Waziri wa Serikali Kuu ndiye atakayehusika. Tuko na mawaziri wetu katika kaunti zetu, na watayaangalia mambo haya kwa marefu na mapana. Ni vizuri ijulikane wazi kwamba sisi, kama Seneti, tunapaswa kuangalia mambo haya ndio tuweze kuwa na usawa katika nchi yetu ya Kenya, na katika kaunti ...
view
2 Oct 2019 in Senate:
Asante sana, Bi. Spika wa Muda.
view
2 Oct 2019 in Senate:
Kwa hoja ya nidhamu, Bw. Spika wa muda. Ningependa kuuliza, kwa sababu kuna lugha ambayo inatumiwa na Mheshimiwa Sen. Shiyonga ambayo sisi hatuifahamu, kwani sio Kiingereza wala Kiswahili. Sijui ni lugha gani---
view
2 Oct 2019 in Senate:
Nimeskia akisema chungaring; sijui kama hicho ni Kiswahili, kwani sielewi. Ningependa atueleze ni lugha gani hiyo, kwani hatuifahamu.
view
2 Oct 2019 in Senate:
Asante, Bw. Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii. Kwanza kabisa natoa risala zangu za rambirambi kwa familia ya mwendazake mama Mariam pamoja na mwanawe. Kwa niaba yangu na ya watu wa Laikipia Kaunti, ninasema pole sana kwa familia.
view
2 Oct 2019 in Senate:
Nampongeza Seneta wa Mombasa kwa kuleta Hoja hii. Ni jambo la kushangaza kwamba jambo hili lilipotendeka tukiangalia katika zile picha ambazo zilipigwa na kusambazwa zinaonyeshana kwamba kulikuwa na muda wa dakika kadhaa kabla ya gari kuzama kabisa. Najiuliza kama pale hapakuwa na wapiga mbizi ambao wangewaokoa mama na mtoto walipokuwa wakizama. Pili, tunaambiwa kwamba katika sehemu ile kuna wanajeshi wetu ambao wanalinda mipaka baharini. Walifanya nini?
view
1 Oct 2019 in Senate:
On a point of order, Mr. Speaker, Sir.
view
1 Oct 2019 in Senate:
Thank you, Mr. Speaker, Sir. I am a Member of the Committee on Education and have heard what Sen. Sakaja has said. I have taken note of it and we will respond accordingly.
view