6 Aug 2019 in Senate:
Asante sana, Bw. Naibu Spika, kwa kunipa fursa hii. Nataka kuchukua fursa hii kuunga mkono Taarifa hii iliyoletwa na Seneta wa Mombasa. Ni ukweli mtupu kuwa tukiondoa hiyo shughuli ya watu kupewa vibali kutoka Mombasa na kuileta Nairobi, hii itafanya vijana wa sehemu ile kukosa kazi kwa sababu hii shughuli inatendeka Mombasa. Itasababisha vijana waliokuwa wakifanya ile kazi kuwa walalahoi. Kwa hivyo, ni vizuri wakati Serikali inapotarajia kufanya jambo lolote, izingatie jinsi inavyowaathiri watu wa sehemu ile. Jambo lingine ni ya kwamba ikiwa tuna Kaunti 47, tunafaa tuzipatie zote kipaombele kwa sababu Mombasa ndipo kuna ziwa na mambo yote yanatendeka ...
view

30 Jul 2019 in Senate:
Mr. Speaker, Sir, this is a very good Statement. I urge the Committee to get information on the qualification of the heads of those institutions as well. The Statement will ensure that the opportunities that are available are distributed throughout the country.
view
30 Jul 2019 in Senate:
Asante sana, Bw. Spika. Nachukua fursa hii kutuma risala zangu za rambirambi na watu wa Laikipia kwa mwenda zake, Gavana Laboso and mwenda zake, mhe. Ken Okoth. Jambo la kuvunja moyo ni kwamba wote waliathiriwa na ugonjwa wa saratani. Sisi tuliobaki, tunafaa kujiuliza ni nini tunaweza kufanya kupigana na janga la ugonjwa wa saratani. Ugonjwa wa saratani umekuwa kizungumkuti kwetu sisi.
view
30 Jul 2019 in Senate:
Bw. Spika, ni muhimu kwa kaunti zote 47 kuweka mahabara za kuchunguza ugonjwa wa saratani kwani jambo hili lasumbua sana.
view
30 Jul 2019 in Senate:
Bw.Spika, nakubaliana nawe kabisa. Sitaki kujadili swala la ugonjwa wa saratani kwa mapana na marefu sasa hivi.
view
30 Jul 2019 in Senate:
Namkumbuka Gov. Laboso kwa utendakazi wake. Mwezi wa Julai mwaka jana, tuliungana naye katika kungamano la magavana kule Marekani na niliona kwamba alijitolea mhanga kufa kufanya kazi yake kwa makini na ueledi mwingi.
view
30 Jul 2019 in Senate:
Bw. Spika, sikuwa nimekutana na mwenda zake, Mbunge wa Kibra, lakini kutokana na yale nimesikia kumhusu, alikuwa mtu aliyefanya kazi yake kwa kujitolea. Alikuwa mtu aliyependa kutabasamu kwani alikuwa mtu wa furaha. Ni vyema sisi kama viongozi kujifunza kwamba mtu anapopewa jukumu, anatakiwa kulitekeleza kwa umahiri mkubwa. Sina mengi ila kusema kwamba Mungu azilaze nyoyo zao mahali pema peponi.
view
30 Jul 2019 in Senate:
Asante sana, Bw. Spika. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view