19 Mar 2019 in Senate:
Asante, Bi. Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii. Kwanza kabisa, hili ni jambo la kuvunja moyo kwa sababu katika nchi yetu ya Kenya, kama vile Mwenyekiti wa Kamati ya Ukulima, Mifugo na Samaki alivyonena, kuna sehemu zinazoendeleza ukulima na wakulima hupata mavuno tele. Ni kweli kwamba kuna shida katika maeneo ya Turkana na Baringo na ni aibu kuona watu wakifa kulingana na picha kunazotumiwa. Sen. (Prof.) Ongeri atakueleza kwamba kabla mtu hajafa kwa kukosa chakula, mafuta ya mwili huwa yanatumika. Baada ya mafuta kutumika huwa ni nyama na hatimaye mifupa. Baada ya mifupa kutumika akili hutumika ndio maana unamwna ...
view
19 Mar 2019 in Senate:
Sasa hivi ukimwuliza gavana yeyote kutoka maeneo yaliyoathirika, atakwambia anatafutia watu wake chakula. Hili ni jambo la kuvunja moyo kwa sababu tulidhania kuwa ugatuzi utafanikisha watu kuwa na chakula. Sasa hivi, kila mtu ananyooshea Serikali ya kitaifa kidole. Inafaa magavana na hata maseneta waelezee watu wanachofanya. Najua kuwa hata Laikipia kuna shida kwa sababu nimekuwa nikiambiwa. Mimi mwenyewe nina jukumu la kufuatilia jinsi Gavana anatumia hela zinazofaa kutumiwa wakati wa dharura. Hata hivyo, Serikali ya kitaifa ina jukumu kwa sababu mwaka jana kuna taasisi za Serikali zilizotutahadharisha kutokana na hali ya hatari. Tuliambiwa kuwa kutakuwa na athari za ukame lakini ...
view
19 Mar 2019 in Senate:
Mimi kama Mwenyekiti wa Kamati ya Ugatuzi na Mahusiano ya Kiserikali, nafaa kumwita Waziri anayehusika kwa sababu tumemwona akijihusisha na ugavi wa chakula. Anafaa kuja hapa ili atuelezee kinaga ubaga nini amefanya kwa sababu watu wanaendelea kudhoofika na kusononeka kutokana na ukosefu wa chakula licha ya kwamba kuna sehemu zingine za Kenya ambapo watu wana chakula lakini Serikali hainunui. Maana ya serikali katika nchi ni kuhakikisha kuwa watu wake wanapata lishe The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view
19 Mar 2019 in Senate:
na usalama. Ikiwa Serikali imeshindwa, iwe Serikali ya kitaifa au serikali za magatuzi, inafaa tujue kuwa serikali fulani imeshindwa na kazi yake.
view
19 Mar 2019 in Senate:
Kule kwetu Laikipia, kuna athari za janga hili lakini sisi tuko ngangari. Hata hivyo, kila mtu anapaswa kujitolea. Ikiwa serikali imeshindwa, basi tunafaa kuambiwa ili tufanye kama ilivyofanywa wakati fulani wakenya walipojitolea kuwapa msaada wenzao. Mpango huo ulijulikana kama Kenyans for Kenya .
view
14 Mar 2019 in Senate:
Mr. Speaker, Sir, there were requests for Statements by Sen. (Dr.) Zani from my Committee, which you did not commit to it. Sen. (Eng.) Mahamud suggested that we can do a joint Committee. You did not give a ruling.
view
14 Mar 2019 in Senate:
Thank you, Mr. Speaker, Sir.
view
13 Mar 2019 in Senate:
Ahsante sana, Bw. Spika. Ninataka kukubaliana na Naibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Afya kwa sababu ni ukweli ya kwamba tulikuwa na mkutano na tulijadilia maswala ambayo yametajwa hapa. Pia, amesema yakwamba tutazingatia mambo ambayo yametajwa hapa. Seneta wenzangu wanasema ya kwamba ni kama alikunywa chai na hakukua na mkutano ambao ulipaswa kufanyika. Sio ukweli alivyosema Sen. Cherargei ya kwamba tulijua ya kwamba haya maneno yangefanyika. Tulijadiliana hayo mambo kwa sababu hayo ndiyo mambo ambayo tunayafuata na tunayatekeleza kama Kamati. Kwa hivyo, hatuwezi kusema ya kwamba Naibu wa Mwenyekiti alifanya jambo la makosa. Tulikuwa tukitekeleza kazi ambazo tunapaswa kutekeleza na ...
view
13 Mar 2019 in Senate:
On a point of order, Mr. Speaker, Sir. I just want to inform the good Senator of Makueni County that it is not KEBS that certifies medicine, but Pharmacy and Poisons Board (PPB).
view