25 Oct 2022 in Senate:
Thank you, Mr. Deputy Speaker, Sir. Ninamshukuru Sen. Thang’wa kwa kuelewa ya kwamba bendera iliyoko pale sio ya Kaunti yake. Kwa hivyo, anafanya kazi yake ya oversight na kuangalia kila mahali. Ninakumbuka nilipokuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Ugatuzi, nilikuwa nikiangalia mambo kwa kindani. Bw. Naibu wa Spika, kumekuwa na shida katika Kaunti yako kati ya Gavana na madiwani. Gavana Mwangaza alipoanza kutoa hotuba yake, madiwani wote walitoka nje mara moja. Sisi kama Maseneta, kazi yetu ni kuangalia vile kaunti zetu zinaendelea. Bw. Naibu wa Spika, huenda ikuwe vigumu wewe kusema, lakini nimeona niseme kwa sababu jambo hilo silo nzuri. Kwa ...
view
25 Oct 2022 in Senate:
Bw. Naibu Spika, nimesimama katika Hoja ya Nidhamu na Sen. Olekina anaelewa sana kuliko mwingine yeyote.
view
25 Oct 2022 in Senate:
Bw. Naibu wa Spika, mambo ya Kaunti ya Meru yanapaswa kuangaliwa kwa kina. Wakae chini na waelewane.
view
25 Oct 2022 in Senate:
Bw. Naibu wa Spika, ndio niweze kuweka mambo haya bayana, ni vyema niseme ya kwamba nilikuwa diwani wa sehemu inayoitwa Mutara. Pia nilikuwa Mwenyekiti wa Kaunti ya Laikipia. Kwa hivyo, Sen. Olekina aelewe hayo. Naona Sen. Madzayo anababaika. Bw. Naibu wa Spika, nataka kwanza kuunga mkono taarifa iliyotolewa kuhusu janga la njaa. Ni ukweli kuwa kuna janga la njaa. Ukitembea sehemu nyingi ya Jamhuri ya Kenya kama Kaunti ya Laikipia, Narok, Lamu na sehemu nyinginezo, utaona ya kwamba tuko na hili janga la njaa. Kwa hivyo, tungeomba Serikali inunue mifugo kutoka kwa wale walio na wanyama, hasa katika sehemu za ...
view
25 Oct 2022 in Senate:
The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view
25 Oct 2022 in Senate:
Madiwani waliohudumia nchi ya Kenya, kama vile Sen. Wambua alivyosema, walikuwa zaidi ya 12,000. Lakini tunapoongea hivi sasa, 9,000 ndio waliobaki na wanaishi maisha ya umaskini na ufukara. Ukitembea sehemu zingine, utawapata wameajiriwa kuchunga mifugo au kazi za kuosha nguo. Tunaomba waangaliwe na wafidiwe. Kama vile, Sen. Wambua, alivyosema, wajumuishwe na wazee wengine wakati wanapewa tiba ya NHIF. Ni vizuri niwaambie Masenata walioko hapa kwamba Mhe. Najib Balala, Mhe. Maina Kamanda na pia Sen. (Dr.) Oburu kutoka Siaya walikuwa madiwani.
view
25 Oct 2022 in Senate:
Bw. Spika wa Muda, Madiwani wanafaa waangaliwe ili waweze kuendelea kufanya kazi zao. Tutasimama nao, tutawatetea hadi wapate haki yao. Sen. Olekina ni mtetezi wa wanyonge. Kwa hivyo, ninamuomba awatetee Madiwani kwa sababu hata kule anakotoka, Narok, kuna madiwani. Wamekuwa wakinipigia simu, wakisema wanataka kuwasikia Maseneta wa Narok, Kilifi, Siaya na Nairobi wakiongea. Wanataka kusikia Maseneta wa kwao wakisema neno kuhusu Madiwani. Asante sana, Bw. Spika wa Muda.
view
25 Oct 2022 in Senate:
Mr. Temporary Speaker, Sir, on a point of information.
view
25 Oct 2022 in Senate:
Mr. Temporary Speaker, Sir, last year, I brought in a Motion, which was canvassed in the House.
view
19 Oct 2022 in Senate:
On a point of order, Mr. Speaker, Sir,
view