6 Aug 2015 in National Assembly:
Thank you, Hon. Temporary Deputy Speaker. I stand to support this Motion. Good leadership entails many things. For us to pass this Motion, we want to demonstrate the kind of leadership we want to have in this country. When you talk about good leadership, you talk about transparency. Without rules and laws that will govern our leadership, transparency will be history in our country.
view
6 Aug 2015 in National Assembly:
The problem we have in this country is lack of accountability. Leaders are not ready to be accountable for the mistakes that they make or for the pronunciation of words that bring hatred and tribalism among our people. When this Motion goes through, our people will learn to be accountable for their words and also for the resources that are entrusted to them by the w ananchi. When you talk about good governance, you also talk about integrity. When we talk about governance, we bring the issue of integrity in place. Without integrity, you cannot have good governance. We want ...
view
6 Aug 2015 in National Assembly:
This country must maintain law and order. If people do not follow the law, our country will be ruined. That is why this country almost went into the abyss in 2007. With those few remarks, I support.
view
30 Jul 2015 in National Assembly:
Mhe. Naibu Spika wa Muda, ninashukuru kwa kunipatia nafasi hii. Nitachangia Hoja hii kwa ufupi. Kwanza, ningependa kuishukuru Kamati ya Mhe. Gumbo kwa kuleta Ripoti hii wakati huu. Imechukua muda sana. Ningependa kusema kwamba ni lazima tutunze na tutumie rasilimali ya Kenya vizuri. Hilo ni jambo ambalo linajulikana na kila mtu katika nchi hii. Mmoja wa wananchi ambaye anaweka mkazo katika kutunza rasilimali ya nchi hii ni Naibu wa Rais. Kila mara akitumia chochote katika nchi hii anakitumia kwa njia iliyo safi na kwa njia ya heshima. Jambo hili lilileta joto jingi katika nchi hii ya Kenya kisiasa kwa sababu ...
view
7 Jul 2015 in National Assembly:
Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda, ningependa kuchukua nafasi hii kumshukuru Mheshimiwa Wanjiku kwa kuleta Hoja hii. Tunapinga pombe haramu kwa uwezo The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor.
view
7 Jul 2015 in National Assembly:
ambao tulionao na kwa lugha yote tunayoweza. Ningependa kusema mambo mawili. Jambo la kwanza ni kuwa kuna askari ambao wamechukua nafasi hii kunyanyasa wananchi. Wanaenda kushika wenye pombe lakini pia wanawanyanganya pesa na kuwaharibia mali yao. Lazima tuchunge askari kama hao ambao wananyanyasa wananchi.
view
7 Jul 2015 in National Assembly:
Jambo la pili nikuwa kuna watu wa aina mbili katika jambo hili. Kuna watu ambao wanatengeneza pombe kwasababu ni maskini. Pia, kuna watua mbao wanakunywa pombe kwa sababu wana pesa. Ningependa serikali za kaunti na Serikali Kuu zihakikishe kwamba kuna njia ambazo zinasaidia watu ambao wanatengeneza pombe kujimudu kimaisha. Ni njia moja kusimamisha watu wasikunywe ama wasitengeneze pombe lakini ni njia nyingine uchumi wa sehemu hiyo uangaliwe kwasababu kuna watu ambao wanatengeneza pombe kwa sababu ya umaskini. Ni bora serikali za kaunti na Serikali Kuu zijaribu njia za kusaidia watu wa namna hiyo ili wajimudu kimaisha.
view
7 Jul 2015 in National Assembly:
Nikimalizia, ningependa kukubaliana na wengine kwamba hili jambo ni janga. Kwa hivyo, ukitoa mtu katika shida lazima pia uwe na njia ya kumsaidia kujimudu kimaisha. Leo huyu mtu ameacha pombe lakini kesho atarudia pombe. Kwa hivyo, ni vizuri hao watu wapelekwe katika shule ama mahali pa kupatiwa mawaidha pole pole na waache pombe. Kwa hivyo, ninaomba Serikali ifungue vituo vya kuwasaidia hao watu na wapatiwe ushauri ili wawe watu wazuri. Ninaunga mkono Hoja hii. Asante
view
24 Jun 2015 in National Assembly:
Asante sana Mhe. Naibu wa Spika wa Muda, kwa kunipatia nafasi hii ili nichangie Hoja hii. Kwanza, ningependa kumshukuru Mhe. Abdul Rahim Dawood kwa kuleta Hoja hii ambayo ni muhimu sana katika nchi yetu ya Kenya.
view
24 Jun 2015 in National Assembly:
Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda, jambo la kwanza, kuwa na kitengo cha watu hali mahututi katika kila hospitali ya eneo la Bunge ni njia moja ya kuokoa maisha ya watu wetu. Nikipeana mfano kwa sehemu ambayo nimetoka kule Turkana, tunasafiri kilomita 800 hadi mji wa Eldoret kuleta mtu ambaye amepata ajali na ni gharama. Ugatuzi nikupeleka huduma karibu na wananchi. Tukiwa na kitengo cha hali mahututi na cha kutoa damu kwa kila eneo la Bunge ni njia moja ya kupeleka huduma karibu na watu ili watu wapate huduma kwa njia iliyo rahisi kuliko tu kusafirisha watu kutoka maeneo mbalimbali hadi ...
view