24 Jun 2015 in National Assembly:
Watu wa Kenya ni wafadhili wazuri. Katika nchi yetu ya Kenya tumebarikiwa na watu walio na mioyo safi. Kuna watu ambao wangependa kutoa damu ili kusaidia wenzao lakini shida ni sehemu ya kwenda kutoa damu hiyo. Kwa mfano, katika kaunti ya Turkana, kuna watu wangependa kuchangia damu lakini mahali pa kuelekeza hao wafadhili ambao wangependa kutoa damu yao ni shida. Kwa hivyo, tukiwa na kitengo kama hiki cha kutoa damu katika kila eneo la Bunge itarahisisha wafadhili ambao wangependa kutoa damu yao kuokoa maisha ya wengine na kupeana kwa haraka. Hii ni muhimu kwa sababu hata kama wewe ni mfadhili, ...
view
24 Jun 2015 in National Assembly:
Ajali nyingi siku hizi zinatendeka kwa sababu ya mambo ya boda boda . Sehemu nyingi ambazo tumetoka utakuta kwamba mtu akipata ajali, kwa mfano akiumia goti ama kichwa lazima asafirishwe kutoka Lodwar hadi Eldoret ama Nairobi. Tukiwa na kitengo kama hiki cha watu mahututi kwa kila eneo la Bunge ni rahisi kupeleka huyu mtu mahali pale. Lazima tuhakikishe ya kwamba kwa wakati kama huu ambao vijana wetu wengi wanapata riziki yao kwa
view
24 Jun 2015 in National Assembly:
wakati jambo lolote limetokea katika maisha yao, tuko tayari kuwasaidia bila gharama kubwa kwa maana wengine wao wanategemea hiyo boda boda kujipatia riziki ya kila siku na wengine wameajiriwa. Hata hizo boda boda siyo zao lakini wanapopata ajali, gharama ya kusafirisha huyo mtu mpaka mahali pa kupata matibabu ni kubwa. Unapata kama ameumia mguu inabidi ukatwe na anakuwa kiwete katika maisha yake.
view
24 Jun 2015 in National Assembly:
Kuhusu jambo ambalo Mheshimiwa amesema kwamba tuwe katika kila eneo, msongamano mwingi uko katika hospitali ya kaunti kwa sababu ni moja tu. Watu wanasafirishwa kutoka sehemu zote za eneo la Bunge na wanapelekwa katika hospitali moja. Hapo unakuta msongamano katika hospitali hiyo na watu wengine wanapoteza maisha yao kabla hata hawajafikia daktari. Tukiwa na kitengo cha hali ya mahututi katika kila eneo itakuwa rahisi mtu kupata huduma kwa haraka. Kama vile Mheshimiwa Abdul amesema, hospitali zingine za kaunti hazina vitanda. Utakuta wagonjwa wawili ama watatu wakilala katika kitanda kimoja. Kwa mfano, tuliona hospitali za Chuka na Isiolo ambazo ziko katika ...
view
24 Jun 2015 in National Assembly:
Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda, ningependa pia kushukuru Mheshimiwa Abdul kwa kusema kwamba tunapokuwa na kitengo hicho akina mama wajawazito nao wawe na sehemu The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor.
view
24 Jun 2015 in National Assembly:
maalum ya kujifungua. Utashangaa kusikia kwamba hospitali zingine hazina sehemu maalum ya kujifungua. Wajawazito wanajifungua katika nyumba ya kawaida ambayo haina malazi mazuri hata sakafu haijatengenezwa. Jambo hili linavunja moyo! Watoto wanazaliwa katika hali iliyo mbaya na hata wanaweza kupata ugonjwa. Kila hospitali iwe na sehemu safi na tena iwekwe vitu ambavyo ni vya kisasa na mazingira yawe ya kupendeza.
view
24 Jun 2015 in National Assembly:
Ningependa kumalizia kwa kusema ya kwamba katika hizo hospitali pia ni lazima tuwe na wauguzi maana bila wafanyikazi ambao wamehitimu itakuwa vigumu kuhudumia wagonjwa. Kwa mfano, kuna mambo yalitokea katika hospitali moja. Mwanafunzi aliyemsaidia mama kujifungua aliosha mtoto na maji moto na yakamchoma. Ningependa pia Mheshimiwa Abdul ahakikishe ya kwamba tutakapokuwa na hivi vitengo katika kila eneo la Bunge, pia tutakuwa na wauguzi na madaktari wazuri ambao wamehitimu vizuri ili wasaidie katika kupeana huduma hii.
view
24 Jun 2015 in National Assembly:
Mwisho, jambo la kuhuzunisha ni kwamba utapata kwamba madaktari ambao wamehitimu na wamekuwa katika chuo kikuu, wanapopelekwa katika kaunti zingine kufanya kazi, wanakataliwa. Hakuna njia tunaweza kuondoa ukabila katika nchi hii na kuwa na utengamano kama tunafukuza madaktari ambao wamehitimu. Tusihukumu mtu kwa sababu ya ukabila ama eneo. Tuongee kuhusu jambo hili pia kwa sababu kuna sehemu ambazo hawana watu ambao wamehitimu katika njia kama hizo. Lazima tukubali hawa watu wapelekwe katika sehemu hiyo wafanye kazi kama wahitimu ambao wamemaliza masomo yao kwa njia nzuri. Kwa hivyo, ningependa kukashifu kaunti ambazo zinafukuza wafanyikazi ambao wametumwa mahali pale na Serikali.
view
24 Jun 2015 in National Assembly:
Kwa hayo machache, Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda, napenda kuunga mkono Hoja hili. Asante sana.
view
23 Jun 2015 in National Assembly:
Hon. Temporary Deputy Chairman, we need to take care of the transition. When the Auditor-General is not there, what next? This is very important.
view