Johnes Mwashushe Mwaruma

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 241 to 250 of 984.

  • 21 Jun 2023 in Senate: The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard Services,Senate. view
  • 21 Jun 2023 in Senate: Wachache na ambaye pia ni Seneta wa Kitui, Sen. Wambua. Huu Mswada ulikuwa katika Seneti iliyopita, ukaenda katika Bunge la Kitaifa lakini ukaishia hapo. Bw. Spika wa Muda, ningependa kumshukuru Sen. Wambua kwa kuuleta tena Mswada huu kwa Bunge hili la kumi na tatu. Mmea wa ndengu ni mmea muhimu na vile alivyosema, huu mmea unakuzwa katika kaunti alizozitaja za Kitui, Makueni, Taita Taveta na zinginezo. Mara ya kwanza kusikia kuhusu mmea huu, nilikuwa mdogo sana. Nilikuwa kijana mdogo; mtoto mdogo na tulikuwa tunapenda kitoweo cha ndengu, haswa ikipikwa na chapati. Zamani, watoto walikuwa wanapenda sana chapati na kitoweo chetu ... view
  • 21 Jun 2023 in Senate: The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard Services,Senate. view
  • 21 Jun 2023 in Senate: Inabidi sasa kama utahifadhi kwa gunia bila kuweka dawa, ama magunia maalum, ile ndengu nyingi inaliwa na wadudu. Kwa hivyo, hasara huwa ni nyingi sana. Changamoto nyingine ni kwamba mmea huu unakua kwetu lakini wakulima wengi hawavuni kwa sababu kule kwetu ni maeneo kame; ni maeneo ambayo yamepakana na wanyama pori. Maeneo ya Kasiyau, Marungu, Kushushe, Mbololo, Bura, Mwakitau ni maeneo yote yanayokuza mmea huu wa ndengu, lakini kwa sababu wanyama pori hawajadhibitiwa kuwa mbugani, wanavuka mpaka wanakuja mahali wananchi wanaishi. Basi watu wengi pia hawavuni. Kwa hivyo, ni changamoto inayokumba huu mmea na mimea mingine kama mahindi na kadhalika ... view
  • 21 Jun 2023 in Senate: Malengo ya huu Mswada yamekuwa ni kutoa mwelekeo ama kuweka sera na sheria zinazopeana mwelekeo wa kutekeleza ukuzaji wa huu mmea wa ndengu katika Kaunti zetu na Serikali la kitaifa, kwa sababu mimea mingi ambayo imetambulika kama mimea ya pesa ama kwa lugha ya Kimombo, cash crops, ni kama mahindi, majani chai, kahawa na kadhalika. Tayari, kuna sheria kuhusiana nazo ingawaje zimekuwa za zamani na zinahitaji marekebisho. Hatujakuwa na sheria zozote ama sera zinazotambua huu mmea kuwa mmea wa pesa ama cash crop . Kwa hivyo, huu Mswada ni muhimu na unalenga kutimiza lengo hilo. La pili pia ni kwamba, ... view
  • 21 Jun 2023 in Senate: Bw. Spika, kuna kitu ambacho kwa Kizungu wanasema Gross Domestic Product view
  • 21 Jun 2023 in Senate: Tukikuza mimea na tupate faida zaidi, itakuwa ni manufaa kwa mkulima hapa nchini. Lengo lingine ni mbinu ya kutafuta soko la ndengu. Haiwezi kuwa wananchi view
  • 21 Jun 2023 in Senate: The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard Services,Senate. view
  • 21 Jun 2023 in Senate: wanapanda kwa bidii, halafu Serikali haiwasaidii kutafuta soko. Mmea huu unaharibikia manyumbani na wakati mwingine mashambani. Tukiangazia mahindi, tayari Serikali imeweka mikakati kadhaa. Ni kwa sababu ni mmea unaotambulika kama mmea wa pesa ama cash crop . Kwa mfano, wakati wakuzaji mahindi wa kaskazini mwa Bonde la Ufa wanapotoa mahindi, wakati mwingine, Serikali inanunua hayo mahindi na kuuzia wasagaji mahindi baadaye. Hii sheria inapelekea kuwe na sera kama hizo ambazo zitapelekea Serikali ya kitaifa na za kaunti kununua hii nafaka na kuhifadhi katika maghala ya kitaifa. Wakati wa njaa, tutakuwa na ndengu ya kutosha kuuzia wananchi. Tukitengeneza hii sheria, sera ... view
  • 21 Jun 2023 in Senate: Vilevile, wakulima wengine wanaopatiwa cushion kwamba wakilima lazima watapata zile pesa kidogo walizotumia, basi katika kutengeneza sera na sheria za huu mmea, ni vizuri kuwe na kanuni kama hizo. Kuna soko kubwa katika shule zetu. Mara ya kwanza kusikia kuhusu ndengu ilikuwa nikiwa kijana mdogo. Nilikua na binamu yangu ambaye alikua anasoma Shule ya Upili ya Wavulana ya Alliance, ambako walikua wanapikiwa ndengu. Tuko na jina la ndengu kwa Kitaita. Kwa hivyo, shule nyingi hupika ndengu. Serikali ikinunua hii ndengu, inaweza kupeana kwa mashule kupitia kwa School view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus