Johnes Mwashushe Mwaruma

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 251 to 260 of 984.

  • 21 Jun 2023 in Senate: Niliona gavana wa Kaunti ya Jiji la Nairobi, ambaye tulikua na yeye kwenye Kamati ya Leba na Ustawi wa Jamii, jana akizindua mpango wa chakula kwa shule zote. Mpango huu ukiingia kwa shule zote nchini, ndengu itapata soko, kisha wananchi wetu watanufaika kutokana na kilimo cha ndengu. view
  • 21 Jun 2023 in Senate: Bw. Spika, naona muda wangu unaisha. Kuna mamlaka au Authority ambayo imebuniwa ili kudhibiti ama kuendeleza ukuzaji wa ndengu. Hoja hii imeeleza sifa za watu wanaofaa kuwa katika mamlaka haya, pamoja na kazi ambayo watafanya. Hivyo basi, sitarudia. Hata hivyo, kuwepo kwa mamlaka utakuwa mpango mzuri utakaoshirikisha serikali za kaunti kwa sababu kilimo kimegatuliwa; na Serikali ya Kitaifa kwa sababu sera hutengenezwa na Waziri wa kitaifa. view
  • 21 Jun 2023 in Senate: La muhimu zaidi, huu Mswada unaeleza zaidi kuhusu jinsi Waziri wa Kilimo katika kaunti atahusishwa ili kuhakikisha sera na sheria zilizotungwa katika kaunti na hata ngazi ya kitaifa zimetekelezwa. Kwa mfano, huu Mswada unasema kila mkulima lazima ajisajili. Umuhimu wa kujisajili ni kwamba Serikali itajua idadi ya wakulima wa ndengu na ekari za ndengu. Kwa hivyo, wakati wa kutoa pembejeo ama mbegu, basi Serikali itaweza kufanya bajeti ili kutayarisha mbegu inayohitajika na mbolea ya ruzuku. Kumbuka changamoto moja ni kwamba hakuna mbegu wakati zinapohitajika. Pembejeo na mbolea zitakapokuja, Serikali itawasiliana na wakulima waliojisajili, kwa sababu itakuwa inajua waliko hawa wakulima ... view
  • 21 Jun 2023 in Senate: Jambo lingine ni ugonjwa ambapo mkulima fulani akivamiwa na ugonjwa fulani, kutakua na mbinu ya mawasiliano ili kuokoa zao la mkulima. Tukijua wakulima wamepewa pembejeo na mbolea kiasi fulani, basi katika wakati wa mavuno tutatarajia mavuno kiasi fulani. view
  • 21 Jun 2023 in Senate: The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard Services,Senate. view
  • 21 Jun 2023 in Senate: Bw. Spika wa Muda, ukiwa na data ama takwimu, wakati wa kutayarisha soko, takwimu zitakuelekeza kwa soko la COMESA ama kwingineko. Takwimu zitaonyesha kiasi cha zao ambalo linatarajiwa Taita Taveta au Makueni, kwa maana mvua ilinyesha vizuri na kadhalika. Kwa hivyo, katika kupanga, tunahitaji takwimu. Tutapata hizi takwimu kwa mawaziri wa kilimo katika serikali za kaunti wamehusishwa kikamilifu. view
  • 21 Jun 2023 in Senate: Bw. Spika, wakulima wa ndengu pia wanahitaji mafunzo kuhusu mbinu za kisasa za kulima. Hayo mafunzo yatafanywa na hayo mamlaka ama Authority . Mamlaka hayo pia yataangazia utafiti ili kubaini mbegu itakayofaa zaidi kwa mchanga wa eneo fulani. view
  • 21 Jun 2023 in Senate: Mhe. Spika wa Muda, kwa sababu naona muda umenipa kisogo, ningependa kusema kwamba tuangazie huu Mswada. Pia, tuangalie vile tutashirikiana na wenzetu wa Bunge la Kitaifa ili Mswada huu usije ukafa vile--- view
  • 21 Jun 2023 in Senate: Bw. Spika wa Muda, kwa hayo mengi au machache, ninaunga mkono Mswada huu. view
  • 21 Jun 2023 in Senate: Asante. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus