20 Jun 2023 in Senate:
Asante, Bi. Spika wa Muda, kwa kunipa hii fursa ili kuchangia Mswada huu. Kwanza nashukuru Seneta Mteule aliyeleta huu Mswada, Sen. Mutinda. Mswada huu unahusu wahudumu wa kilimo. Si mara ya kwanza tumekuwa na wahudumu wa kilimo. Wamekuwa tangu zamani nikiwa mtoto mdogo. Tulikuwa na Serikali ya kitaifa, walikuwa wakisaidia sana wakulima wetu. Ile kazi walifanya ilikuwa kazi kubwa sana. Afisa hao walisaidia kuendeleza kilimo katika jamii. Hiyo huduma ilififia na kwa saa hizi haieleweki vizuri kama hawa wahudumu wa kilimo bado wako ama hawako.
view
20 Jun 2023 in Senate:
The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard Services,Senate.
view
20 Jun 2023 in Senate:
Ninakumbuka kuna wakati nilikuwa mkulima miaka 20 iliyopita. Nilipanda nyanya nyingi sana kama ekari tatu. Ilikuwa ni nyingi kulingana na mimi nikiwa kijana mdogo. Nilitafuta mhudumu wa kilimo na ilichukua siku mbili yeye kuja sababu nyanya zangu zilikua zimepata ugonjwa siuelewi, uliokuwa kama blight. Bi. Spika wa Muda, alipokuja baada ya siku tatu, nilipoteza nyanya nyingi ilhali makisio yangu nilikua nipate kama tani tano. Huyo mhudumu alikua mgonjwa na alikua mmoja na kwa kuchelewa kwake, nilivuna nusu tani peke yake. Lazima niseme hawa wahudumu ni wa muhimu sana. Nashukuru Sen. Mutinda kwa kuona kwamba ni vyema aweke mswada ambao unaleta ...
view
20 Jun 2023 in Senate:
ambayo itakua ni kama body corporate au shirika linaloweza kushtakiwa na kuangazia mbinu za kukuza kilimo. Mswada huu umeelezea sifa au qualifications za hawa wahudumu katika hii huduma. Bi. Spika wa Muda, naunga mkono huu Mswada kwa sababu kilimo ndicho uti wa mgongo haswa kwa nchi kama Kenya. Kama kutakua na viwanda, vitakua agri-based ; viwanda kutokana na ukulima. Kwa mfano, tukiangalia Kaunti kama Makueni, wameweza mambo ya ukulima na sasa hivi kuna kiwanda cha maembe kiko kule Makueni, na kwa sababu hio, Kaunti ndiyo inazalisha maembe kwa wingi.
view
20 Jun 2023 in Senate:
The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard Services,Senate.
view
20 Jun 2023 in Senate:
Ninakubaliana na wasemaji wengine ya kwamba zamani tukiwa wadogo, kulikua na shule za kufunza wakulima au Farmers Training Centres. Saa hizi nyingi zimetelekezwa, zikaachwa na haziendelei. Labda hio bodi ya National and CountyExtension Service inatakiwa iangazie kuwa na zile shule mashinani ili kuhakikisha ya kwamba wakulima wetu wanafunzwa mbinu totafuti tofauti za ukulima. Bi. Spika wa Muda, nakuabaliana na huu Mswada sababu kilimo kimegatuliwa na kuna huduma fulani zinatakikana zifanyike Serikali ya kitaifa. Kwa mfano, Waziri wa Serikali ya kitaifa anatakikana kuandika sera na sheria za kuangazia ama kuhakikisha hii huduma kwa wakulima iko sawa kwa kaunti zote 47. Je, ...
view
20 Jun 2023 in Senate:
Bi. Spika wa Muda, huu ni Mswada mzuri na ningeomba tuunge mkono. Tukitaka nchi hii ifike katika kiwango kingine, kilimo lazima kistawishwe. Kwa hayo machache, naunga huu Mswada. Asante.
view
15 Jun 2023 in Senate:
Asante, Bw. Spika, kwa kunipa hii fursa ya kuchangia Mjadala huu wa kumwondoa mamlakani naibu wa Gavana wa Kaunti ya Siaya. Ninakubaliana na Senate Business Committee (SBC), kuwa tuende njia ya Kamati. Njia hii inahusisha watu wachache na wanapata fursa ya kuangalia yale mashtaka kwa undani. Nilikuwa na fursa ya kumwondoa maamlakani Gavana wa Kaunti ya Meru na ninakubaliana mia kwa mia, kwamba hii ndio njia mzuri zaidi. Nilitarajia kuwa kati ya wale Maseneta waliowekwa katika Kamati hii, kungekuwa na mmoja ambaye angalau alikuwa katika ile Kamati nyingine kwa sababu ya kumbukumbu ya taasisi. Kwa sababu hamna yeyote, basi maafisa, ...
view
15 Jun 2023 in Senate:
The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view
15 Jun 2023 in Senate:
kuangalia hili swala la kuondolewa mamlakani, umependekeza kwamba muda uwe mrefu zaidi, labda siku 15 badala ya 10. Asante.
view