Johnes Mwashushe Mwaruma

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 271 to 280 of 984.

  • 8 Jun 2023 in Senate: Asante, Bi. Spika wa Muda, kwa fursa hii umenipa ili nichangie Mswada wa County Allocation of Revenue Bill (CARB) ambao ni muhimu kwenye Bunge hili la Seneti. Mwaka wa 2010 kama Wakenya tulijipa Katiba mpya ambayo ilileta mfumo wa uongozi kwa ngazi mbili -- ngazi ya Kitaifa ama National Government na ngazi za kaunti ama magatuzi. view
  • 8 Jun 2023 in Senate: Katiba mpya ilipopita, kulibuniwa Consolidated Fund ama hazina ya kitaifa. Tume ambayo inahusika katika kugawanya hizi pesa mara mbili kwa serikali ya Kitaifa na serikali za kaunti ni CRA. Tume hii ikipitisha mfumo wa ugavi wa pesa kwa serikali ya Kitaifa na kaunti kwa sheria inayoitwa Division of Revenue Act (DORA), Wakenya walisema kwamba ni vizuri kuwa na wawakilishi ama wabunge wa Bunge la Kitaifa na Bunge la Seneti ili kupiga msasa sheria ile. Wiki kadhaa zimepita tangu kupitisha DORB. Baada ya kugawanya pesa mara mbili, pesa za kwenda kwa magatuzi inagawanywa mara 47, kwa sababu magatuzi ni 47. view
  • 8 Jun 2023 in Senate: Sheria inayotumika kugawanya raslmali ya kitaifa mara 47 ni CARB ambayo tunajadili leo. Sheria hii kupita kwenye bunge la Seneti inahitaji formula ama mfumo wa kugawanya pesa. view
  • 8 Jun 2023 in Senate: Mwaka wa 2020 kulikuwa na patashika, vuta nikuvute kati ya Maseneta na view
  • 8 Jun 2023 in Senate: kwa sababu ya ule mfumo uliopendekezwa. Kaunti zingine zilikuwa zinapoteza pesa. Tuling’ang’ana na kukubaliana kwamba tutumie formula ama mfumo wa pili wa kugawanya pesa. Hii leo katika hii sheria DORB, Ksh385.4 bilioni imependekezwa kuenda kwa magatuzi. Kati ya hizi pesa, asilimia 14.5 ama Ksh35.9 billion zimeenda kwa countyassemblies. Bi. Spika wa muda, bila kuongea sana kuhusu undani wa CARB, ningependa kusema kwamba magatuzi ni mfumo wa serikali ambao ni mpya. Mfumo huu umekuwa kwa muda wa miaka 13 lakini umekumbwa na changamoto si haba. Nafikiri katika kuongea kwangu na kuchangia huu Mswada, ni vyema niangalie zile changamoto ambazo zimekumba serikali ... view
  • 8 Jun 2023 in Senate: Changamoto ni nyingi na ya kwanza ambayo inafanya ugatuzi usinawiri ni kucheleweshwa kwa kutolewa kwa mgao kwa magatuzi. Hivi sasa, serikali za magatuzi zinadai pesa nyingi za mwaka wa kifedha 2022/2023 ambao unaisha mwezi huu. Hata hizi pesa zikiachiliwa na Hazina ya Kitaifa, bado hakutakuwa na muda wa magavana kuzitumia. Kucheleweshwa kwa mgao kwa magatuzi kunapelekea kuwa na huduma duni. Kwa mfano, hospitali hazina madawa na vifaa vya kutibu. Wafanyikazi, madaktari na walimu hawajalipwa. Hivyo basi, huduma zitakuwa duni kwa sababu wafanyikazi hawana motisha. Kama daktari huwezi kufanya kazi ukiwa na motisha ikiwa haujalipwa mshahara. Motisha umekuwa chini kwa wengi. ... view
  • 8 Jun 2023 in Senate: The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view
  • 8 Jun 2023 in Senate: sheria. Sheria imesema asilimia 35 ya zile pesa zinazoenda kwa magatuzi itumike kwa uajiri lakini kaunti nyingi zimeajiri watu kupita kiasi. Wengine wametumia asilimia 40 na 50. Kwa mfano, Kaunti yangu ya Taita Taveta, tuko kwa asilimia 52 ya ule mgao unaenda kwa kaunti yetu. Kama tunahitaji kufanya maendeleo na kile kiwango kilichowekwa ni asilimia 35, tukilipa zaidi, zile pesa zinazobaki za operation s inakuwa kama asilimia 10 peke yake. Ni vizuri kama Seneti tuhimize kaunti zetu na tuwalazimishe kufuata sheria za kuajiri. La sivyo, pesa zote zinazoenda kwa kaunti zitatumika kuajiri na maendeleo yatakuwa duni. La tatu ni ufisadi ... view
  • 8 Jun 2023 in Senate: The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view
  • 8 Jun 2023 in Senate: na wizi unaendelea kwa kaunti zetu na Wawakilishi Wadi hawaongei. Kwa hivyo, hilo ni swala lingine ambalo limepelekea ugatuzi kutonawiri. Swala lingine ambalo tumeliongelea katika Bunge hili ni mfufumko wa bei. Seneta wa Siaya aliangazia hili jambo. Alisema zile pesa zinazotumwa kwa magatuzi hazilingani na mfufumko wa bei kulingana na vile gharama ya maisha imepanda. Ukiangalia kwa ile sheria ya Division of Revenue Allocation Bill (DORB) tuliyopata mapendekezo kutoka kwa County Revenue Allocation (CRA), ilisemekana mfufumko wa bei ilikuwa asilimia nane. Ilitakikana pesa za kwenda kwa kaunti ziwe Ks407 bilioni ili kuangazia mfufumko wa bei lakini tumepeleka Ksh385 bilioni. Kwa ... view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus