11 May 2021 in Senate:
Mwananchi wangu wa Taita-Taveta alitoa mawazo mengi sana kuchangia kwa Mswada huu lakini mengi hayajazingatiwa ama kuangaziwa. Jambo la kwanza ni kwamba asilimia 62 ya Gatuzi la Taita-Taveta iko chini ya mbuga za wanyama. Katika mapendekezo ya Mtaita na Mtaveta, tulisema kwamba ile mbuga ya wanyama iwe gamereserve badala ya kuwa national park ili mwananchi wa Taita-Taveta afaidike moja kwa
view
11 May 2021 in Senate:
The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view
11 May 2021 in Senate:
moja kutokana na rasilmali ya mbuga za wanyama. Hilo halijawekwa katika Mswada huu. Kwa hivyo, mwananchi wa Taita-Taveta ninayemwakilisha hana furaha.
view
11 May 2021 in Senate:
Mbuga ya Wanyama ya Masaai Mara iliyoko katika Eneo Mbunge la Narok inafaidi wananchi kutokana na pesa nyingi tunayoita own source revenue . Kinyume ni kwamba kwetu hatupati faida hata kidogo bali maafa. Ninapoongea sasa hivi, kuna mtu atakayezikwa leo katika maeneo ya Bughuta katika Eneo Bunge la Voi. Mtu huyo aliuawa juzi na ndovu aliyemfuata mpaka shambani kwake. Mimea inaliwa na wanyama pori lakini kupata fidia imekuwa ngumu. Wakulima wale pia hawana pesa za kuweka uzio za umeme pia ni ngumu. Sehemu hizo zingetambulika kama sehemu maalum ya hifadhi ya wanyama pori au game reserves, tungeweza kujitengenezea uzio za ...
view
11 May 2021 in Senate:
The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view
11 May 2021 in Senate:
Kenya Urban Roads Authority (KURA) na Kenya Rural Roads Authority (KeRRA) yanaweza kuendea serikali za ugatuzi kwani barabara zinazoshughulikiwa na mashirika hayo zote ziko katika serikali za ugatuzi. Pesa zinazoendea mashirika hayo na mengine mengi yanafaa kuendea serikali za ugatuzi ili mchango wa pesa iongezeke mpaka asili mia 35.
view
11 May 2021 in Senate:
Bw. Spika, pesa zinazoendea Wizara za Kilimo, Afya na Michezo pia zinafaaa kuendea serikali za ugatuzi kwani hayo ni mambo yanayoshughulikiwa na serikali hizo. Kwa mfano, Wizara ya Michezo ina pesa nyingi mpaka wanalazimika kupatia serikali za ugatuzi misaada ya kujenga viwanja vya michezo. Kwa nini pesa hizo zisipewe serikali za ugatuzi ili zifanyiwe bajeti na serikali hizo? Kwa nini pesa zinazobaki katika Wizara ya Kilimo zisiendee serikali za ugatuzi ilhali maswala ya ukulima zinashughulikiwa na serikali za ugatuzi?
view
11 May 2021 in Senate:
Swala la ugatuzi ni swala nzito sana kwangu kama Seneta wa Kaunti ya Taita- Taveta. Wananchi wetu wanfaidika sana na maendeleo kutokana na ugatuzi. Kaunti ya Taita-Taveta ni moja wapo ya kaunti ndogo nchini na wengi wanaopinga ugatuzi uuliza inakura ngapi? Kwa kweli, kura zetu ni chache sana. Sisi mfumo huu wa ugatuzi ni baraka kubwa sana kwetu. Tangu kuanzishwa kwa mfumo wa ugatuzi, Kaunti ya Taita- Taveta imepokea zaidi ya Kshs4.5 bilioni za maendeleo kila mwaka. Kabla ya mfumo wa ugatuzi, haikuwa inapata kiwango hicho cha pesa. Tunapata pesa nyingi sana za maendeleo katika mfumo huu wa ugatuzi.
view
11 May 2021 in Senate:
Kuanzia mwaka 2013, mfumo wa ugatuzi ulipoanza, hakuna mradi umefanywa katika Kaunti ya Taita-Taveta kutokana na pesa za Serikali ya Kitaifa unaozidi Kshs200 milioni. Pesa zaidi tulipata kwa mradi mmoja haukuzidi Kshs50 milioni. Hata hivyo, mwaka huu, Kaunti ya Taita-Taveta ilipata msaada kutoka kwa Benki ya Dunia wa Kshs900 milioni ya mradi wa maji. Mwaka wa 2018, niliuliza swali hapa Bungeni nikitaka Wizara ya Maji itueleze miradi yote nchini katika wizara hiyo. Ripoti hiyo ilipoletwa hapa Bungeni, nilishangaa kuona Kaunti ya Embu ilipata kiasi cha Kshs2.5 bilioni za miradi ya maji kuanzia 2013 hadi 2018. Kaunti ya Murang’a ilipata kiasi ...
view
11 May 2021 in Senate:
Bw. Spika, jambo lingine linalonihimiza niunge mkono Mswada huu wa BBI ni kwamba linapendekeza pesa za CDF katika katiba. Nilitangulia kusema kwamba Kaunti ya Taita-Taveta ina maeneo mbunge manne na kila eneo bunge linapata zaidi ya Kshs130 milioni kila mwaka. Pesa za CDF sikitambulika kikatiba, tunahuakika kwamba hautawahi kupoteza pesa hizo za CDF zinazosaidia wananchi wengi kugharamia karo za shule, kujenga mashule na kutimiza mandeleo mengine mengi yanayo husika na elimu vile usalama.
view