11 May 2021 in Senate:
Kutambulika kwa CDF kikatiba kunamaanisha kwamba Kaunti ya Taita-Taveta haitawahi kukosa pesa hizo. Kuna watu walipeleka kesi kortini wakitaka pesa za CDF
view
11 May 2021 in Senate:
The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view
11 May 2021 in Senate:
zitupiliwe mbali bila wao kutambua kwamba mfumo wa ugatuzi na pesa za CDF zimeleta maendeleo mengi katika serikali za ugatuzi. Sisi tunashangilia pesa CDF kutambulika kikatiba.
view
11 May 2021 in Senate:
Bw. Spika, mfuko wa kuendeleza kata au Ward Development Fund pia unahakikisha kwamba pesa za maendeleo zitafikia kila kata. Pesa hizo zinawakilisha kwamba kila kata inapata pesa za maendeleo hata kama mwakilishi wa kata hiyo hamuungi mkono gavana wa kaunti hiyo. Ninamshukuru Sen. Kang’ata aliyeleta Mswada wa County Wards Development Equalisation Fund Bill, 2018 katika Bunge hili. Isipokuwa Mswada huo haukupita, ninafuraha kwamba Mswada huu wa BBI unapendekeza kutambua pesa hizo kikatiba. Namsihi Sen. Kang’ata wa Murang’a aunge Mswada huu mkono kwani unazingatia maswala ambayo amekuwa akipigania hapa Bungeni.
view
11 May 2021 in Senate:
Jambo lingine nzuri katika Mswada huu wa BBI ni kwamba kunahakikisho kwamba kutakuwa na usawa wa kijinsia. Mimi ni mwanaharakati wa usawa wa kijinsia. Nina furaha kwamba Mswada huu wa BBI ukipita, Bunge zetu zote zitakuwa na usawa wa jinsia. Mwaka uliopita, mahakama ilisema ya kwamba Bunge livunjiliwe mbali kwa sababu lilikuwa limeshindwa kupitisha sheria ambayo ingehakikisha usawa wa jinsia katika Bunge. Ilikuwa hata tungelivunja Bunge, watu wanaochagua ni walewale wanacnhi wetu. Hawachagui wakizingatia usawa. Building Brides Iniatieve inasema hatuwezi kuwa tunaendelea huku tumeacha wananchi wengi ama nusu yao nyuma ambao ni wanawake, walemavu na vijana.
view
11 May 2021 in Senate:
Pia, ninaunga Mswada huu mkono kwa sababu Mawaziri watakuwa hapa Bungeni. Mara kwa mara tumeuliza mwaswali yanayohusiana na wananchi wetu yajibiwe lakini tumepata shida kupata Mawaziri. Wengine hawataki kuja Bungeni kujibu maswali. Tukiwa na Waziri Mkuu ama Mawaziri Bungeni, itakuwa rahisi kupata majibu kwa maswali tunayouliza Bungeni.
view
11 May 2021 in Senate:
Yale masuala ambayo labda hayako vizuri katika serikali yetu wakati huu ni kwamba ugatuzi ni jambo nzuri lakini kutoa pesa kuzipeleka kwa kaunti ili zifanye maendeleo kumekuwa kizungumkuti. Nina imani kwamba tukiwa na uongozi mzuri unaoangalia mambo ya fedha na kumaliza ufisadi, tutakusanya fedha za kutosha na kwa wakati unaofaa ili ziende katika kaunti kufanya maendeleo. Mambo ya ufisadi yanaua maendeleo katika nchi yetu tukufu ya Kenya. Leo tunaambiwa kuwa billioni mbili fedha za Kenya zinapotea kila siku. Tukifunga huo mfereji wa ufisadi, basi zile pesa za kwenda kufanya maendeo mashinani zitapatikana na tutazidi kudumisha ugatuzi. Mambo wakati huu yamekuwa ...
view
11 May 2021 in Senate:
The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view
11 May 2021 in Senate:
lini? Hatujui. Hatujui kama litakuwa kama mafua au kohozi ambalo tunaendelea nalo milele na milele. Mambo ya kusema tusibadilishe Katiba kwa sababu kuna Korona hayana umuhimu wowote kwa sababu hatujui kama janga hili litaenda mpaka lini. Mambo ya kukopa sana ili kufanya maendeleo yanatufisha moyo sana hapa Kenya. Kabla ya mwaka wa 2012 tuliweza kumudu asilimia 95 ya bajeti yetu. Mwaka wa 2012 asilimia 95 ya bajeti ya Kenya ilichangiwa na fedha zilizotoka Kenya kwenyewe. La kuvunja moyo sasa ni kwamba bajeti yetu ni Kshs3 trillioni katika nchi inayokusanya chini ya Kshs2 trillioni. Jambo hili linaonyesha kuwa katika mwaka wa ...
view
11 May 2021 in Senate:
The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view