7 Jul 2015 in Senate:
Bw. Spika, nimesikiza taarifa iliyotolewa na Naibu Mwenyekiti. Ningependa kumjulisha na kumkosoa kwamba shida ambayo inakabili Kaunti ya Kitui inahusu makabila mawili; Wasomali na Wakamba. Ni dhahiri kwamba hatua zilizochukuliwa zinatenganisha makabila haya mawili. Ikiwa watu wa Kitui watachukua hatua, itaelekezwa kwa Wasomali kisha itakuwa vita vya kikabila. Inafaa Naibu Mwenyekiti afahamu kwamba chochote kitakachotokea ni vita vya makabila. Ikiwa vitaanzia Kitui, vitaenea taifa nzima. Kwa nini Serikali haichukui hatua madhubuti kuhakikisha kwamba matendo haya yanasimamishwa haraka iwezekanavyo?
view
7 Jul 2015 in Senate:
Bw. Spika wa Muda, ni matumaini yangu kwamba mhe. Rais wa taifa hili atapokea ujumbe tunaotuma kwa sasa. Serikali ya Jubilee ina jukumu la kulinda maisha ya Wakenya. Tangu Jubilee iingie mamlakani, tumeshuhudia maafa ya Wakenya ambao hawana hatia. Juzi Wakenya walishuhudia mhe. Rais katika mkutano wa kumaliza pombe haramu akinyosha kidole na kusema: “Wewe fulani ninakuagiza hivi sasa ufanye msako mkali kabisa.” Anayeambiwa mambo hayo, juu yake kuna Mkuu wa Polisi. Mhe. Rais mwenyewe anaruka kitengo cha uongozi na kupeana amri kwa askari wa mamlaka ya chini ambaye anasimamiwa na Mkuu wa Polisi. Ni Mkuu wa Polisi ambaye anasatahili ...
view
7 Jul 2015 in Senate:
Bw. Spika wa Muda ukienda katika kila choo jijini Nairobi kuna maandishi ukutani kuwa Bi. Anne Waiguru ameiba Kshs826 milioni kupitia kwa The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate.
view
7 Jul 2015 in Senate:
Bw. Spika wa Muda, mambo yanayotokea katika nchi yetu ni mambo ya kuudhi sana. Wananchi wakiwa wanauwawa bila hatia ilhali Serikali ya Jubilee inapanga kutumia pesa ambazo hazijapitishwa na Bunge kujenga ukuta mipakani wa Kenya na Somalia. Vijana wetu hawana kazi, watu wanauwawa lakini wanataka kujenga ukuta huku wakipora pesa. Wananchi Wakenya tunasema kwamba serikali yoyote ambayo haiwezi kulinda maisha ya wananchi wake haistahili kuwa katika uongozi. Hivi sasa tunaongea kwa majonzi. Mtu yeyote ambaye anasimama hapa na kupinga mambo haya, hata yeye ni muuaji. Hii ni kwa sababu hakuna mtu ambaye atapinga mauaji yakizungumziwa na kuleta siasa za sera ...
view
7 Jul 2015 in Senate:
Bw. Spika wa Muda, kupinga sio kutokubaliana na wengine, bali tunapozungumza juu ya vile pesa za umma zinatumiwa na mtu anasimama na kusema kwamba haitumiki namna hiyo. Hiyo inaonyesha kwamba yeye anapinga Hoja hii. Ninaunga mkono.
view
2 Jul 2015 in Senate:
On a point of order, Mr. Deputy Speaker, Sir. This is just a rider. The statement being sought by Sen. Bule is very important. In fact, it has issues in all counties. I would like Machakos County to be considered along the same aspect when a statement is issued.
view
2 Jul 2015 in Senate:
Bw. Spika wa Muda, ninashukuru sana kwa nafasi hii ili nichangie Hoja hii ambayo ni ya maana sana. Matukio au vituko haviishi katika taifa letu. Kutoka mwaka wa 1963 tuliponyakua Uhuru, majukumu fulani yalipewa kipaumbele. Haya ni elimu, maji na umasikini. Jinsi tulivyo sasa ni dhahiri kwamba taifa hili linarudi nyuma. Kamwe hatuendi mbele. Ukigusia mambo ya elimu ni shida tupu. Walimu hawatoshi na wale walioko wanadai malipo zaidi. Waziri mhusika ameweka miguu katikati; hatembei wala hasimami. Zaidi ya hayo, swala la ukosefu wa usalama linajitokeza; linawavuta na kuwatoa walimu wachache kutoka sehemu ambazo wanahitajika sana. Tume ya kuwaajiri Walimu ...
view
2 Jul 2015 in Senate:
Bw. Spika wa Muda, ningetaka kurudia yale nilikuwa ninasema; mpaka siku mhe. Rais aliyeko madarakani iwe ni sasa ama siku zijazo aandamwe na wananchi na wamlazimishe afanye yale wanayoyataka. Inafaa aingiliwe vilivyo hadi anyanyue mbio. Hivyo atakuwa ameweka rekodi ya kusema kwamba kama hutendi yale matendo yanayofaa, Wakenya hawatakupatia nafasi. Labda nimejielezea kwa lugha ngumu kidogo, lakini hivyo ndivyo nilivyomaanisha. Inafaa Wakenya walalamike wazi wazi na kukataa kutendewa maovu. Ni dhahiri kwamba mhe. Rais wa kwanza wa Taifa letu la Kenya ndiye aliyemiliki mashamba makubwa zaidi. Mhe. Rais wa pili ndiye anayemfuata, na mhe. Rais wa tatu anawafuata. Huyu wa ...
view
2 Jul 2015 in Senate:
Bw. Naibu Spika wa Muda, kuna chanzo cha kila tatizo. Tatizo halitokei bila sababu. Hivi leo shida ya nchi yetu ni uharibifu wa mali ya Wakenya na mpangilio mbaya ambao pesa zinachukuliwa na kuwekwa pahali itatoa marupurupu. Tunapoongea juu ya matatizo haya, hatuwezi kukosa kusema kwamba chanzo cha matatizo haya ni uongozi mbaya. Ni nani anayebeba msalaba wa kutoa uongozi mwema na kujaza pengo la mahitaji ya Wakenya? Ni sisi viongozi. Watu wasikubaliwe kufanya wanavyotaka katika nchi hii bila kushtumiwa. Hatuwezi kusingizia kuwa Hoja hii ni juu ya waalimu, kwa hivyo tusiongee mambo mengine ila tu kumshtumu Bw. Sosion, kwa ...
view