All parliamentary appearances
Entries 431 to 440 of 461.
-
22 Apr 2009 in National Assembly:
On a point of order, Mr. Speaker, Sir. Would I be in order to request that you put the Question, because, generally, the mood of the House is known? Could you call upon the Mover to reply?
view
-
18 Feb 2009 in National Assembly:
Jambo la nidhamu, Bw. Naibu Spika. Waziri anayezungumza amesema kwamba ikiwa Waziri yeyote anaweza kushindwa na kazi, achukue hatua ya kuwajibika kisiasa. Hivi majuzi, Bunge liliweza kufutilia mbali na kuzamisha katika kaburi la sahau, hatua ya Serikali ya kubuniwa kwa jopo la kuchunguza maafa ya kisiasa. Mswada huo uliletwa na afisi yake. Yeye, kwanza, angechukua hatua ya kujiuzulu kisiasa. Hiyo itakuwa ni kuwajibika kisiasa ndani ya Serikali!
view
-
17 Feb 2009 in National Assembly:
Ahsante sana, Bw. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi hii. Kwanza, ningependa kuipongeza Kamati ya Bunge inayohusika na masuala ya ukulima kwa kuwasilisha Ripoti mbele ya Bunge hili ili ijadiliwe. Tangu Mwenyekiti mpya, Bw. Mututho, achukue usukani katika Kamati hiyo, tunatarajia kuwa mambo mengi yatatokea. Tutaweza kuelewa sana mambo ya kilimo katika taifa la Kenya. Lazima tukumbuke kwamba kilimo ndicho uti wa mgongo wa taifa la Kenya. Sekta ya kilimo imekumbwa na matatizo mengi. Katika sekta hii ya pareto, itakumbukwa kwamba wakulima wengi waliweza kuangamia na kufutilia mbali kilimo cha pareto katika taifa la Kenya. Katika miaka ya tisini, ...
view
-
17 Feb 2009 in National Assembly:
Bw. Naibu Spika wa Muda, ufisadi katika sekta ya kilimo ni kielelezo cha kila siku. Ripoti kama hii inapotolewa, ni lazima iwe kielelezo kwa Wizara ya Kilimo kuhakikisha kuwa uchunguzi unafanywa katika kila sekta, ili wakulima waweze kufaulu.
view
-
17 Feb 2009 in National Assembly:
Bw. Naibu Spika wa Muda, Ripoti hii inaonyesha kwamba wakulima walitia bidii ya jino na ukucha na kutoa jasho yao ili waweze kupata mlo. Waliweza kuwasilisha pareto yao katika mwaka wa 2002, lakini walilipwa baada ya miaka mitatu au minne. Jambo hilo limewafanya wakulima wengi sana kuingiliwa na upweke. Vile vile, hadi sasa, wakulima waliopeleka pareto yao hawajalipwa. Huo ni ufisadi wa hali ya juu! Katika Bajeti ya Serikali kila mwaka, kuna pesa ambazo huwekwa katika sekta hiyo. Lakini haijulikani ni nani hulipwa pesa hizo! Kwa hivyo, wakulima wamekuwa samaki wadogo, huku samaki wakubwa wanaosimamia kampuni hiyo wakila!
view
-
17 Feb 2009 in National Assembly:
Vile vile, Bw. Naibu Spika wa Muda, katika Ripoti iliyotolewa na Kamati ya Bunge, inasemekana kwamba kulikuwa na shamba la zaidi ya ekari 850, ambalo liliuzwa kwa Kshs33 milioni. Wale waliolinunua shamba hilo walilipa Kshs19 milioni peke yake. Mpaka sasa, pesa zilizozalia hazijalipwa!
view
-
17 Feb 2009 in National Assembly:
Tatizo tulilo nalo katika taifa hili la Kenya ni ukosefu wa mbinu mpya za udadisi, uchunguzi na uzalishaji, kutokana na uongozi mbovu. Kwa vile shamba hilo liliuziwa mtu binafsi ili atumie katika kazi zake yeye mwenyewe, jambo hilo lilifanya Serikali kukosa namna ya kuweza kutoa maonyesho ya kisasa ya kilimo kwa wakulima!
view
-
17 Feb 2009 in National Assembly:
Bw. Naibu Spika wa Muda, tatizo lingine ambalo lilitokea pale ni kwamba wale walionunua shamba hilo hawajakamilisha kulipa pesa zile. Ni kana kwamba Kamati hiyo ama Bodi ilikuwa na nia ya kuliuza lile shamba, ili kupata fedha za kuendelesha kazi za Wizara. Lakini mpaka sasa, limebaki deni ambalo halijalipwa. Ndiyo maana tunasema kwamba lazima uchunguzi ufanywe!
view
-
17 Feb 2009 in National Assembly:
Bw. Naibu Spika wa Muda, Bodi hiyo ilianza kupigwa na mvua ama kupata kichapo cha mbwa msikitini wakati Waziri aliyekuwepo wakati huo, Bw. Kipruto arap Kirwa, alipomchagua mama ambaye alikuwa anaitwa Madam Sego. Hapo ndipo matatizo yalipoanza kuikumba Bodi hiyo. Lakini nawashukuru watu wa Cherangany kwa sababu walichukua hatua madhubuti na ya haraka na kuhakikisha kwamba wamemng'atua uongozini kwa sababu tabia kama hiyo ingejikita mizizi. Walifanya kile ambacho Halmashauri ya Kufanya Uchunguzi katika Taifa la Kenya haingefanya! Kwa hivyo, natoa shukrani kubwa sana kwa watu wa eneo la Bunge la Cherangany kwa kumleta kijana mufti, tena ambaye ana tabia "kuli-kuli" ...
view
-
17 Feb 2009 in National Assembly:
Vile vile, Bw. Naibu Spika wa Muda, natoa changamoto kwa Serikali kwamba, kutokana na Ripoti ambayo imeletwa hapa--- Serikali imepoteza pesa zaidi ya Kshs3.5 bilioni katika sakata ya ufisadi katika halmashauri hiyo. Tungependa hatua kali ichukuliwe ili iwe kielelezo na mfano mzuri
view