Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 11 to 20 of 121.

  • 10 Jul 2024 in Senate: Asante sana, Bw. Spika. Ninachukua nafasi hii niweze kujumuika na Seneta mwenzangu wa kutoka katika Jimbo la Mombasa, Sen. Faki kwa kuunga mkono swala hili ambalo amelileta siku ya leo, ya kwamba, Kiswahili kitukuzwe katika Jamhuri yetu ya Kenya. Bw. Spika, nimefurahishwa na Taarifa ambayo ametoa siku ya leo. Ni vizuri ibainike ya kwamba, tunapofanya campaign katika Jamhuri yetu ya Kenya, sisi hutumia lugha ya Kiswahili ili wananchi waweze kuelewa ni mambo gani ambayo tutaweza kuwafanyia tukichaguliwa. Tunapofika katika Bunge, Miswada inachapishwa kwa lugha ya Kingereza. Jambo hilo huwa linatatiza wananchi wetu tunao waakilisha ikizingatiwa kwamba, kuna asilimia kubwa ambao ... view
  • 10 Jul 2024 in Senate: Asante. view
  • 9 Jul 2024 in Senate: Asante, Bw. Naibu Spika, kwa kunipa nafasi pia niweze kujumuika pamoja na Senators wenzangu kuunga mkono Hoja hii ambayo imeletwa na Kiongozi wa Walio Wengi katika Bunge hili na pia ukaungwa mkono na Kiongozi wa Walio Wachache. Naungana pamoja na Wakenya na viongozi wenzangu kutoa risala za rambi rambi kwa familia za vijana wetu ambao walipoteza maisha yao wakati ambapo walikuwa wamejitokeza kupigania haki yao katika sehemu mbali mbali za Jamhuri yetu. Vijana hawa ambao wamepoteza maisha yao walikuwa na umri mdogo sana. Walikuwa wanaelekea katika umri ambao wanaweza kutegemewa katika jamii. Lakini, kwa sasa, wamepoteza maisha yao. Kwa hivyo, ... view
  • 9 Jul 2024 in Senate: nchi yetu. Wanaongea jambo la kweli kwa sababu tunapoongea, asilimia kubwa ya vijana katika Jamhuri ya Kenya hawana kazi. Kwa hivyo, wakati wanapotoa kilio, wanaposimama na kusema kwamba wanapigania haki zao za ukosefu wa kazi, wako na haki ya kusikizwa ili ijulikane ni nini wanachozungumzia. Sio kuwachapa na kuwafukuza kwa njia ambayo haistahili. Ni vizuri wasikizwa. view
  • 9 Jul 2024 in Senate: Wanadai kwamba, Bw. Spika wa Muda, matibabu katika sehemu mbali mbali katika Jamhuri ya Kenya yamekuwa duni. Hicho ni kilio cha haki kwa sababu tumeona kwamba huduma zimedorora katika sekta ya matibabu kwa muda mrefu. Kwa hivyo, wanapolia na kusema kwamba matibabu hayako vile inavyostahili katika nchi yetu, wanaongea jambo la haki. Elimu ni jambo lingine ambalo limeleta shida katika Jamhuri yetu ya Kenya. Gharama ya kusomesha watoto imekuwa juu. Wazazi wamelia kwamba karo za shule zime enda juu. Ikizingatiwa pia vile vile, gharama ya shule za upili imepanda. Tukiingia katika vyuo vikuu, unakuta pia gharama imepanda. Kwa hivyo, wanapotoa ... view
  • 9 Jul 2024 in Senate: Unakuta kwamba leo wamepewa barua kusimamishwa kazi na kuambiwa, “mmepewa hadi mwezi wa saba kutoka hapa mwende nyumbani, hakuna kazi view
  • 9 Jul 2024 in Senate: Ni jambo la huzuni kubwa sana ikizingatiwa kwamba vijana hao katika Jamhuri yetu ya Kenya ndio viongozi wetu wa kesho. Ni watu wenye nguvu ambao Serikali inafaa iwalinde sana kwa sababu ndio watakaotengeneza uchumi wa nchi na Jamhuri yetu ya Kenya ili isonge mbele. Tumeona juzi kamati yetu ya Agriculture, Livestock and Fisheries ilikuja kuthathmini kashfa ya fertilizer ambayo imekumba nchi hii yetu ya Kenya. Corruptio n ambayo iko katika Ministry of Agriculture, Livestock and Fisheries saa hii ni kwamba lazima Serikali iaangalie jambo hili kwa kina na ione kwamba hilo jambo limeathiri Wakenya limeshughulikiwa na kuwekwa katika kaburi la ... view
  • 9 Jul 2024 in Senate: waliopewa haikuwasaidia na wameingia hasara. Kwa hivyo, unaporeconstitute C abinet yako, yule Waziri awe ni wa kwanza kukanyaga mlango na kutoka nje. Atakapotoka nje, tupate Waziri ambaye atakuwa competent katika kufanya kazi ya kuinua hali ya uchumi katika Jamhuri yetu ya Kenya kupitia kilimo. Bw. Spika wa Muda, tulipokuwa wadogo, nakumbuka vizuri sana marehemu hayati Rais wa Pili katika Jamhuri wa Kenya alikuwa anasema kwamba kilimo ndio uti wa mgongo wa uchumi wa Kenya. Nakubaliana na jambo hilo. Kwa hivyo, tunaposema kwamba tunataka kiongozi ambaye ana ukakamavu, uwezo na experience ya kuendesha view
  • 9 Jul 2024 in Senate: ile ya kilimo, tunasema jambo la haki. Linafaa lisikizwe na tuone kwamba tumewekewa kiongozi ambaye atapeleka Kenya mbele katika masuala ya kilimo. Nikiendelea kujadilia mambo ya corruption, katika serikali zetu za kaunti, kuna nafasi nyingi sana ambazo zilikuwa zimetolewa za kazi. Tumeona corruption ikiwa na magavana wetu katika kaunti zote 47. Magavana wengine wanaandika vijana kazi kupitia discrimination . Hilo ni jambo ambalo tunafaa kulilaani katika Bunge hili na tuseme kwamba kijana yeyote ambaye ana view
  • 9 Jul 2024 in Senate: ya kuajiriwa kazi katika kaunti yake aweze kupata kazi. Tusiandike wananchi wetu kazi kwa kujuana, kuwa alinifanyia campaign au alisimama nami katika mambo tofauti. Tupatie watu competent wafanye kazi na vijana ambao wamehitimu na kusoma ili Kenya yetu isonge mbele. Bw. Spika wa Muda, ningependa nitoe pendekezo kwamba ili Kenya lsonge mbele, jambo la kwanza ni kwamba Serikali hii lazima ipigane na ufisadi kabisa. Itakapopigana na ufisadi, hizi pesa ambazo zinapotea kila uchao zitakosa mashimo ya kuingia na zitafanyia wananchi kazi. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can ... view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus