20 Aug 2024 in Senate:
Thank you, Mr. Speaker, Sir, for giving me this opportunity to contribute to this very important Motion. Mr. Speaker, Sir, I was privileged to be among the people that vetted the IG of Police. I want to confirm to this House that the IG demonstrated a wide range of experience for 39 years. The committee was convinced beyond reasonable doubt that Mr. Kanja is suitable for that position. On the issue of insecurity; I was very much concerned about the issues of insecurity and how he would handle these issues. Nonetheless, he was very eloquent in terms of elaborating on ...
view
14 Aug 2024 in Senate:
Bw. Spika, ningependa kuchukua fursa hii kuchangia mjadala huu unaohusu watu wa Meru. Napinga Hoja hii kwa sababu si vizuri kuwachia Maseneta 11 kuamua hatima ya watu wa Meru ikizingatiwa kuwa hii ni mara ya tatu kwa Gavana huyo kuletwa katika Seneti. Jambo hili linafaa kuangaziwa na Seneti nzima ili kutoa uamuzi. Maseneta 67 wataangazia jambo hili kwa kina na kwa njia itakayosaidia wakaazi wa Kaunti ya Meru. Kuna mambo ambayo Gavana wa Meru ameshtumiwa kufanya. Tukiwa na vikao hapa, mambo hayo yatakuwa yanaangaziwa si na Kenya pekee bali ulimwengu mzima. Watu watakuwa wakifuatilia ili kuona uamuzi wa Seneti. Bw. ...
view
10 Jul 2024 in Senate:
Asante sana, Bw. Spika. Ninachukua nafasi hii niweze kujumuika na Seneta mwenzangu wa kutoka katika Jimbo la Mombasa, Sen. Faki kwa kuunga mkono swala hili ambalo amelileta siku ya leo, ya kwamba, Kiswahili kitukuzwe katika Jamhuri yetu ya Kenya. Bw. Spika, nimefurahishwa na Taarifa ambayo ametoa siku ya leo. Ni vizuri ibainike ya kwamba, tunapofanya campaign katika Jamhuri yetu ya Kenya, sisi hutumia lugha ya Kiswahili ili wananchi waweze kuelewa ni mambo gani ambayo tutaweza kuwafanyia tukichaguliwa. Tunapofika katika Bunge, Miswada inachapishwa kwa lugha ya Kingereza. Jambo hilo huwa linatatiza wananchi wetu tunao waakilisha ikizingatiwa kwamba, kuna asilimia kubwa ambao ...
view
9 Jul 2024 in Senate:
Asante, Bw. Naibu Spika, kwa kunipa nafasi pia niweze kujumuika pamoja na Senators wenzangu kuunga mkono Hoja hii ambayo imeletwa na Kiongozi wa Walio Wengi katika Bunge hili na pia ukaungwa mkono na Kiongozi wa Walio Wachache. Naungana pamoja na Wakenya na viongozi wenzangu kutoa risala za rambi rambi kwa familia za vijana wetu ambao walipoteza maisha yao wakati ambapo walikuwa wamejitokeza kupigania haki yao katika sehemu mbali mbali za Jamhuri yetu. Vijana hawa ambao wamepoteza maisha yao walikuwa na umri mdogo sana. Walikuwa wanaelekea katika umri ambao wanaweza kutegemewa katika jamii. Lakini, kwa sasa, wamepoteza maisha yao. Kwa hivyo, ...
view
9 Jul 2024 in Senate:
nchi yetu. Wanaongea jambo la kweli kwa sababu tunapoongea, asilimia kubwa ya vijana katika Jamhuri ya Kenya hawana kazi. Kwa hivyo, wakati wanapotoa kilio, wanaposimama na kusema kwamba wanapigania haki zao za ukosefu wa kazi, wako na haki ya kusikizwa ili ijulikane ni nini wanachozungumzia. Sio kuwachapa na kuwafukuza kwa njia ambayo haistahili. Ni vizuri wasikizwa.
view
9 Jul 2024 in Senate:
Wanadai kwamba, Bw. Spika wa Muda, matibabu katika sehemu mbali mbali katika Jamhuri ya Kenya yamekuwa duni. Hicho ni kilio cha haki kwa sababu tumeona kwamba huduma zimedorora katika sekta ya matibabu kwa muda mrefu. Kwa hivyo, wanapolia na kusema kwamba matibabu hayako vile inavyostahili katika nchi yetu, wanaongea jambo la haki. Elimu ni jambo lingine ambalo limeleta shida katika Jamhuri yetu ya Kenya. Gharama ya kusomesha watoto imekuwa juu. Wazazi wamelia kwamba karo za shule zime enda juu. Ikizingatiwa pia vile vile, gharama ya shule za upili imepanda. Tukiingia katika vyuo vikuu, unakuta pia gharama imepanda. Kwa hivyo, wanapotoa ...
view
9 Jul 2024 in Senate:
Unakuta kwamba leo wamepewa barua kusimamishwa kazi na kuambiwa, “mmepewa hadi mwezi wa saba kutoka hapa mwende nyumbani, hakuna kazi
view
9 Jul 2024 in Senate:
Ni jambo la huzuni kubwa sana ikizingatiwa kwamba vijana hao katika Jamhuri yetu ya Kenya ndio viongozi wetu wa kesho. Ni watu wenye nguvu ambao Serikali inafaa iwalinde sana kwa sababu ndio watakaotengeneza uchumi wa nchi na Jamhuri yetu ya Kenya ili isonge mbele. Tumeona juzi kamati yetu ya Agriculture, Livestock and Fisheries ilikuja kuthathmini kashfa ya fertilizer ambayo imekumba nchi hii yetu ya Kenya. Corruptio n ambayo iko katika Ministry of Agriculture, Livestock and Fisheries saa hii ni kwamba lazima Serikali iaangalie jambo hili kwa kina na ione kwamba hilo jambo limeathiri Wakenya limeshughulikiwa na kuwekwa katika kaburi la ...
view
9 Jul 2024 in Senate:
waliopewa haikuwasaidia na wameingia hasara. Kwa hivyo, unaporeconstitute C abinet yako, yule Waziri awe ni wa kwanza kukanyaga mlango na kutoka nje. Atakapotoka nje, tupate Waziri ambaye atakuwa competent katika kufanya kazi ya kuinua hali ya uchumi katika Jamhuri yetu ya Kenya kupitia kilimo. Bw. Spika wa Muda, tulipokuwa wadogo, nakumbuka vizuri sana marehemu hayati Rais wa Pili katika Jamhuri wa Kenya alikuwa anasema kwamba kilimo ndio uti wa mgongo wa uchumi wa Kenya. Nakubaliana na jambo hilo. Kwa hivyo, tunaposema kwamba tunataka kiongozi ambaye ana ukakamavu, uwezo na experience ya kuendesha
view