31 Mar 2015 in National Assembly:
Ahsante sana Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda . Kwa sasa hivi, tukiangalia watoto wetu kwenye mashule, wamepata umeme na wanaweza kusoma usiku. Baadhi ya hayo, kuna pia Uwezo Fund . Lakini ningependa kushikilia mambo mawili. Kwanza, ni swala sugu la ufisadi. Nilipoangalia hii Ripoti ambayo imeletwa na Tume ya Kupigana na Ufisadi, ni Ripoti ambayo kwa kusema kweli, inashika viongozi wengi katika wale ambao wamechaguliwa kisiasa. Uchunguzi wa ripoti hii haujakamilika. Lakini leo ukitajwa kua wewe ni mfisadi, nakupa mia fil mia; mwananchi aliyekupigia kura anatoka imani. Hili ni suala ambalo linatatiza sana. Niliposikia kuwa kutakuwa na ripoti kuhusu magavana ...
view
31 Mar 2015 in National Assembly:
Mhe. Naibu Spika wa Muda, historia ya watu wetu kunyang’anywa mashamba imekithiri. Zaidi ya mara tatu, tumeihusisha Tume ya Ardhi kwenye masuala ya mashamba ambayo yamechukuliwa. Lakini Tume hiyo bado haijatupatia mwelekeo wowote. Hivi sasa, hata wakazi wangu wa Lunga Lunga wanaoishi kwenye kipande cha ardhi chenye ekari 1,083 wanaondolewa. Nyumba zao zimeharibiwa na wataondolewa wakati wowote kutoka kwa mashamba hayo. Mamlaka ya Kukusanya Ushuru (KRA) hukusanya fedha ambazo hutumika kutekeleza miradi ya Serikali. Kupitia Kamati ya Fedha, Mipango na Biashara, nilitaka kujua viwango vya ushuru wa VAT wanaotozwa wanabiashara wanaoingiza magari humu nchini, na jinsi ushuru huo unavyokusanywa. Lakini ...
view
31 Mar 2015 in National Assembly:
Kwa hayo machache, naiunga mkono Hotuba ya Rais na kumpongeza kwa sababu maandalizi ya safari ya kesho huanza leo.
view
10 Feb 2015 in National Assembly:
Ahsante sana, Mhe. Spika. Kwanza kabisa, ningependa kutoa ushuhuda kuwa katika siku za mwisho, nilikuwa na mheshimiwa Muchai. Nilikaa sana naye kwa muda mrefu tukizungumza mambo mengi. Vile vile, tulipokuwa tukipitia maswala ya bajeti, alikuwa ni mmoja kati ya wale ambao walichangia sana katika hoja zile.
view
10 Feb 2015 in National Assembly:
Mhe. Spika, ningependa kutuma salamu za rambirambi kwa familia ya Muchai na watu wa Kabete. Nawapa pole kwa niaba ya watu wa Lungalunga na familia yangu kwa jumla. Hoja yangu ni kwa walinzi wetu. Inasemekana kwamba alifuatwafuatwa kutoka mbali. Ningeomba kwamba walinzi wetu wapatiwe redio kwa sababu trailing ama kufuatwafuatwa huanza mbali. Sisi katika siasa na mbio tunazokwenda tunapishana na watu wengi kimaneno na kihoja. Kwa hivyo, tunaomba usalama kwa mwananchi. Sisi kama viongozi usalama wetu uongezwe na walinzi wetu wapewe redio na wasomeshwe zaidi.
view
10 Feb 2015 in National Assembly:
Ahsante sana.
view
26 Nov 2014 in National Assembly:
Asante sana Naibu Spika wa Muda. Ningependa kwanza kumshabikia Mhe. Keynan kwa kuuleta Mswada huu. Ningependa kusema kuwa kule nje ni kubaya. Kwa wakati ule mdogo ambao nilipelekwa kwa uchaguzi mdogo, niliona kama ndoto. Ukiwapigia simu, wenzako hawashiki. Kwa hivyo, huu Mswada utawasaidia wengi. Kwa upande wa bima, wengi wa wabunge ambao wamekuwa katika viti, ningependa kutoa mifano lakini sio kwa majina, wale wa kutoka Pwani, ukiangalia hali zao sasa hivi za kiafya, zimekwenda chini kwa sababu ya kukosa matibabu. Kwa hivyo, ninaunga mkono Mswada huu ambao umeletwa Bungeni wakati ufaao.
view
26 Nov 2014 in National Assembly:
Asante sana kwa kunipatia fursa hii ili nichangie Ripoti hii kuhusu usalama. Usalama umekuwa tatizo ambalo limekuwa changamoto sana katika Serikali hii ya Kenya. Sisi viongozi wageni, tangu tuchaguliwe katika mamlaka haya, tumekuwa na changamoto nyingi sana.
view
26 Nov 2014 in National Assembly:
Asante sana, Naibu Spika wa Muda. Usalama umekuwa suala gumu. Ni suala ambalo bila vitengo vya usalama kukaa sawasawa na kubuni mipango mipya ambayo itaweza kuboresha usalama, tutakuwa kati ya wale wanaopata hasara. Ninapozungumuzia haya, ninatoa mfano wa kitegauchumi kule kwetu Kwale. Pwani, kwa jumla,tumekuwa katika hali yakutoelewa kwa nini uchumi wetu unashuka. Ukiangalia sekta ya utalii, kati ya wale wanaofaidika ni sisi watu wa Pwani. Sasa hivi, asilimia themanini ya wale ambao walikuwa wakifanya kazi kwenye hoteli hawana kazi. Kina mama ambao walikuwa wakishona viondo na vijana ambao walikuwa na lugha tofauti ya kujieleza kupitia kwa watalii, wote wamekosa ...
view
26 Nov 2014 in National Assembly:
Katika sehemu ya mpaka, niko na changamoto kubwa sana na hii changamoto nimeizungumzia muda mrefu. Sisi hatuna vifaa kama sehemu ya Lungalunga. Washikadao wa usalama na wao vile vile wanashindwa kuwafikia wakubwa wao. Hatuna magari hadi wakati huu na ukiangalia maafisa wetu, ni wachache sana. Wale wanaofanya nchi yetu kutopata usalama wanapitia kwa ile mipaka na sisi kama viongozi tumelizungumzia jambo hili sana. Ni jambo la kuhuzunisha kwamba hadi wakati huu hatujaona hatua ikichukuliwa kuhusu jambo hili.
view