Khatib Abdallah Mwashetani

Parties & Coalitions

Email

khatibabdallah@yahoo.com

Telephone

0722716614

Telephone

0723922222

All parliamentary appearances

Entries 291 to 300 of 311.

  • 29 Oct 2014 in National Assembly: Ahsante sana, mhe. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii. Kwanza kabisa ningependa kutoa shukurani kwa ndugu na rafiki yangu, Chris Wamalwa, kwa kuileta Hoja hii Bungeni. Mimi nilijikuta kwenye ulingo wa siasa kwa sababu ya marehemu Kijana Wamalwa. Nikiwa naibu mwenyekiti wa chama cha FORD(K), na kwa sababu marehemu Kijana Wamalwa alikuwa mwanzilishi wa chama chetu, ninamushabikia zaidi. Ninawaomba Wabunge wenzangu tuipitishe Hoja hii ili tuweze kumtambua kama kiongozi aliyechangia kuwepo kwetu Bungeni. Kwa hayo machache, ninaiunga mkono Hoja hii. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report ... view
  • 28 Oct 2014 in National Assembly: Asante sana, Bi Mwenyekiti. Ningependa kuunga mkono marekebisho hayo kwa sababu yametoa nguvu kwa mtu mmoja katika kutoa maamuzi. Swala la madini limeleta utata sana. Iwapo marekebisho haya yatapita, itakuwa rahisi kwa watu kuzunguka na kufanya utafiti bila kusumbua ile ardhi ambayo inatarajiwa kutolewa madini. Kwa hivyo, ninaunga mkono. view
  • 28 Oct 2014 in National Assembly: Asante sana, Mhe . Naibu Mwenyekiti wa Muda. Ningependa kuchangia na kuunga mkono kwa njia ya kuwa utafiti ukiendelea katika mashamba, wananchi walioko pale hawasumbuliwi sana. Nazungumza kwa kuwa nina sehemu yangu kule kwangu ambapo madini yametafutwa na wananchi wako palepale na leseni imepeanwa. Lakini sasa hivi kulingana na mikakati iliyokuwepo – Pengine hawakufuata mikakati kisawasawa ikaregeshwa nyuma na ikachukuliwa na Serikali. Kwa hivyo, kwa upande wangu, mimi husema kuwa katika utafiti hakuna suala la kusumbuliwa kwa wananchi kivyovyote. Kwa hivyo, naunga mkono. view
  • 10 Sep 2014 in National Assembly: Ahsante sana Mhe. Spika kwa kunipa fursa hii ili nichangie Hoja hii ambayo imeletwa mbele yetu. Ningependa kwanza kumpongeza Rais kwa kuchagua mabalozi hawa. Vile vile ninampongeza Rais kwa kuangalia sehemu zote za Kenya. Alihakikisha kwamba mhakilishi ametoka kila sehemu ya nchi yetu ya Kenya. view
  • 10 Sep 2014 in National Assembly: Mhe.Spika, ninatoa shukrani kwa Kamati ambayo imeunda Ripoti hii, mbali na kuwa ina matatizo hapa na pale. Sisi ni wanadamu na hakuna aliyekamili. Kwa hivyo ninawapongeza. Vile vile ninatoa kongole kwa wale ambao walichaguliwa kuwa wakilishi wa nchi yetu ya Kenya. Ninashukuru kwa kuchaguliwa kwa mmoja wetu kuwa Balozi wa Tanzania. Mhe. Mwakwere amepata fursa hii kutokana na ujuzi alionao. Mbali na kuwa ana umri mkubwa, zote tunatambua juhudi zake na alivyochangia katika Serikali hii kuweza kuwa mahali ilipo. Kwa hivyo, natoa kongole vile vile. view
  • 10 Sep 2014 in National Assembly: Mhe.Spika, ningependa kueleza Bunge hili kuwa Kiswahili ni lugha ambayo imetambulika Kikatiba. Katika fikra zangu si lazima uzungumze Kiingereza sana ndio utambulike kuwa umesoma. Mhe. Amb. Sheikh Dor, leo tungekuwa tunatambua hali yake kulingana na elimu aliyonayo--- Mhe. Dor ni kiongozi ambaye katika kifua chake ametambua anaweza kusoma Quran yuzuu thelathini pasipona kusita wala kukosea hata sentensi moja. Hiyo ni katika jarida la juu zaidi ya yule professor ambaye anatambulika katika wakati wa sasa. Kama tunavyojua sasa hivi, makaratasi ya udaktari na professor yanaweza kupatikana sehemu zo zote kwenye Kenya hii. Lakini hauwezi kuielewa na kuitambua Qurani kwa kupitia njia ... view
  • 10 Sep 2014 in National Assembly: Bw. Spika, nikimalizia, ningependa kumpa kongole Rais kwa kumteua dada Sophie Kadzo ambaye ametoka katika familia dogo na hatambuliki Kenya hii. Hii inaonyesha ishara ya kuwa tunakoelekea, mtu ambaye si mtu anaweza kuwa mtu kulingana na uongozi ambao uko wakati huu. view
  • 10 Sep 2014 in National Assembly: Nikimalizia kabisa, ninajua sasa hivi tuko kwenye utata wa kura ya maoni. Mambo mengi ambayo yametajwa katika kura ya maoni ni mambo ambayo tuko na imani kuwa sisi hapa kama Wabunge tunaweza kuyamaliza. Tumezungumza maswala ya kuhakikisha kuwa sura za wakenya ziko kila mahali na hili ni dhihirisho tosha kuwa Serikali ambayo ipo inayatambua maoni yetu kama Wabunge. Tumepewa fursa hii kubadili ama kutatua matatizo yalioko. view
  • 10 Sep 2014 in National Assembly: Kwa hayo machache, naunga mkono Ripoti hii. view
  • 25 Jun 2014 in National Assembly: Thank you, hon. Speaker. My request for Statement goes to the Chairman of the Departmental Committee on Finance, Planning and Trade regarding the criteria used by Kenya Revenue Authority (KRA) to determine duty payable to imported motor vehicles. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus