All parliamentary appearances
Entries 131 to 140 of 186.
-
15 Nov 2006 in National Assembly:
Kuna swala la wezi wa mashamba. Ukiangalia kijitabu hiki nilichonacho, utakuta kwamba kuna orodha ndefu ya majina ya watu ambao walinyakua mashamba katika maeneo ya misitu, kwa mfano, misitu ya Ngong, Kiptagich, Karura, Nyandarua na kwingineko. Tunajua majina ya watu walionyakua mashamba katika maeneo haya na tutayatwaa hayo mashamba kutoka kwao. Ni sharti Serikali itwae mashamba yaliyonyakuliwa ili iweze kuwapatia wale ambao wanastahili kuwa nayo. Aidha, mashamba hayo yarudishwe mikononi mwa Serikali ili tuweze kuyafanyia maendeleo.
view
-
15 Nov 2006 in National Assembly:
Kama wewe ni mmoja wa wale walionyakua mashamba, basi kaa chonjo kwa sababu tutakuchukulia hatua!
view
-
15 Nov 2006 in National Assembly:
Bw. Naibu Spika wa Muda, nilikuwa nasema kwamba wizi wa mashamba uko pahali pengi na siyo tu katika maeneo ya misitu. Mimi ninatoka Subukia, ambako kwa miaka mingi, watu ambao walikuwa wanachama katika makampuni yaliyonunua mashamba kutoka kwa wazungu ili yaweze kuwagawia Waafrika, wamekosa mashamba. Watu walinyang'anywa mashamba yao wakati wa utawala wa giza katika nchi hii. Ingawa watu walinunua hisa katika makampuni kama vile Ngwataniro, Ndeffo au Kihoto, watu hao wanashikilia stakabadhi za mashamba yao lakini hawana mashamba yenyewe kwa sababu walinyang'anywa. 3676 PARLIAMENTARY DEBATES November 15, 2006 Ingawa tunaongea kwa niaba ya Serikali, tungetaka Wizara ya Ardhi ielewe ...
view
-
15 Nov 2006 in National Assembly:
On a point of order, Mr. Temporary Deputy Speaker, Sir. Is the hon. Member in order to allege that I was given land, I do not know by who, when, in fact, all the land that I own is the one that I bought? I have never been given land. Could he substantiate that I was given land by anyone by presenting documents here that prove his point?
view
-
15 Nov 2006 in National Assembly:
On a point of order, Mr. Temporary Deputy Speaker, Sir. We will be here tomorrow, and the day after, and I will love to see his substantiation and then we can continue from there.
view
-
18 Oct 2006 in National Assembly:
Bw. Naibu Spika wa Muda, ningeomba kutoa dakika mbili kwa Mhe. Onyancha halafu nitaendelea na kujibu.
view
-
18 Oct 2006 in National Assembly:
Bw. Naibu Spika wa Muda, kwanza, ningetaka kumpongeza Prof. Anyang'-Nyong'o kwa kuleta Hoja hii ambayo tunaomba kuunga mkono. Tunatoka katika enzi ya giza; kule ambako mambo mengi sana yalifichwa. Tunaelekea kule ambako tunaamini kutakuwa na mwangaza. Kwa sababu hiyo, itakuwa vigumu sana Mbunge yeyote kupinga Hoja ya aina hii. Kusema kweli, Wizara imetayarisha Mswada kuhusu uhuru wa habari. Mswada huu utakuwa tayari hivi karibuni. Mara tu utakapokuwa tayari, tutauwasilisha hapa Bungeni ili Wabunge waweze kuujadili na, ninatumai, kuupitisha. Hata hivyo, Bw. Naibu Spika wa Muda, nimezungumza na Prof. Anyang'-Nyong'o humu ndani kwa muda wa dakika chache na tumekubaliana ya kwamba ...
view
-
18 Oct 2006 in National Assembly:
Bw. Naibu Spika wa Muda, Hoja hii ni muhimu sana. Hatuwezi tukashinda vita vya kupigana na ufisadi bila uhuru wa habari. Ufisadi ni kufichua wizi na huwezi kufichua wizi, bila habari. Sheria hii itatusaidia kupigana na uongo tunaosoma katika vyombo vya habari. Uhuru huu ukiwepo, na kama watu wataweza kupewa habari zilizo sahihi, basi mtu akipatikana anasema uongo itakuwa ni haki mtu huyo kuchukuliwa hatua. Kwa hivyo, naamini sheria hii itatusaidia kuondoa uongo wakati wa kupatia watu wetu habari, yaani upotoshaji wa habari. Unakwenda kwa mkutano na unasema moja, lakini ukiangalia magazeti keshoye, habari ni tofauti kabisa hata huwezi kutambua ...
view
-
18 Oct 2006 in National Assembly:
Bw. Naibu Spika wa Muda, niliangalia na nikapata nilikuwa na dakika 20. Bw. Naibu Spika wa Muda, hata hivyo, ninaunga mkono Hoja hii lakini ninatumai ni habari sahihi---
view
-
18 Oct 2006 in National Assembly:
On a point of order, Mr. Temporary Deputy Speaker, Sir.
view