Maison Leshoomo

Parties & Coalitions

Born

1962

Post

Parliament Buildings
Parliament Rd.
P.O Box 41842 – 00100
Nairobi, Kenya

Email

laikipiawest@parliament.go.ke

Telephone

0724958726

Maison Leshoomo

The fact that she received limited education doesn’t stop her from pursuing her dreams. As a victim of retrogressive culture, Leshoomo vows to help other girls to be educated to beat cultural norms that act as a hurdle. Maison’s political journey arose out of a gutsy choice she made to attend public meetings against her husband’s orders. The move opened the door for her to become a nominated councilor in 1992 a position she maintained for 10 years. She joined Maendeleo ya Wanawake in 1995 and rose to become the chairperson in Maralal District. In 2008, the Party of National Unity (PNU) nominated her to parliament. As a long serving member of the Samburu District Peace Committee, she has taken it upon herself to promote peace between the Samburu and the neighbouring communities.

All parliamentary appearances

Entries 1 to 10 of 291.

  • 18 Feb 2020 in National Assembly: Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi hii. Nampa Mheshimiwa hongera kwa kuleta Hoja hii ya nzige. Kulingana na jinsi wenzangu walivyoongea, nzige hawajaanza kuja leo. Nzige walikuja kitambo sana. Kuna wakati walikuja wakati wa ukoloni. Wakati walipoingia Kenya enzi za ukoloni, nzige wana madhara mengi ya kula miti, matawi na nyasi. Baada ya hapo, kuna ugonjwa wa ng’ombe. Kwa hivyo, tunalia kwani hili ni janga baya zaidi. Hili ni jambo ambalo limetushtua sisi ambao tuna wanyama kama ng’ombe. Tunajua baada ya nzige kuisha na dawa ama kuisha kwa njia yoyote, wataleta ugonjwa wa ng’ombe. Tumetembea upande ... view
  • 18 Feb 2020 in National Assembly: North Horr wakati waliingia upande wa Marsabit. Nzige hao ni wengi sana. Pia vile wenzangu wamesema, wanazaa kila baada ya masaa mawili. Wakati wanamwaga mayai, hata ukisimama wakati wanapita wanamwaga kinyesi chao na wewe mwenyewe unakuwa mweusi The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor. view
  • 18 Feb 2020 in National Assembly: kama makaa. Huwa wanamwaga mbegu zao na wanawacha hapo chini. Saa hii tumeshtuka sana kwa sababu nzige hawa wana ugonjwa ambao tunaogopa hata sasa. Mara ya kwanza walipomwaga dawa hiyo, haikuwaua wale nzige. Badala ya kufa, wakaanza kushuka chini na kufagia kila kitu vile ambavyo trekta hufagia. Hutaona nyasi hata moja. Ni jambo ambalo litaleta shida katika Kenya nzima kwa sababu nzige wanahama na yale mayai yamemwaga pale ndiyo yanaamka. Naomba Serikali iamke na kuangalia ile dawa inamwagwa kwa sababu isipopimwa vizuri, tunaogopa kuwa italeta shida. Pahali ambapo dawa inamwagwa hapa chini panakauka. Nyasi inakauka. Tuna shida na ni lazima ... view
  • 10 Feb 2020 in National Assembly: Asante sana, Mhe. Spika kwa kunipatia nafasi hii nitoe pole zangu na za familia yangu na Kaunti ya Samburu kwa baba yetu Moi. Tunamkumbuka Baba Moi kwa mengi sana. Kile amefanyia Kaunti ya Samburu hatuwezi kusahau. Tunaamini yeye ndiye mtu wa kwanza kuanzisha shule ya upili ya wasichana katika Kaunti ya Samburu. Hatuwezi kusahau hata kidogo. Kila Mkenya anakumbuka kwamba Baba Moi hakuwa rais wa kuchezewa. Alikuwa rais wa kuheshimiwa zaidi. Ukiangalia kati yake na rais wa sasa, unaona kuna tofauti kubwa sana. view
  • 30 Oct 2019 in National Assembly: Asante sana, Mhe. Spika, kwa kunipatia hii nafasi ili niunge mkono Ombi la Hon. Lentoimaga. Kuna maana ya Mhe. Lentoimaga kuandika Ombi hili. Nafikiri tuko na shida kubwa sana kuhusu haya mambo ya wizi wa mifugo. Sijui kwa nini inaitwa wizi wa mifugo ilhali ni kitu inaua wananchi katika pembe zote. Vita vilivyoko Baragoi ni mbaya zaidi. Ninaomba Kamati ya Usalama ichukue hatua na ihakikishe Waziri wa Usalama awe hapa ili wakutane. Shida kubwa iko kwenye hii ofisi. Watu wanauawa na inaporipotiwa, hakuna mtu anayejitokeza kuwa ni kweli watu wameuawa. Mali inaenda na watu wanaachwa bila chochote. Hakuna mtu anaangalia ... view
  • 30 Oct 2019 in National Assembly: Miaka nenda miaka rudi, watu wamekuwa maskini na wengine kuuliwa. Hata sasa, tuko na watu karibu wanne ambao wako hospitalini Nakuru. Wamevunjika miguu na hakuna mtu anayewashughulikia. Wanapigana na kuuana tu ilhali Serikali iko kila mahali. Ng’ombe wanapita tu wakiangaliwa. Pia wao wanauliwa na hakuna hatua inayochukuliwa. Ninaunga mkono Kamati ya Usalama ichukulie maanani Ombi hili. Ni suala ambalo halina mchezo. Asante Bwana Spika kwa kunipatia hii nafasi. view
  • 16 Oct 2019 in National Assembly: Asante sana, Mheshimiwa Naibu Spika. Naunga mkono Mswada huu. Mambo ya wanyama wetu ni mengi. Niko katika Kamati ya Ukulima. Kila wakati huwa tunajiuliza ni kwa nini wafugaji wetu hawana njia yoyote ya kufaidika kutokana na wanyama wao. Sababu ya kutofaidika ni kwamba hawana soko lolote la kuuza wanyama. Hawana mahali pa kuchinjia wanyama. Katika Kenya nzima, hakuna mtu anayeweza kula chakula bila nyama. Unapokula nyama ndipo unahisi umekula chakula. Wanaofuga wanyama huwa wanaumia sana kwa sababu wakati wa ukame, wanyama wote wanakufa kwa sababu hakuna mahali pa kuwauza. Wakati mvua inaponyesha na wanyama wanapopata nguvu, wafugaji wanakosa mahali pa ... view
  • 16 Oct 2019 in National Assembly: ya wanyama. Ni muhimu kwa sababu wafugaji wa wanyama wanaumia kwa sababu hawana njia yoyote ya kufaidika au kusaidia familia zao kutokana na wanyama wao. Wale wanaokuza miwa, majani na kahawa wako na njia zote za kujisaidia. Wana soko. Kwa mfano, kuna soko la Kahawa ya Kenya katika kila nchi. Tukipata bodi inayoweza kuwasaidia wafugaji wa wanyama, watapata njia za kufaidika. Tunajua vizuri sana kwamba wafugaji wa wanyama humu nchini hawana njia yoyote ya kujifaidisha isipokuwa kutokana na hao wanyama. Kule Samburu ninakotoka na katika sehemu nyingine kama Laikipia, Turkana na Pokot, utaona wanyama wanapigwa risasi kama wanyamapori. Kwa sababu ... view
  • 15 Oct 2019 in National Assembly: Asante, Mhe Spika kwa kunipatia nafasi hii. Sote tuna maoni kuhusu misitu kwa sababu misitu inaathiri maisha ya wananchi wote nchini. Wakati watarudia kuangalia Ripoti hiyo, nawaomba Mwenyekiti na The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor. view
  • 15 Oct 2019 in National Assembly: Kamati yake wazunguke Kenya nzima kwa sababu kuna shida ya misitu kila pahali, haswa katika Kaunti ya Samburu. Tuko na shida kubwa. Wengine wetu ni wakimbizi. Tulizaliwa kwenye msitu na hatuna mahali pakuita kwetu hadi leo. Kwa hivyo, naomba kuwa ikiwa watarudia, wazunguke Kenya yote. Asante. view