The fact that she received limited education doesn’t stop her from pursuing her dreams. As a victim of retrogressive culture, Leshoomo vows to help other girls to be educated to beat cultural norms that act as a hurdle. Maison’s political journey arose out of a gutsy choice she made to attend public meetings against her husband’s orders. The move opened the door for her to become a nominated councilor in 1992 a position she maintained for 10 years. She joined Maendeleo ya Wanawake in 1995 and rose to become the chairperson in Maralal District. In 2008, the Party of National Unity (PNU) nominated her to parliament. As a long serving member of the Samburu District Peace Committee, she has taken it upon herself to promote peace between the Samburu and the neighbouring communities.
5 Jan 2022 in National Assembly:
On a point of order, Hon. Deputy Speaker.
view
5 Jan 2022 in National Assembly:
Asante sana, Mheshimiwa Naibu Spika kwa kunipa nafasi hii. Tuna sheria ambazo zinalinda Bunge hili. Ningeomba mtumie sheria hizo ili tumalize Mswada huu. Ningependa pia kuuliza kama mashine za upande huu na upande huo mwingine ni tofauti. Ni muhimu tuelewe kwa sababu ninafikiria kuwa tunatumia mashine aina moja.
view
5 Jan 2022 in National Assembly:
Niruhusu nimalize.
view
5 Jan 2022 in National Assembly:
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kweli, mashine hii ni moja. Hata upande huu tulikuwa na shida na kadi zetu lakini zilirekebishwa. Tuko hapa kupitisha sheria na tunaangaliwa na Wakenya wote. Ningeomba tupige kura kama watu wazima wanaojua wanachokifanya. Ni lazima pia tutumie sheria.
view
5 Jan 2022 in National Assembly:
Ingekuwa vyema tukiheshimiana. Kila mtu aheshimu mwingine. Tupige kura na watakaoshinda ndio watakuwa washindi. Tafadhali tuwache kuzungumza sana. Mashine ni moja na ni lazima tuendelee.
view
1 Dec 2021 in National Assembly:
Ahsante sana, Mhe. Spika kwa kunipatia nafasi ili niungane na wenzangu kumshukuru Rais wetu, Uhuru Muigai Kenyatta, kwa kazi ambayo amefanya. Mhe. Spika, kusema ukweli, Rais alitaja sekta zote katika nchi hii ambazo amefanyia kazi. Kila Mkenya ameona kile Mhe. Rais amefanya. Katika utawala wake, amefanya mengi. Ni vyema tujue kama Wakenya kuwa wakati alichukua usukani kama Rais, alipata wakati mgumu sana. Hii ni kwa sababu alichukua usukani akiwa bado na kesi kule Hague na pia hali ya usalama ilikuwa imedorora. Kwa hivyo, ameweza kufanya kazi miaka minne tu pekee. Katika miaka minne, kila Mkenya ameona kile Rais amefanya. Sisi ...
view
1 Dec 2021 in National Assembly:
shukrani kwa yale ambayo ametendea wengine. Tunaomba Mungu amlinde Rais Uhuru na aendelee na moyo huo wa kuishikilia Kenya hata anapostaafu. Hatakufa na atarudi tu. Kama Katiba ingebadilishwa, tungesema arudi miaka mingine mitano ili Kenya iende mbele. Ahsante sana, Mhe. Spika kwa muda ulionipa.
view
23 Sep 2021 in National Assembly:
Asante sana, Mhe. Naibu Spika, kwa kunipatia nafasi hii. Kwanza, nashukuru Mhe. Sankok kwa kuleta hii habari ya Laikipia katika hili Jumba. Hata ninapomshukuru, mambo ya Laikipia siyo ya leo wala jana. Mambo ya Laikipia yamekuwepo. Vita vimekuwepo. Mazungumzo ya Jumba hili hayatatatua shida hiyo. Kile kitatatua jambo hili ni watu kukaa chini na kujua shida ya Laikipia kwa sababu unaweza kufikiria ni jamii mbili tu ndizo zinasikia uchungu; Pokot na Samburu. Hii ni kwa sababu gani? Kila kabila la Kenya liko Laikipia, lakini shida ambayo iko Laikipia ni shida ya kawaida. Kila mara ikiwa imebaki mwaka moja kabla ya ...
view
23 Sep 2021 in National Assembly:
hilo. Hakuna mtu pia anayefurahia ng’ombe ambao ni mali ya mtu kuuawa na abaki bila chochote. Hakuna mtu anafurahia kitendo hicho. Kwa hivyo, kila mtu ana shamba huko na watu wamenunua mashamba huko. Kama mtu amenunua ama amenyakua shamba ya Serikali hawezi kuenda na kusema: “Nimepeana shamba; kujeni basi mchukue ama mgawanyiwe.” Tunagawanyiwa na nani? Kwa hivyo, ikiwezekana, kama viongozi wa Laikipia, Samburu, Isiolo na Pokot, tunafaa kukaa chini sisi sote na kujua tatizo liko wapi na tulitatue, kwa mfano, kwa kukabiliana Serikali kama ndiyo inatuletea shida ya kupigana na bunduki na wakuje watuambie. Tunavyoongea hivi kama watu wa Samburu, ...
view
29 Jun 2021 in National Assembly:
Asante sana, Mhe. Spika. Nilikuwa nataka kumsaidia mama mwenzangu, Mheshimiwa wa Meru, kwa sababu…
view