Millicent Omanga

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 181 to 190 of 296.

  • 5 Nov 2019 in Senate: Waswahili husema kuwa kizuri chajiuza na kibaya chajitembeza. Kama Hoja hii ingekuwa nzuri, basi watu hawangetoa maoni yao wenyewe na wapige kura inavyostahili bila kushurutishwa na Kiongozi wa Wengi katika Seneti? Inaonekana kwamba kuwa kuna watu mahali wanaotaka Seneti ipige kura vile wanavyotaka, si vile itakavyommfaidi view
  • 5 Nov 2019 in Senate: Bw. Naibu Spika, tukikubali kuongezwa kwa kiwango cha Serikali kukopa, ina maana kuwa tunaua ugatuzi Kenya hii. Tunaua ugatuzi vipi? view
  • 5 Nov 2019 in Senate: Bw. Naibu Spika, nina huzuni sana kwamba mwezi uliyopita tumekuwa kwenye vuta nikuvute na Bunge la Kitaifa kwa sababu ya mgao wa pesa unaoenda kwenye kaunti. Tukikubalia Serikali uwezekano wa kuchukua madeni zaidi, mwaka unaokuja, tutapata pesa chache katika kaunti. Mwaka mwingine na mtondoo na mtondogoo pesa chache muno zitapelekwa mashinani. Bw. Naibu Spika, iwapo tutapitisha Hoja hii itamaanisha kwamba sisi hatutakuwa tunapigania ugatuzi na pesa nyingi ziende kwa kaunti zetu. view
  • 5 Nov 2019 in Senate: Siwezi kubali Seneta aiingie katikati yangu! Bw. Naibu Spika, kuipitisha Hoja hii ni kuuza nchi yetu. Tukikubali Serikali nafasi ya kukopa zaidi, inamaana kwamba tunaua ugatuzi. Iwapo kweli tunapigania ugatuzi na kusisitiza kuwa tunataka pesa nyingi ziende kwenye kaunti, halafu sasa tukisema kwamba Serikali iendelee kukopa na kaunti ziendelee kupata mgao wa pesa wa chini zaidi ya ile tumekuwa tukipigania juzi, tunamaanisha kuwa sisi si wakweli. Bw. Naibu Spika, ukimtazama Mwenyekiti alipokuwa akiwasilisha Hoja hii, alikuwa anaongea polepole sana. Hii ni kwa sababu tulikuwa na yeye kwenye Kamati, na ilikuwa kana kwamba hata yeye mwenyewe haamini anachokisema. Hii ni kwa ... view
  • 5 Nov 2019 in Senate: The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view
  • 5 Nov 2019 in Senate: Nimekuelewa, Bw. Naibu Spika. view
  • 5 Nov 2019 in Senate: Nimesikia, Bw. Naibu Spika. Ni kwa sababu tulipokuwa kwenye Kamati hiyo pamoja na Waziri, idara yake ya wataalamu wa maswala ya kifedha, sote tuliukataa msimamo wake. Lakini tulipotoka kule na kuenda kuandika ripoti kesho yake, wengine walibadili mawazo yao. Sikuelewa walibadili mawazo yao vipi kutoka wakati tulipokuwa nao tukielezwa, na keshoye wakati wa kuandika ripoti. Haiwezekani kuwa Serikali inakopa ili kulipa madeni mengine. Hii ni kumaanisha kuwa tunachimba shimo ambalo halina mwisho. Kusema ukweli, hii itakuwa na madhara hata kwa watoto wetu na watoto wa watoto wetu watakaokuja baadaye. Bw. Naibu Spika, napinga Hoja hii. view
  • 15 Oct 2019 in Senate: On a point of order, Mr. Deputy Speaker, Sir. view
  • 15 Oct 2019 in Senate: Thank you, Mr. Deputy Speaker, Sir. I am sorry to interrupt my Chairman. I would like to draw your attention to the fact that there is no one listening to what the Chairman of CPAIC is moving in this House. view
  • 15 Oct 2019 in Senate: Mr. Deputy Speaker, Sir, no one is listening; they are talking to each other in pairs. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus