Hon Mishi Juma Khamisi

Mishi actively participated in Likoni political campaigns in 1997 and 2002. She vied for Likoni parliamentary seat in 2007 and lost in party nominations which were marred by irregularities. She would like to see government funded drug rehabilitation centres established in Mombasa.

All parliamentary appearances

Entries 181 to 190 of 404.

  • 3 Jul 2019 in National Assembly: ya ugatuzi sioni ni kwa nini Mawaziri wake waitwe Seneti kuzungumzia mambo ambayo ni ya kitaifa na si ya ugatuzi. Lazima tujue mipaka yetu ni ipi. Hapa hakuna cha Bunge kubwa wala Bunge ndogo. Hapa ni, Katiba inasema nini, imetupatia nguvu gani, imetupatia majukumu gani na mipaka yetu itakuwa gani? view
  • 2 May 2019 in National Assembly: Mhe. Mwenyekiti wa Muda, biashara ya kamari inafaida watu wengi sana. Pia, ina hasara kwa Wakenya wengi sana mpaka watoto wetu. Majumba mengi yameadhirika kwa sababu ya biashara ya kamari. Hii Kshs20 milioni ni sawa. view
  • 25 Apr 2019 in National Assembly: Ahsante sana, Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi hii ili niweze kupongeza Hotuba ya Mheshimiwa Rais. Hotuba yake ilikuwa Hotuba ya kizalendo na ya kujenga taifa la Kenya. Aliongea juu ya maendeleo ya kimsingi ya taifa letu. Wakati alizungumzia mambo ya umoja kupitia kile tunaita “ handshake” alisema ni jambo ambalo hatarudi nyuma ila atalizingatia sana. Sisi kama Wakenya, tumeona umuhimu wa view
  • 25 Apr 2019 in National Assembly: kwa sababu tumeona amani na upendo katika taifa letu. Pia, tumeona sekta nyingi zikistawi. Vile vile, Rais alizungumzia mambo ya ugatuzi na akasema hatarudi nyuma. Ni jukumu letu kama viongozi haswa Bunge la Seneti, liwe chonjo kujua pesa ambazo zimetolewa katika ugatuzi zitamfaidi Mkenya. Kama Wakenya, tuweze kufanya kile tunaita kwa Kiingereza, socialaudit, ili tuweze kujua faida ambayo tunapata katika mambo ya ugatuzi. Vile vile, ningependa kuzungumzia wajibu wa kitaifa katika mambo yakiulimwengu. Kwa Kiiingereza, tunasema international obligations . Ninajua taifa letu limeweza kuweka sahihi mikataba tofauti tofauti, ikiwemo ule mkataba wa African Free Trade Area Agreements ambayo itatuwezesha kupata ... view
  • 25 Apr 2019 in National Assembly: suala lile. Postmortem ilifanyika pasipo daktari wetu wowote wa Kenya kuweza kuhusishwa kama shahidi. Wakati mwili ulifika Kenya, tulisema tupate pathologist wetu wa Kenya ndio afanye view
  • 25 Apr 2019 in National Assembly: . Tulishtuka tulipopata kuwa viungo vyote vyake vya ndani mpaka ubongo vilikuwa vimeondolewa. Tulipouliza kwa wizara, tuliambiwa ni sheria ya Cuba, kuwa, wakifanya view
  • 25 Apr 2019 in National Assembly: , viungo hutolewa na kuhifadhiwa. Serikali ilipotuma delegation kwenda Cuba, kuuliza kuhusu viungo hivyo, walisema walivichoma. Hili ni jambo ambalo limeumiza familia kwa sababu tuna maadili yetu kama Wakenya na kama Waafrika. Iwapo postmortem ilifanyika na wakatoa viungo, kwa uchache wa elimu yangu, ninajua hata hapa Kenya, wakati wa postmortem, si viungo vyote hutolewa? Hukatwa hata sehemu ndogo ndogo ili waangalie sababu ya kifo cha mwendazake. Kwa hivyo, jambo kama hili lilitutamautisha sana. Wakati tunaweka mikakati kama hiyo, lazima tujue, sisi kama Wakenya, tukiwa nchi za nje, tuna sheria zetu, tuna maadili yetu na tuna mambo yetu ambayo ni lazima ... view
  • 25 Apr 2019 in National Assembly: na kutakuwa na viwanda tofauti tofauti kama vile vya nguo za EPZ na viwanda vya ngozi. Viwanda kama hivyo vitaleta ajira nyingi kwa watoto wetu, haswa kwa vijana wetu. Mheshimiwa Rais alisema kutakuwa na Mswada unaoitwa Sovereign Wealth Funds Bill ambao utazungumzia yale mapato kutoka rasilmali zetu kama mafuta, gasi na madini. Tuna madini mengi sana kule Kwale na mafuta kule Turkana. Cha msingi, lazima tuangalie wakaazi na wenyeji wataweza kufaidika vipi na madini na rasilmali zile kupitia Mswada huu ambao utaletwa. Katika jambo la usalama, ninataka turejeshe zile programmes za NYS ili tuweze kuwapatia vijana wengi ajira. Vijana wengi ... view
  • 21 Nov 2018 in National Assembly: Asante sana, Mhe. Naibu Spika. Nashukuru kwa kupata nafasi hii ili nizungumze kwa lugha ya kitaifa inayojulikana na Wakenya wengi hususan akina mama. Namshukuru Mhe. Duale pamoja na vinara wa Taifa la Kenya, Rais Uhuru Muigai Kenyatta, Mhe. Raila, Mhe. Ruto, Mhe. Mudavadi, Mhe. Kalonzo na wale wengine kwa sababu leo ni siku ambayo sisi kama Wabunge wa Taifa la Kenya, tutaandika historia na iingie katika kumbukumbu ya kwamba tumeheshimu Katiba yetu kwa kutekeleza matakwa yake. Ukisoma Katiba, kuna vipengele kadhaa na ibara tofauti tofauti ambazo ni wajibu wetu kama Wabunge tuzitekeleze sheria zake. Vifungu 27(3), 27(6), 27(8) vyote vinazungumuzia ... view
  • 21 Nov 2018 in National Assembly: tumekuwa na usawa wa jinsia na pia tutahakikisha kwamba akina mama wameweza kujengwa uwezo ili wapate afueni waweze kushindana sawia katika ulingo wa kisiasa, kiuchumi na hata kijamii. Sisi kama Wakenya katika Afrika Mashariki ni kama wale kaka wakubwa. Kwa lugha ya kiingereza “ the big brothers” . Ikiwa sisi ndio wakubwa, ni lazima tuonyeshe mifano bora katika uongozi na katika kuhakikisha kwamba tumeweka usawa wa kijinsia. Tukiangalia jirani yetu, Rwanda, wametupita kwa asilimia 56, Uganda asilimia 35 na Tanzania asilimia 36. Hata hapa jirani Ethiopia, juzi tu wamepata Rais mwanamke na pia jaji mkuu ni mwanamke. Haya yote ni ... view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus