Hon Mishi Juma Khamisi

Mishi actively participated in Likoni political campaigns in 1997 and 2002. She vied for Likoni parliamentary seat in 2007 and lost in party nominations which were marred by irregularities. She would like to see government funded drug rehabilitation centres established in Mombasa.

All parliamentary appearances

Entries 331 to 340 of 404.

  • 30 Jul 2015 in National Assembly: Jambo la usalama ni muhimu sana. Hapa Kenya, bali na kuwa na mambo ya usalama, tumekuwa na utesi mdogo mdogo, kwa mfano, katika mipaka yetu. Mpaka wetu na Uganda pale Malaba, pale Busia and mpaka wetu na Tanzania pale Horohoro, kumekuwa na matatizo madogo madogo. Watu wamekuwa wakitumia njia za kando kuingia Uganda na Tanzania. Hayo ni mambo ambayo yamekuwa yakileta tetesi. Tunapokuwa na mkataba na ushirikiana kama huu, mambo kama hayo hayatakuwa maswala nyeti ama maswala magumu. Yatakuwa ni maswala ambayo yanaweza kurekebishwa kwa pamoja. Katika Mkataba kama huu, kutakuwa na kamati ya pamoja ambayo italeta maofisa kutoka nchi ... view
  • 30 Jul 2015 in National Assembly: . Iwapo tungekuwa na ushirikiano kama huu wa kidete, pengine maafa kama yale yangepungua. Yangekuwa machache. Hakungekuwa na haja ya kuanza mikataba mingine, kusema ni lazima tuwe na stakabadhi fulani, tupatiwe ruhusa na nchi fulani na zile sheria nyingi sana ambazo ziko katika mambo ya kitaifa ya usalama. Tungeingia pale kwa haraka na kuwasaidia ndugu zetu. Tuliwasaidia wakati ule, lakini hatukuwa na makubaliano kama haya ambayo kwa lugha ya Kiingereza wamesema ni mutual benefits kutoka kwa majeshi yetu. Hii ni kusema kuwa sote tutakuwa katika hali ya usawa katika ushirikiano wetu. Hakutakuwa na nchi ambayo itakuwa mbele zaidi au nchi ... view
  • 30 Jul 2015 in National Assembly: Ahsante sana Mhe. Spika Naibu wa Muda. Naichukua nafasi hii kuunga mkono Hoja hii ambayo inazungumzia Karatasi No. 3 ya Mwaka 2013 ambayo inazungumzia sera za kuwezesha uzalishaji wa kitaifa. Inazungumzia kuhusu uzalishaji katika kuleta bidhaa ambazo zina bei na pia kuleta huduma njema katika nchi yetu ya Kenya. Hapo nyuma, nchi yetu ya Kenya ilikuwa katika daraja moja na nchi kama Korea na Malaysia. Hivi sasa, nchi hizi zimechukua hatua kubwa sana katika uzalishaji. Zimekuwa zikizalisha bidhaa zenye dhamani na pia kuweka huduma bora sana katika ulimwengu. Hiyvo basi, tutakapoweza kuratibisha Karatasi hii na kuleta Mswada tutaweza, hata sisi ... view
  • 30 Jul 2015 in National Assembly: Vile vile, tunaona ya kwamba kama nchi, tumekuwa na changamoto kadhaa katika kuboresha uzalishaji wa bidhaa na huduma katika nchi yetu. Changamoto ni kama kujua teknolojia na kuambatana na teknolojia ya kisasa. Tunaona kuwa nchi ambazo zimestawi kiuchumi zimeweza kuingia katika tekinolojia ya kisasa na kufanya uzalishaji katika mambo ya bidhaa na hata katika huduma. Ukitembea katika nchi kama China hivi sasa, utaona katika kijiji fulani pengine wana kiwanda cha kutengeza vibiriti, vijiko na vinginevyo. Hii yote ni kwa sababu wamekuwa na mikakati na wamekuwa na sera mwafaka ambazo zimekuwa katika kila sekta katika nchi yao. Tukiiga hayo, tutaona ya ... view
  • 28 Jul 2015 in National Assembly: Ahsante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipa nafasi kutathmini Ziara ya Rais wa Marekani, Obama. Kwanza kabisa, natoa pongezi kwa Serikali ya Kenya ikiongozwa na Mhe. Uhuru pamoja na Serikali ya Marekani kwa kufanikisha ziara hiyo. Ziara hiyo ilikuwa ya kihistoria. Kwanza kabisa, Obama ni Rais wa Marekani wa kwanza kuja Kenya. Rais Obama pia ana asili ya Kenya kwa sababu ana mizizi yake Kogelo. Pia, tunatoa pongezi kwa Rais Obama kwa sababu anajua “mwacha asili ni mtumwa.” Hajaacha asili yake. Ningependa kutoa pongezi kwa Rais Obama kwa kuzungumzia uimarishaji wa uwezo wa kiuchumi wa akina mama na ... view
  • 28 Jul 2015 in National Assembly: mtoto wa Nairobi kwa kupata haki za elimu. Pia, akazungumzia ukosefu wa usawa kati ya mtoto wa eneo la kati na mtoto wa Nyanza kwa kupata huduma za afya. Jambo hili sio jambo la uchochezi. Ni jambo ambalo sisi kama viongozi wa nchi lazima tulitathmini na tuhakikishe ya kwamba yale mapengo ambayo yaliwekwa kuanzia utawala wa ukoloni ambayo yalichangia sehemu fulani kuendelea kimiundo msingi, kiafya na kielemu, sasa tuendeleze sehemu ambazo zina umaskini na sehemu ambazo hazijawahi kustawi kimaisha na kiuchumi ili ziwe sawa na sehemu zingine za Kenya. Rais Obama alitambua mashirika yasiyo ya kiserikali na akakuwa na kongamano ... view
  • 28 Jul 2015 in National Assembly: Pia nataka kusema kwamba Mheshimiwa Rais Obama hakuweza kuwasahau viongozi wa upinzani. Alijua katika demokrasia kuna Serikari na pia kuna uongozi wa upinzani. Aliwapatia masikio yake na wakakaa chini na kujadili--- view
  • 29 Apr 2015 in National Assembly: Ahsante sana Naibu Spika kwa kunipatia nafasi hii kuunga mkono Mswada huu. Kwanza napenda kumpa kongole mhe Wangwe kwa sababu ya kuleta Mswada huu. Katika nchi yetu tunaelewa kwamba jambo lolote likifanywa kisheria, linaweza kutekelezwa, na hivyo basi kuona limetendeka kwa njia inayofaa. Ni haki ya kimsingi kwa kila mtoto wa Kenya kupata elimu yenye manufaa. Jambo hili limesisitizwa katika Kifungu 42 cha Katiba yetu. Elimu yenye manufaa ni elimu ambayo mwanafunzi amesoma na baada ya kusoma ameweza kutahiniwa na baadaye kuweza kuendelea katika daraja ya pili ya kielimu. Kwa mfano, watoto wetu wengi sana hapa Kenya huweza kusoma katika ... view
  • 1 Apr 2015 in National Assembly: Asante sana mhe. Naibu Spika wa Muda. Mimi pia nasimama hapa kama wabunge wenzangu walivyofanya ili kuzungumzia Hotuba ya Mhe. Rais ambayo aliitoa katika Bunge hili letu la Kumi na Moja. Mimi nataka kuzungumza kama kiongozi na kiongozi huzungumzia mazuri na pia yale yenye udhaifu. Kwanza, nataka kusema kwamba, wakati Mhe. Rais alipozungumza na kuomba msama juu ya matukio ambayo yamefanyika kupitia utawala wa wale viongozi wa wakati wa nyuma, The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor. view
  • 1 Apr 2015 in National Assembly: Asante sana mhe. Naibu Spika wa Muda. Mimi pia nasimama hapa kama wabunge wenzangu walivyofanya ili kuzungumzia Hotuba ya Mhe. Rais ambayo aliitoa katika Bunge hili letu la Kumi na Moja. Mimi nataka kuzungumza kama kiongozi na kiongozi huzungumzia mazuri na pia yale yenye udhaifu. Kwanza, nataka kusema kwamba, wakati Mhe. Rais alipozungumza na kuomba msama juu ya matukio ambayo yamefanyika kupitia utawala wa wale viongozi wa wakati wa nyuma, The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus