Mishi actively participated in Likoni political campaigns in 1997 and 2002. She vied for Likoni parliamentary seat in 2007 and lost in party nominations which were marred by irregularities. She would like to see government funded drug rehabilitation centres established in Mombasa.
1 Apr 2015 in National Assembly:
aliomba msamaha na pia akataja tukio moja la mauaji ya Wagalla. Nataka kusema kuwa, Mhe. Rais, katika jambo hili msamaha huu uweze kupatikana kwa njia ya usawa na uweze kuwa ni msamaha kweli ambao umelenga wananchi wa Kenya. Mhe. Rais, ningekuomba kwa unyenyekevu uweze kuhimiza utekelezaji wa Ripoti ya TJRC ambayo inazungumzia ukweli, haki na maridhiano. Mhe. Rais, katika Ripoti hii, kumezungumziwa mambo mengi sana kuhusu haki nyingi sana za kimsingi kwa sababu wakenya wengi wamekuwa wakinyanyaswa. Mbali na Wagalla, pia imezungumzia Molo. Molo kulikuwa na vita vingi vya kikabila. Pia imezungumzia Pwani ambako kulikuwa na vita vya kikabila vya ...
view
1 Apr 2015 in National Assembly:
aliomba msamaha na pia akataja tukio moja la mauaji ya Wagalla. Nataka kusema kuwa, Mhe. Rais, katika jambo hili msamaha huu uweze kupatikana kwa njia ya usawa na uweze kuwa ni msamaha kweli ambao umelenga wananchi wa Kenya. Mhe. Rais, ningekuomba kwa unyenyekevu uweze kuhimiza utekelezaji wa Ripoti ya TJRC ambayo inazungumzia ukweli, haki na maridhiano. Mhe. Rais, katika Ripoti hii, kumezungumziwa mambo mengi sana kuhusu haki nyingi sana za kimsingi kwa sababu wakenya wengi wamekuwa wakinyanyaswa. Mbali na Wagalla, pia imezungumzia Molo. Molo kulikuwa na vita vingi vya kikabila. Pia imezungumzia Pwani ambako kulikuwa na vita vya kikabila vya ...
view
25 Mar 2015 in National Assembly:
Asante sana, Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda. Nasimama kuunga mkono Hoja hii iliyoletwa ni dadangu Mheshimiwa Joyce Lay. Kwanza nataka kusema ikiwa Kiswahili ni lugha rasmi na ya kitaifa ni lazima tuitukuze na kuienzi kwa mahaba kama tunavyoipenda lugha ya Kiingereza ambayo tuliletewa na wakoloni. Nataka kusema kuwa Katiba yetu ya sasa ni sheria mama na ndiyo inasimamia utawala wa nchi yetu. Vipi Katiba hii itakuwa haijatafsiriwa kwa Kiswahili? Hili ni suala ambalo lazima sisi watungasheria katika Bunge hili tunafaa tuliangalie kwa undani sana. Katika utekelezaji wa sheria, lazima washikadau husika wahusishwe katika mambo ya sheria.
view
25 Mar 2015 in National Assembly:
Kwa mfano, mshikadau ambaye ni mahakama; ambayo inatoa hukumu kwa wale ambao wamekiuka sheria, ni lazima aelewe sheria hii. Wenye kutunga sheria, kama sisi Wabunge katika Bunge hili, ni lazima tuzielewe sheria ili tuweze kufanya utekelezaji. Pia The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor.
view
25 Mar 2015 in National Assembly:
Wakenya ni lazima wazielewe sheria hizo kinaga ubaga ili waweze kuzifuata na kuepuka kufanya maovu, kinyume na sheria hizo.
view
25 Mar 2015 in National Assembly:
Mhe. Naibu Spika wa Muda, katika barabara zetu hapa Kenya tunaona kwamba kuna sheria ambazo zimewekwa. Kwenye kibao, utaona kumeandikwa “Keep Left” kwa Kiingereza ama “Keep Right”. Kwa Mkenya ambaye hajui lugha ya Kiingereza, huoni kwamba anaweza kufanya ajali kwa sababu ya kutoijua lugha iliyotumiwa kwenye alama ile? Akina mama wengi na mabanti wetu wadogo, ambao wanabakwa, wanaelewa Kiswahili. Wanapokwenda kwenye afisi za wahusika wa kisheria kuandikisha taarifa kuhusu dhuluma ambayo wamefanyiwa, wengi wao hawawezi kuandikisha taarifa kwa Kiingereza. Hivyo basi, mhasiriwa anapoandikisha taarifa yake kwa Kiswahili, afisa wa polisi anamwambia: “Dada, ninaweza kukutafsiria taarifa hii kwa lugha ya Kiingereza.” ...
view
26 Nov 2014 in National Assembly:
Thank you, hon. Temporary Deputy Chairman. I stand here to withdraw my amendments to the Alcoholic Drinks Control (Amendment) Bill. I am withdrawing because I have done a lot of consultations with the experts from this National Assembly and even with National Authority for Campaign against Alcohol and Drug Abuse (NACADA). I have even looked at the Bill and I have seen that it has just talked about alcoholism and it has not mentioned anything about hard drug abuse. That is why I think my amendment will not be relevant. I am still doing some consultations and I am going ...
view
26 Nov 2014 in National Assembly:
Thank you, hon. Temporary Deputy Chairman. I also withdraw the second amendment because it is just the same. It does not have anything to do with the abuse of hard drugs. I am coming with a comprehensive Bill which will have all those amendments.
view
26 Nov 2014 in National Assembly:
Thank you, hon. Temporary Deputy Chairman. I withdraw.
view
25 Nov 2014 in National Assembly:
Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipatia nafasi hii. Nataka kutoa risala zangu za rambirambi kwa ndugu zetu wa Mandera, Kapedo na Mombasa kwa sababu ya kuuawa katika njia tatanishi za kupitia hawa AlShabaab . Wakati huu si wakati wa kutoa tu matatizo. Ni wakati wa kuuliza: Ni njia gani mwafaka itatusaidia ili Kenya yetu iwe na usalama? Ingekuwa sawa kwanza tujizatiti katika kulinda mipaka yetu. Lazima kuna ulegevu katika kulinda mipaka yetu. Juzi katika Jimbo la Mombasa, tuliona katika Masjid Musa na Masjid Mina kumepatikana gruneti, bastola na silaha zingine. Silaha hizi zinaingia kutoka wapi na kupitia ...
view