Hon Mishi Juma Khamisi

Mishi actively participated in Likoni political campaigns in 1997 and 2002. She vied for Likoni parliamentary seat in 2007 and lost in party nominations which were marred by irregularities. She would like to see government funded drug rehabilitation centres established in Mombasa.

All parliamentary appearances

Entries 351 to 360 of 404.

  • 19 Nov 2014 in National Assembly: Thank you hon. Speaker Sir. I also want to join my colleagues in passing my sincere condolences to the people and the family of hon. Otieno Kajwang’. I want to say I knew hon. Otieno Kajwang’ when I was a youth in the LDP Party and he used to call me Nyamombasa . Hon. Otieno Kajwang’ was a remarkable person who spoke clearly and stood firmly with two principles; the principle of democracy and the rule of law. He fought so many battles, be it arguments, conflicts and even division. He never shied away from any kind of fight. The ... view
  • 16 Jul 2014 in National Assembly: Ahsante sana Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi hii. Kwanza, ningependa kumshukuru dada yangu, mhe. Millie Odhiambo kwa kutuletea Mswada huu ambao unazungumzia maswala nyeti na muhimu sana yakusaidia waathiriwa katika jamii yetu. Mswada huu unasema kwamba waathiriwa watatoa habari ambazo zitawasaidia ili wapate huduma na fidia kutoka kwa wale ambao wamewaathiri. view
  • 16 Jul 2014 in National Assembly: Sura ya Pili, Aya ya Tatu inazungumzia mambo yamaridhiano katika kesi fulani na pia, katika kuleta amani. Tukiangalia katika nchi ya Rwanda, tunaona kwamba kitambo walikuwa na vita vya kikabila lakini kwasababu ya maridhiano baina ya zile jamii mbili tunaona hii nchi ikiwa na amani na umoja. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor. view
  • 16 Jul 2014 in National Assembly: Kwa hivyo, Mswada huu utaangalia mambo ya maridhiano kwa sababu kesi nyingine huwa ni kesi ambazo mwathiriwa na mwathiri wanapowekwa pamoja na jamii na familia huwa kunapatikana amani ya kudumu na haki itakayowaridhisha wote wawili. view
  • 16 Jul 2014 in National Assembly: Pia, Mswada huu unazungumzia ushirikiano baina ya vitengo vya Serikali vinavyoangalia mambo ya waathiriwa kutokana na majanga ya uhalifu. Kwa mfano, kuna kitengo cha polisi na kitengo cha mahakama. Mara nyingi watoto wetu ambao wameathiriwa kwa sababu ya kubakwa ama kwa kufanyiwa mambo machafu na mabaya kama vile ya ngono huwa wanakosa kupata haki kwasababu vitengo hivi havina ushirikiano dhabiti. Unapata polisi katika uchunguzi wao na ushahidi unakuwa na utata na mahakama inapata ripoti ambayo haitaweza kumsaidia mtoto yule. Lakini wakati vitengo hivi vitakuwa na ushirikiano dhabiti basi mtoto huyu atapata haki yake na anapopata haki, basi hata sisi Wakenya ... view
  • 16 Jul 2014 in National Assembly: Vile vile, Mswada huu umezungumzia maadili ambayo yako katika Katiba yetu. Mswada huu unasema kwamba waathiriwa wasibaguliwe kwa misingi ya kikabila, kijinsia, dini au umri. Hivyo basi tunasema Mswada huu umezingatia Katiba yetu ambayo inatupatia haki, nasisi Wakenya tunasema “haki iwe ngao na msingi wetu”. view
  • 16 Jul 2014 in National Assembly: Sisi kama viongozi, tunaiomba Serikali izingatie mambo yaliyozungumziwa katika Mswada huu, kwa mfano, mambo yamaridhiano. Kwa hivyo, ripoti ya TJRC ambayo inaongea juu ya ukweli, haki na maridhiano inafaa itekelezwe ili tusiwe na matukio ya vita vya kijamii kama vile vilitokea kule kwetu Pwani, Kaya Bombo na Molo. Mambo haya hutokea kwasababu hatuna miundomisingi au mikakati ambayo inaweza kuzuia mambo kama haya kuweza kutokea tena. view
  • 16 Jul 2014 in National Assembly: Ninaunga mkono huu Mswada kwa kusema tutakuwa na hazina itakayoitwa “Victim Protection Trust Fund”. Hazina hii, pia, itaweza kumsaidia yule mwathiri aweze kupata huduma zitakazo mwezesha kupata haki. Nikiangalia katika Mswada huu, ninaona kwamba huduma zimezungumziwa kwa utaratibu unaofaa. Hakika tukifuata mtiririko wa huduma hizi basi haki itakuwa ngao na msingi wetu kama Wakenya. view
  • 16 Jul 2014 in National Assembly: Mhe. Naibu Spika wa Muda, jambo lingine ambalo ninaunga mkono na ninatoa kongole sana kwa mhe. Millie linahusu kuweka mtoto katika hali ya usalama wakati ameathirika. Tumeona mifano katika nchi yetu. Unapata baba wa kambo anambaka mtoto wa mkewe. Wakati anatenda kitendo hiki, anaenda mahakamani, anapewa bond na anatoka nje. Akiwa nje na akina mama ni sisi, wengine tunawapenda waume wetu, unaona kwamba huwezi kuwa kando na mme wako. Unaendelea kuishi na mme wako na mtoto huyu anapolegeshwa katika familia kuishi na mama na baba wakambo aliyembaka, hawezi kupata haki. Huyo mtoto ataendelea kuathiriwa zaidi na mambo mengine. Basi ikiwa ... view
  • 16 Jul 2014 in National Assembly: Pia, Sura ya Nne, Aya 13 inazungumzia wale ambao ni walemavu katika kupata haki zao. Inasema kuwa miundomisingi lazima iwawezeshe walemavu ambao wameathiriwa kupata haki yao. Tunaona katika mahakama zetu mwathiriwa ambaye ni mlemavu anashindwa kufika katika kizimbani ama kuingia katika mahakama na hii ni kwasababu ya vile imejengwa, miundo misingi yake haikuzingatiwa. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus