Hon Mishi Juma Khamisi

Mishi actively participated in Likoni political campaigns in 1997 and 2002. She vied for Likoni parliamentary seat in 2007 and lost in party nominations which were marred by irregularities. She would like to see government funded drug rehabilitation centres established in Mombasa.

All parliamentary appearances

Entries 361 to 370 of 404.

  • 16 Jul 2014 in National Assembly: Pia, kuna mambo mengi sana ya wale watu ambao wana ulemavu. Uhalifu unaofanyiwa mtu aliye sawa kimaumbile na ule unaofanyiwa mtu ambaye ni mlemavu ni The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor. view
  • 16 Jul 2014 in National Assembly: tofauti. Ninaona Mswada huu pia umewazingatia hao ndugu zetu. Hivyo basi tunasema kwamba huu ni Mswada ambao lazima tuupigie debe sisi kama Wakenya na sisi kama viongozi katika Bunge hili la Kumi na Moja ili haki itendeke. view
  • 16 Jul 2014 in National Assembly: Tumeona wengi wameuwawa kwa njia hii. Kwa lugha ya Kiingereza tunasema “ mob justice ”. Unaweza kuwa na chuki na mtu fulani, unapiga nduru na kusema huyu mtu ni mwizi ama huyu mtu amefanya jambo fulani. Huyo mtu anauwawa na tunakosa haki kwa watu kama hao. view
  • 16 Jul 2014 in National Assembly: Jambo la mwisho ambalo ninatoa kongole kwasababu limenifurahisha sana katika Mswada huu ni lile la kuzungumza katika lugha ambayo utaielewa ama lugha ambayo umeichagua. Tunafahamu kwamba lugha za taifa ni mbili, nazo ni lugha ya Kiingereza na lugha ya Kiswahili lakini unapata watoto na akina mama wengi katika mashinani wanapenda kuzungumza katika lugha yao. Hii pengine ni lugha yake ya Kikuyu, Kidigo au Kiluhya ili aweze kuzungumzia yale mambo ambayo yamemvika yeye kama Mkenya. Hivyo basi kukiwa na mkalimani, tunaweza kusikia yaliyojili katika mikasa kama hiyo. view
  • 16 Jul 2014 in National Assembly: Mhe. Naibu Spika wa Muda, ninashukuru sana na ninaunga mkono Mswada huu. Ninatoa kongole kwa mhe. Millie. view
  • 30 Apr 2014 in National Assembly: Thank you, hon. Temporary Deputy Speaker. I stand to support the Bill by hon. Wamunyinyi. I support this Bill because it will establish bodies to administer examinations to ensure persons who have trained are qualified for registration. We have been having so many fake counselors who purport to give services, yet they cannot give the service to the required standards. I am also supporting this Bill because it is going to regulate the charges set by the counselors. Most times when you go for such services you are charged very high fees or, sometimes, very low fees. We do not ... view
  • 3 Apr 2014 in National Assembly: Asante sana, Bw. Naibu Spika wa Muda. Nasimama kuzungumzia Hotuba ya Rais wetu. view
  • 3 Apr 2014 in National Assembly: Bw. Naibu Spika wa Muda, nachukua nafasi hii hata mimi kuzungumzia Hotuba iliyotolewa na Rais. Ningependa kuzungumzia vipengele kadhaa ambavyo alivizungumzia katika Hotuba yake. Kwanza kabisa nataka kupongeza habari za kawi ambazo amezungumzia, kwamba tutaweza kuwa na megawatts 5,000 ambazo zitatuwezesha kupata umeme kwa asimilia 80 ya jamii. Swala la umeme limetupa shida sana kama Wakenya. Tumekuwa tukipimiwa umeme na kuukosa katika nyakati nyingi. Hivyo basi, Wizara husika inahitajika kueneza huu mradi vilivyo. Jambo la pili ningezungumzia swala la usalama ambao kwa sasa katika nchi yetu umedorora sana. Ni swala ambalo Serikali, na zile Wizara husika, inatakikana iangalie kwa upeo ... view
  • 27 Nov 2013 in National Assembly: Ahsante Bi. Naibu Spika wa Muda. Nasimama kuunga mkono Mswada huu. Huu Mswada umekuja wakati unaofaa; wakati ambapo Wakenya tunasherehekea miaka 50 tangu tujikomboe kutoka kwenye minyororo ya wabeberu na kuweza kujitawala kama Wakenya. Mswada huu unatambua na kuteua mashujaa. Wakenya tumekuwa na fikira kwamba mashujaa wa ukombozi wa uhuru wametoka katika jamii fulani ama sehemu fulani humu nchini. Lakini mashujaa wetu wa uhuru wametoka katika Jamhuri yetu yote ya Kenya. Kwa mfano, kule kwetu pwani tunaye mama yetu Mekatilili wa Menza. Yeye alikuwa shujaa ambaye alitembea kilomita 1,200 kwenda na kurudi ili kuwatetea wakenya dhidi ya dhuluma za wabeberu. ... view
  • 27 Nov 2013 in National Assembly: Kuna wale pia watakuwa wameleta maadili fulani katika nchi yetu. Huu Mswada kwa kweli umezungumzia nani ndiye shujaa. Tumekuwa tukifikiria kwamba ushujaa ni wa wale waliopigania uhuru peke yao. Hata hivyo, tunaona kwamba mashujaa wako katika nyanja nyingi sana. Tuna mashujaa hata katika mambo ya elimu. Tuna waalimu na maprofesa ambao wamevumbua hali nyingi. Mfano ni maprofesa wa hesabu ambao wamevumbua formula za kutatua matatizo yetu katika nyanja ya hesabu. Vile vile, tuna mashujaa katika soka. Wengi pale mashinani wamesahaulika. Tunawataja sana wanasoka wa nchi za nje na tunawasahau wetu. Mswada huu ukipitishwa tutakuwa na miundo misingi wa kuwatambua mashujaa ... view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus