Hon Mishi Juma Khamisi

Mishi actively participated in Likoni political campaigns in 1997 and 2002. She vied for Likoni parliamentary seat in 2007 and lost in party nominations which were marred by irregularities. She would like to see government funded drug rehabilitation centres established in Mombasa.

All parliamentary appearances

Entries 371 to 380 of 404.

  • 27 Nov 2013 in National Assembly: Nafurahishwa sana pia na Mswada huu kwa sababu umezungumzia kuhusishwa kwa Wakenya ama jamii katika kutambua mashujaa. Itakuwa vyema zaidi wakati baraza litaundwa ili kuhusisha Wakenya kule mashinani ambao pengine wana historia kuhusu mambo yaliyotokea tulipokuwa tunapigania uhuru wetu. Tunajua pia kuna Wakenya waliochukuliwa wakati wa nyuma katika Vita Vikuu vya Dunia ama World War, ambao mpaka sasa hawatajwi na hawajulikani. Lakini ikiwa tutahusisha jamii kwa jumla katika jambo hili, itakuwa vizuri. Kwa hakika, wale wakongwe wetu kule mashinani wanaijua historia ya nchi yetu ya Kenya vizuri. Nashukuru sana kwa kunipatia nafasi hii. Nawaomba Wakenya wenzangu tuunge mkono Mswada huu ... view
  • 27 Nov 2013 in National Assembly: Kwa hayo mengi, nashukuru sana na naunga mkono Mswada huu. view
  • 27 Nov 2013 in National Assembly: Ahsante sana Bi. Naibu Spika wa Muda. Kwa hakika, hata ukiangalia maneno yaliyotoka katika kinywa changu, hauwezi kuwa umeandika maneno kama hayo. Nimeyazungumza yakitoka katika akili yangu. Nilikuwa nikiangalia tu kama ninataka kufanya reference ya kuonyesha kifungu fulani, ambayo inaruhusiwa kulingana na Kanuni za Bunge. Maneno kama hayo siwezi kuyaandika na kuweza kuyasoma. Huu ni mtiririko wa maneno ambayo yametoka katika kinywa changu na akili yangu. view
  • 14 Nov 2013 in National Assembly: Bw. Naibu Spika wa Muda, nimesimama kuupinga Mswada huu kwa sababu ingawaje ni Mswada mzuri, unatashiwishi. Waswahili wanasema hata unapopika mchuzi wako mzuri, unapoingia jongoo hauwezi kuwa mzuri. Kama Wakenya, tunatambua kwamba tumekuwa katika mapambano makali sana kuhakikisha kwamba kumekuwa na uhuru wa habari na kuvipatia vyombo vya habari uhuru na kupata uhuru wa kujieleza. Katiba yetu, katika Sura ya Nne, Vipengele 33, 34 na 35, inazungumzia jinsi tulivyopata uhuru wa kujieleza, uhuru wa vyombo vya habari na uhuru wa kupata habari katika nchi yetu. Kwenye Mswada huu, kuna Kipengele kinachosema kwamba kutakuwa na Tume itakayopokea malalamiko. Tume hiyo imepewa ... view
  • 14 Nov 2013 in National Assembly: Ahsante, Bw. Naibu Spika wa Muda. Nakushukuru sana kwa sababu hata sisi wengine tumekuwa tukijaribu sana kuzungumza katika Bunge hili lakini hatukupata nafasi. Nilikuwa nimeingiza kadi yangu alafu nikatoka nje. Sasa ndiyo nimerudi. view
  • 14 Nov 2013 in National Assembly: Jopo lililopendekezwa kwenya Mswada huu ili kuangalia nidhamu ya wanahabari ni jopo ambalo nguvu zake ni nyingi mno kiasi cha kwamba mwanahabari anaweza kupokonywa kibali cha kazi yake, na taasisi za uanahabari pia kupokonywa vibali vya kufanyia kazi na akaunti zao kwenye mabenki kufungwa na kuambiwa wasiendelee na kazi yao. Hili ni jambo ambalo halitaweza kukubalika. Cha msingi ni kuweza kuangalia na kupima uanahabari ulio na nidhamu na uanahabari usio na nidhamu na wenye kutumia nguvu. Naibu Spika wa Muda, pengine ningezungumza kwa Kingereza ili wenzangu ambao hawaelewi lugha sanifu ya Kiswahili, waweze kuelewa. We need to address media so ... view
  • 14 Nov 2013 in National Assembly: ni yeye ataliunda. Wakati jopo hili la kuangalia mambo ya utetezi litakuwa limepeleka mapendekezo yake kwa Waziri, basi Waziri anaweza kusema kwamba, mtu fulani ua mwandishi habari amekosea katika jambo hili. Lazima tujue tutokako ni mbali na tunakofika ni karibu. Iwapo tunataka kubaki pale karibu tulipo, na kulinda wanahabari; kuhakikisha Wakenya walalahoi wamepata haki zao za kimsingi ambazo ni Katiba iliowapa haki kama hizo, tuwache wanahabari wenyewe watengeze jopo lao ama baraza lao kuu la kuangalia haki za wanahabari. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained ... view
  • 14 Nov 2013 in National Assembly: Tunajua kwamba baraza hili, bila ya kuwa na hilo tume la malalamiko, lina nguvu zaidi. Mswada huu umezungumzia mambo mengi zaidi ambayo yameangazia vile watalinda wanahabari na vile watalinda nchi katika kuangazia habari. Kwa hayo mengi ama machache, ninapinga Mswada huu. Ikiwa Mswada huu utaendelea, basi Wabunge wenzangu, tuweze kuupiga msasa, tufanye marekebisho madogo madogo, ndipo tuweze kupata Mswada ambao utawapatia hadhi wanahabari na sisi tunaosikiza habari. Asante. view
  • 24 Jul 2013 in National Assembly: Hon. Deputy Speaker, I beg to give notice of the following Motion:- THAT, aware that over 300,000 children live and work in the streets in the country, with over 50 per cent of them concentrated in and around Nairobi; concerned that the number of street children is increasing rapidly owing to poverty and HIV/AIDS and collapsing of family structure; noting that street children are not only denied access to the mainstream social services, but also their basic needs; deeply concerned that these children also face police harassment and social molestation, this House resolves that the Government creates community and family ... view
  • 24 Jul 2013 in National Assembly: Ahsante sana mhe. Naibu Spika wa Muda. Nasimama kuiunga mkono hoja hii iliyoletwa na mhe. Francis Kige Njenga. Tunafahamu kwamba tunayo ruwaza ya 2030. Hivyo basi ili tuweze kufikia ruwaza hii ni lazima tuangalie taasisi zetu za kuwapa ujuzi watoto wetu. Serikali imeng’ang’ana kutuletea taasisi hizi vijijini. Taasisi hizi ni nyingi lakini ajabu ni kwamba vijana wetu bado hawajapata mafunzo. Hii ni kwa sababu ya umaskini. Wazazi wengi wanashindwa kulipa karo. Serikali hivi punde ilipunguza karo katika taasisi hizi za vijijini lakini bado katika takwimu zile zinaonekana, watoto wanaokwenda kupata masomo ni wachache sana na hii yote ni kwa sababu ... view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus