Mohamed Faki Mwinyihaji

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 1301 to 1310 of 1995.

  • 1 Dec 2020 in Senate: Thank you, Madam Deputy Speaker, Sir. I want to clarify that in this era of electronic gadgets, communication with the Senator may also be on WhatsApp or by message. Sen. Sakaja, look at the Constitution. view
  • 1 Dec 2020 in Senate: Asante Bi. Naibu Spika, kwa kunipa fursa hii kuchangia Taarifa iliyoletwa na Sen. Iman. Ni jambo la kusikitisha kwamba kwa sasa wakati tuna vifaa vyote vya kutambua uhai na kifo, mhusika alipelekwa kwa chumba cha kuhifadhia maiti kabla ya siku zake kufika. Tangu janga la COVID-19 kuanza, kuna wengi ambao wamepata visa kama hivi. Hii imesababishwa na ugonjwa wa COVID-19 ambao umeathiri hata madaktari. Madaktari wengi ambao wanatibu watu katika hospitali na zahanati ni vijana ambao The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard ... view
  • 1 Dec 2020 in Senate: wako na umri kati ya miaka 30 na 45. Kwa hivyo, hawana tajriba ya kutosha kuweza kutibu na kuangalia wagonjwa kama hao. Nikizungumzia Mombasa, nimewahi kuzuru hospitali kuu ya Coast General Hospital mara tatu kwa muda wa wiki mbili ili kusaidiana na watu waliofiwa, kuweza kuchukua miili zao. Ni jambo la kusikitisha kwamba unapopelekwa katika wadi ya COVID-19, huo unakuwa mwisho wa mawasiliano yako na jamii yako na huenda ukapoteza maisha bila ya kuwa karibu na jamii yako kuweza kukuombea dua ama kukuombea Mungu ili safari yako, unapokwenda, iwe ya salama. Bi. Naibu Spika, tunaona kwamba madaktari, bali na kuwa ... view
  • 1 Dec 2020 in Senate: On a point of order, Mr. Temporary Speaker, Sir. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view
  • 1 Dec 2020 in Senate: Mhe. Spika wa Muda, kwanza naipongeza Kamati kwa hiyo Ripoti yake, lakini masikitiko ni kwamba Kamati hii haijaangazia Taarifa yangu ambayo nilileta hapa Tarehe 24 Mwezi wa Tano mwaka huu kuhusiana na kuangushwa kwa ndege ya Kenya nchini Somalia. Ndege ile ilikuwa ya Shirika la African Express Airways ambayo ilipigwa ikiwa inatua katika uwanja mmoja nchini Somalia. Mwezi uliopita pia nilipewa fursa kuikumbusha Kamati hii kwamba hiyo Taarifa bado haijajibiwa na kwamba tunahitaji majibu kwa haraka kwa sababu kuna ripoti inayotakikana kutayarishwa na nchi ya Somalia ambamo ndege ilianguka. Ripoti ile itasaidia kulipwa ridhaa kwa wale waliohusika katika ajali ile ... view
  • 1 Dec 2020 in Senate: Asante, Bw. Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii kuunga mkono Ripoti ya Kamati ya Haki, Sheria na Haki za Kibinadamu katika Seneti. Kwanza naipongeza Kamati hii kwa kukaa kwa muda mchache na kuja na Ripoti ambayo ina ufasaha makubwa. Itakumbukwa kwamba Kamati hii ina Wakili Waandamizi watatu ambao ni Sen. Omogeni ambaye ni Mwenyekiti, Sen. Amos Wako ambaye alikuwa Mkuu wa Sheria na Sen. Orengo ambaye pia ni Senior Counsel. Vile vile, Kamati hii ina mawakili wengine watatu wakiwamo Sen. Dullo ambaye ni Deputy Majority Leader, Sen. Mutula Kilonzo Jnr. ambaye ni wakili mwenye tajiriba kubwa na Sen. Iringu ... view
  • 1 Dec 2020 in Senate: Bw. Spika wa Muda, Sen. Kang’ata ni wakili kama mimi. Mara nyingi wakati wakili senior wako anazungumza, wakili ambaye ni junior anafaa kuketi na kusikiza ili aweze kupata hekima ya mafunzo yanayotokana na wakili senior. Sitakuwa mrefu wa mazungumzo. Yangu ni kusema kwamba yale mapendekezo ambayo yalitolewa na Kamati ya Kudumu ya Haki, Mambo ya Kisheria na Haki za Binadamu ambayo yako katiki Ripoti hii yameangaziwa katika Mswada wa BBI ambao umechapishwa rasmi. Wananchi wanaweza kusoma Mswada wa BBI na kuweka sahihi ili kutimiza mapendekezo ya sheria kuhusiana na ruwaza hiyo. Hii itaenda kwenye kumbukumbu ya Seneti kuwa wakati tulipokuwa ... view
  • 1 Dec 2020 in Senate: tulitoa mchango wetu kuona kuwa Seneti inabaki kuwa chombo muhimu cha kulinda ugatuzi katika Jamhuri ya Kenya. Mapendekezo kuwa Nairobi iwe metropolitan ya mekataliwa. Nairobi itabaki kuwa kaunti kama kaunti zingine. Tunapongeza kazi ambayo inafanywa na Nairobi Metropolitan Services (NMS) lakini utawala lazima urudi kwa wananchi. Utawala unarudi kwa wananchi ili wakati wananchi wapate fursa ya kuchagua viongozi wanaowataka. Napongeza Mswada wa BBI kwa sababu ya kutupa Kaunti ya Mombasa maeneo Bunge tatu ili kuboresha utendakazi wa wabunge katika eneo lile. Naunga mkono Ripoti ya Kamati ya Kudumu ya Haki, Mambo ya Kisheria na Haki za Binadamu na naomba kwamba ... view
  • 1 Dec 2020 in Senate: Asante, Bw. Spika wa Muda. Mapendekezo yote na mijadala ambayo imetolewa na Maseneta katika kujadili Ripoti hii yatazingatiwa na Kamati. Tutaweza kuboresha utendakazi wa Kamati hii wakati tutakaporudi mwakani. Kama alivyosema Sen. (Dr.) Ochillo-Ayacko, kuna sheria nyingi ambazo zinatarijwa kufanyiwa ukarabati wakati BBI itakapopitishwa. Kamati itakuwa macho wakati wote kuweza kutekeleza. Asante, Bw. Naibu Spika wa Muda. view
  • 1 Dec 2020 in Senate: Asante, Bw. Spika wa Muda, kwa kunipa fursa kuchangia Hoja ya kuahirishwa kwa Seneti kwa sherehe za Krismasi na mwaka mpya. Kwanza, ninapongeza Seneti kwa kazi ambayo tumefanya. Kazi hii imeangaziwa na Mratibu wa Waliowengi. Kwa hivyo, sitaguzia kila kitu tumefanya. Vikao vya mwaka huu vimeshuhudia mabadiliko ya uongozi wa Seneti kwa upande wa Waliowengi. Tulipata kiongozi mpya wa Waliowengi pamoja na Wenyeviti wa karibu Kamati zote za Seneti. Pia mimi nilibahatika kuchaguliwa kama Mwenyekiti The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, ... view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus