9 Jun 2020 in Senate:
Tarehe moja mwezi huu, nilizuru kituo cha matibabu pale the Technical University of Mombasa (TUM). Jambo la kusikitisha ni kuwa wagongwa wa COVID-19 walilalamika kwamba walikuwa wamefungiwa na hawakuwa na nafasi ya kutoka nje na kuzungumza. Endapo watarudi nyumbani, itakuwa shida kwa jamii kuwakubali kwa sababu tayari jamii imewatenga kwamba hawafai kujumuika na wengine.
view
9 Jun 2020 in Senate:
Katika kupambana na ugonjwa wa COVID-19, lazima tuondoe unyanyapaa. Bila kufanya hivyo, inamaanisha kuwa tutaendelea kuwatenga wagongwa wa COVID-19. Mwishowe, kila mtu atajitenga na mwingine.
view
9 Jun 2020 in Senate:
Bw. Spika, ijapokuwa sipongezi mfumo wa Rais Magufuli wa Tanzania, maisha yao yanakwenda vizuri. Watu wanakutana na kuswali misikitini au kusali makanisani. Juzi tarehe 31 Mei walikuwa na maombi. Sasa nchi yao haina visa vya COVID-19.
view
9 Jun 2020 in Senate:
Lazima tuwe na ujasiri wa kutowatenga watu hawa. Maelezo kutoka kwa World Health Organisation (WHO) yanasema kuwa baada ya muda wa siku saba au nane, mtu hawezi kuambukiza mwingine virusi vya korona. Haifai wawe wanatusomea statement kila siku saa tisa kutuelezea idadi ya walioambukiza na waliopona, wakati wale wanaoachiliwa kwenda nyumbani hawajui kama jamii itawakubali au la.
view
2 Jun 2020 in Senate:
Asante Mhe. Spika kwa kunipa fursa hii kumpa kongole Sen. (Prof.) Kamar kwa kuchaguliwa kwake kama Naibu Wa Spika wa Seneti. Kuchaguliwa kwake ni jambo kubwa sana katika nchi yetu kwa sababu tunaweza kuwapa mamlaka wanawake katika nchi yetu na kutambua kwamba kuna umuhimu wa wao kuwa pamoja na sisi katika kuongoza nchi hii.
view
2 Jun 2020 in Senate:
Nilibahatika kusafiri na Sen. (Prof.) Kamar kwenda Belgium, Mwaka wa 2018 kuhudhuria Mkutano wa African, Caribbean & Pacific Parliamentary Assembly (ACP). Ijapokuwa ilikuwa mara yangu ya kwanza, kupitia kwa ushauri na mwongozo wake, niliweza kuhudumu katika zile kamati nilizochaguliwa kule kama ambaye nilikuwa na uzoefu kabla ya hapo.
view
2 Jun 2020 in Senate:
Vile vile, yeye ni mfanyakazi kwa sababu katika mikutano tulioweza kufanya kule, mingine ilikuwa inaendelea mpaka saa tatu usiku. Tuliweza kuhudhuria yote na kuhakikisha kwamba mchango wetu katika mikutano ile umeweza kusikika. Vile vile, tuliona kwamba tulikuwa tumefanya kazi ya kueleweka.
view
2 Jun 2020 in Senate:
Kuchaguliwa kwake katika Bunge hili la Seneti na tukiangalia uzoefu wake, ina maana kuwa Seneti hii itasaidika pakubwa kwa uongozi ambao ataweza kuleta. Katika kila kazi kuna misukosuko, lakini tumeona kwamba Sen. (Prof.) Kamar kupitia kwa tajriba na elimu yake yote, yatamsaidia kuhakikisha kwamba, amevuka misukosuko ile.
view
2 Jun 2020 in Senate:
Ningependa kuwapa kongole wale wote ambao walikuwa wamejitokeza kuwania kiti cha Naibu wa Spika. Wote kama Maseneta ni watu ambao wanaweza kufanya kazi hiyo, lakini wakaamua na kuona kwamba Sen. (Prof.) Kamar anafaa zaidi kuliko wao. Hao pia tunawapa pongezi kwa uamuzi wao. Sote katika Bunge la Seneti tutashirikiana kuhakikisha kwamba maslahi ya wananchi wa Kenya na kaunti zetu yanawekwa mbele.
view
2 Jun 2020 in Senate:
Asante, Bi. Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii ili kuchangia Taarifa ambayo imeletwa na Seneta wa Nandi, Sen. Cherargei. Swala la mauaji ya kiholela na polisi limeongezeka pakubwa katika nchi yetu. Ningependa kutoa rambirambi zangu kwa wale wote waliyofariki mpakani wa Kaunti za Nandi na Kakamega. Tarehe 30 Mei, 2020, kule kwetu pwani tulipata kisa ambapo polisi waliwaua watu wanne akiwemo mwenye nyumba hiyo, Ramadhan Mohammed Chizwa na wanawe watatu baada ya polisi kuvamia nyumba yao usiku na kuwapiga guruneti na pia kuwapiga risasi wanawe wawili, akiwemo kijana wa miaka sita, Ramadani Chiswa and msichana wa miaka minne kwa ...
view