Mohamed Faki Mwinyihaji

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 1441 to 1450 of 2123.

  • 1 Dec 2020 in Senate: Kamati hizo zote zinaongozwa na viongozi shupavu kutoka upande wa upinzani wa Seneti. Hii imeongeza diversity katika Bunge hili kwa sababu viongozi ambao wamechaguliwa wote ni watendakazi, na itaboresha kazi ya Bunge hili zaidi. Ningependa pia kupongeza Bunge hili kwa kusimama kidete na kuenda mahakamani kutetea sheria zilizopotishwa bila mchango wa Seneti. Imethibitishwa na mahakama kuwa lazima sheria ifwatwe wakati Bunge la Kitaifa linapitisha sheria ambazo zitawaathiri Wakenya. Bw. Spika wa Muda, ninafurahi kwamba tulipitisha formula mpya ya third view
  • 1 Dec 2020 in Senate: ya ugawaji wa rasilimali za kitafia kwa serikali za ughatuzi na Serikali Kuu. Hii itachangia pakubwa maendeleo katika kaunti zetu. Kaunti ya Mombasa, ambayo ilikua inpoteza takirban Kshs700 millioni sasa imebahatika na kupata Kshs1 billioni zaidi katika mgao wa 2021/2022. Bw. Spika wa Muda, pia ningependa kughusia hali ya nchi ilovyo kwa sasa. Sasa tunapambana na janga la Korona, tumeona kwamba huu mlipoko wa pili umekuja kwa kasi. Watu wengi wamepoteza maisha yao kuliko katika mlipuko wa kwanza. Huu mlipuko wa pili umeonyesha dhahiri shahiri kwamba kaunti nyingi hazikuwa zimejitayarisha. Walipaka wananchi mafuta kwa mgongo wa chupa. Wengi hawakuwa wamejitayarisha. ... view
  • 1 Dec 2020 in Senate: Bado kuna visa vya maafisa wa polisi kula hongo na kusumbua wananchi hususan wale wanaosafiri. Kwa mfanao, katika Barabara Kuu ya kutoka Mombasa kuenda Lamu, kuna vizuizi karibu ishirini ambazo zinachangia kuongezeka kwa gharama ya kufanya biashara katika nchi yetu. Madereva hawawezi kupita vizuizi katika barabara zetu bila ya kuwacha chochote. Utaona pia kuna ubaguzi katika kusimamisha magari katika vizuizi hivyo. Kwa mfano, magari yanayobeba miraa na bidhaa zingine za haraka zinakubaliwa kupita kwa haraka bila kuzuiliwa kama bidhaa za kisawasawa zinazoenda kuwafaidi watu wa Lamu. view
  • 1 Dec 2020 in Senate: Bw. Spika wa Muda, tunapoenda katika mapumziko haya na tunapokaribia sherehe za Krismasi na Mwaka Mpya, watu wengi watakuwa wanasafiri kutoka sehemu The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate. view
  • 1 Dec 2020 in Senate: moja kwenda sehemu nyingine. Kwa hivyo ningependa kuwahimiza kuzingangatia kanuni zilizopo za kupambana na COVID-19 hivyo wanafaa kupunguza msongamano katika maeneo watakoenda kusherehekea. Nawahimiza Wakenya pia kuangalia kwamba kuna usalama wao binafsi na usalama wa wananchi wengine kokote watakapokuwa. view
  • 1 Dec 2020 in Senate: Maafisa wanaohusika na kulinda usalama lazima pia wawe macho kuhakikisha kwamba wananchi wanafwata sheria na vile pia wale wanaeka vizuizi vya uongo ili kuwagandamiza wananchi katika sehemu mbali mabli kule mashambani wanapelekwa mahakamani ili kuona sheria inafwatwa. view
  • 1 Dec 2020 in Senate: Bw. Spika wa muda, nachukuwa fursa hii kuwatakia Maseneta wote sherehe murwa za Krismasi na Mwaka Mpya. Ningependa pia kukupongeza kwa kutilia mkazo matimizi ya lugha ya Kiswahili katika Bunge hili. Nilifurahi sana wiki iliyokwisha--- view
  • 1 Dec 2020 in Senate: Bw. Spika wa Muda, nilifurahi sana wiki iliyokwisha kumuona kiongozi wangu wa waliowachache katika Seneti, Sen. Orengo, akizungumza kwa lugha ya Kiswahili. Sen. Orengo alizungumzia jambo muhimu ambalo tunafunzwa katika dini ya Kiislamu kwamba alama za mtu mnafik ni tatu. Ya kwanza akiweka ahadi, huvunja ahadi yake. Ya pili, akiaminiwa, hufanya hiana na ya tatu, akitoa ahadi, hawezi kutimiza. Asante Sana, Bw. Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii. view
  • 24 Nov 2020 in Senate: Thank you, Mr. Speaker, Sir, for giving me this opportunity to make a Statement regarding the alleged transfer of Kenya Ferry Services to the Kenya Ports Authority. I rise pursuant to Standing Order No.47 (1) to make a Statement on an issue of general topical concern, namely the alleged transfer of Kenya Ferry Services (KFS) to Kenya Ports Authority (KPA). The KFS is currently the most convenient link between the mainland south and Mombasa Island in Mombasa County. The last two weeks have been marred with allegations that plans are underway to transfer the functions of KFS to KPA. The ... view
  • 24 Nov 2020 in Senate: To date, 26 years later, the victims of the MV Mtongwe Ferry disaster have never been compensated. The proposed handing over of the KFS to KPA violates Article 186 and Schedule 4 (2) of the Constitution of Kenya, which provides that ferry services are functions of county government and should be transferred to the County Government of Mombasa. The Kenya Ports Authority Act gives KPA a specific mandate of managing the ports in Kenya, but does not extend this mandate to managing the operations of ferries. Over the years, the management and operation of KFS has deteriorated, largely because of ... view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus